Ufaulu wa darasa la saba wapanda kwa asilimia 4.76%

Ufaulu wa darasa la saba wapanda kwa asilimia 4.76%

Imany John

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
2,935
Reaction score
1,185
Matokeo ya darasa la saba yametangazwa na kuonesha wanafunzi 67567 wemefaulu sawa na asilimia 58.28% kati ya wanafunzi zaid ya laki tisa waliofanya mtiani huo mwaka huu.
Hivyo kufanya ufaulu huo kuwa umepanda kwa asilimia 4.76% ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.
 
hakuna cha laki tisa wala nini 58.28% ni wanafunzi 115935 tu ndio wamemaliza std 7 same on you tanzania wakati kenya hiyo ni number ya mkoa mmoja
 
Hivi huwa wanafaulu au wanahamishwa tu kwenda sekondari? Maana unakuta mwanafunzi wa form 1 au II hajui kunadika na kusoma alfu mnasema wamefaulu. Anyway, hongera kwa walichaguliwa na pole kwa walikosa maana ada ya private yataka moyo
 
hivi huwa wanafaulu au wanahamishwa tu kwenda sekondari? Maana unakuta mwanafunzi wa form 1 au ii hajui kunadika na kusoma alfu mnasema wamefaulu. Anyway, hongera kwa walichaguliwa na pole kwa walikosa maana ada ya private yataka moyo

chekecha mwenyewe...
 
hakuna cha laki tisa wala nini 58.28% ni wanafunzi 115935 tu ndio wamemaliza std 7 same on you tanzania wakati kenya hiyo ni number ya mkoa mmoja

nina mashaka na idadi uliyotaja mkuu, japo sina takwimu ya sasa, lakini hiyo mia moja, kumi na tano elfu, mia tisa thelathini na tano si sahihi kwani nakumba miaka kama sita hivi iliyopita tayari walikuwa wanahitimu watoto idadi kama hiyo. la zaidi ni kwamba hata hapa tanzania, idadi uliyoitaja ni kama ya mkoa. labda umechanganya na sekondari
 
nina mashaka na idadi uliyotaja mkuu, japo sina takwimu ya sasa, lakini hiyo mia moja, kumi na tano elfu, mia tisa thelathini na tano si sahihi kwani nakumba miaka kama sita hivi iliyopita tayari walikuwa wanahitimu watoto idadi kama hiyo. la zaidi ni kwamba hata hapa tanzania, idadi uliyoitaja ni kama ya mkoa. labda umechanganya na sekondari

Source:Tbc saa 10 leo
 
hakuna cha laki tisa wala nini 58.28% ni wanafunzi 115935 tu ndio wamemaliza std 7 same on you tanzania wakati kenya hiyo ni number ya mkoa mmoja

Hiyo idadi ya wanafunzi ulioandika hapo juu co sahihi.cna uhakika sana lkn wanafika mpaka laki laki nane waliomaliza darasa la 7 mwaka jana.
 
sijayaona kwenye website, mwenye direction ya kuyaona msaada tafadhali
 
Hivi huwa wanafaulu au wanahamishwa tu kwenda sekondari? Maana unakuta mwanafunzi wa form 1 au II hajui kunadika na kusoma alfu mnasema wamefaulu. Anyway, hongera kwa walichaguliwa na pole kwa walikosa maana ada ya private yataka moyo

Umenena mkuu. Hayo ni matokeo ya kupima ubora wa elimu kwa kigezo cha "quantity "
 
hivi bado kuna aliyemaliza la 7 na akafeli?! Basi huyo atakuwa kilaza kwelikweli
 
Kwa hesabu za kuchagua ilitegemewa kiwango kipande zaidi ya hicho, maana nina imani hakuna aliyepata 0 ya somo hilo
 
updates,

Mitihani ya Darasa la Saba
yachakachuliwa

WANAFUNZI 9000 WAFUTIWA
MATOKEO, HATA WALE
WATAKAOINGIA KIDATO CHA
KWANZA KUPIMWA UWEZO
WAO UPYA

WIZARA ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi imetangaza
matokeo ya mitihani ya darasa
la saba ikieleza kuwa wanafunzi 9000 wamefutiwa
matokeo kutokana na
udanganyifu na hata wale
ambao watapangiwa shule za
sekondari wapimwa uwezo
wao kabla ya kuanza masomo. Akitangaza
matokeo hayo jijini Dar es
Salaam jana, Naibu Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philipo Mulugo pamoja na
mambo mengine, alisema kutokana na tatizo hilo,
wanafunzi waliochaguliwa
kujiunga kidato cha kwanza
mwakani, watapaswa
kuchujwa upya. “Baada ya udanganyifu
kuongezeka mwaka huu,
tumeanzisha utaratibu huu ili
kuwabaini wanafunzi
wanaingia kidato cha kwanza
wakiwa hawajui kuhesabu, kusoma wala
kuandika,"alisema Mulugo. Mulugo alisema wanafunzi
waliofutiwa mtihani huo ni
9,736 na utaratibu wa kuchuja
wale waliochaguliwa kujiunga
na Kidato cha Kwanza utaanza
rasmi Januari mwakani. Kuhusu wanafunzi
kudanganya, alisema Wizara
imegundua kuwapo kwa aina
nne za udanganyifu ikiwamo
wanafunzi 94 kukutwa na
majibu katika karatasi, rula na viatu. “Watahiniwa wanne
walibainika kuandikiwa
majibu ambapo ilionekana
miandiko zaidi ya mmoja
kwenye karatasi ya
mtahiniwa mmoja. Wataalamu wa masuala ya
maandishi wamethibitisha
suala hilo,’’alisema Maugo na
kutaja udanganyifu mwingine
kuwa ni wanafunzi tisa
kurudia darasa la saba kinyume na taratibu. Alisema
aina nyingine ya udanganyifu
waliougundua ni kuwapo kwa
wanafunzi 9,629 waliokuwa
na mfanano usio wa kawaida
katika kukosea majibu ya maswali. Manyara kinara wa
kuchakachua
Waziri Mulugo alisema Mkoa
wa Manyara ndio unaoongoza
kwa kuwa na idadi kubwa ya
wanafunzi waliofutiwa matokeo. Alisema Mkoa huo
una wanafunzi 1, 573
waliofutiwa matokeo,
ukifuatiwa na mikoa ya
Arusha (1,012) na Lindi (63). Akizungumzia kiwango cha
ufaulu, Waziri Mulugo, alisema
mwaka huu kimeongezeka
kwa asilimia 4.76. Kiwango
kimepanda hadi asilimia 58.28
kutoka asilimia 53 .52 ya mwaka jana. Mulugo alisema
wanafunzi waliofanya mtihani
huo walikuwa 983,545 na
waliofaulu ni 567,567.
"Wasichana waliofaulu ni
278,377 sawa na asilimia 54.48 na wavulana ni
289,190 sawa na asilimia
62.49," alisema. Waziri Mulugo alisema katika
kundi la wanafunzi wenye
ulemavu, waliofaulu ni 355,
kati yao wasichana ni 159
sawa na asilimia 44.79 na
wavulana 196 sawa na asilimia 55.21.
Waliochaguliwa kidato cha
kwanza Waziri Mulugo
alisema kati ya wanafunzi
567,567 waliofaulu,
wanafunzi 515,187 sawa na asilimia 90.1,
wamechaguliwa kujiunga na
kidato cha kwanza katika
shule za Serikali huku na
52,380 hawakupata nafasi.
"Wasichana waliochaguliwa ni 253,402 sawa na asilimia
49.1 na wavulana 261,785
sawa na asilimia 50.9,"
alisema. Ufaulu kwa kila somo Mulugo
alisema kuwa viwango vya
ufaulu katika masomo ya
Kiingereza, Hisabati na
Sayansi, vimeongezeka
ikilinganishwa na matokeo ya mwaka jana. "Kiwango cha
ufaulu kwa somo la
Kiingereza kimeongezeka kwa
asilimia 10.23 kutoka asilimia
36.47 ya mwaka uliopita hadi
asilimia 46.70 mwaka huu," alisema. Naibu Waziri huyo alisema
kuwa tofauti na mwaka jana,
wahitimu wa mwaka huu
wamefanya vizuri katika
somo la Hisabati, hivyo
kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 24.70 hadi
asilimia 39.36 mwaka huu. Alisema katika somo la
Sayansi ufaulu umekuwa hadi
asilimia 61.33 kutoka asilimia
56.05 mwaka jana. Mulugo
alisema viwango vya ufaulu
kwa masomo ya Kiswahili na Maarifa ya Jamii
vimeporomoka kutoka
asilimia 71.02 hadi asilimia
68.58 kwa Kiswahili na
kutoka asilimia 68.01 hadi
54.85 kwa Maarifa ya Jamii.
Source:mwananchi
 
Jamani Great Thinkers tunaomba hayo matokeo kutoka source yoyote
 
Back
Top Bottom