Ufaulu wa somo la Hesabu kidato cha nne 2022

Ufaulu wa somo la Hesabu kidato cha nne 2022

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,092
Reaction score
5,386
Nilisikia kupitia radio one leo asubuhi kuwa, takribani asilimia 70 ya watahiniwa wa kidato cha nne wamepata alama sifuri katika somo la Hesabu?

Kama ni kweli, nafikiri hakuna haja ya kutafuta Mchawi kwani tatizo liko wazi kabisa ambalo ni ukosefu wa Waalimu wenye sifa ya kufundisha somo la hisabati katika shule za Msingi (hata wakipeleka wenye Diploma huko msingi bila kuweka kigezo cha umahiri wa Hesabati haitasaidia) lakini pia kuna upungufu mkubwa wa waalimu wa Hesabu katika shule za sekondari. Sababu nyingine tofauti na ukosefu/upungufu wa waalimu adhari yake ni chini ya 10% hivyo sio za kipaumbele....

Naamini bila hisabati/hesabu, mambo mengi hayaendi hivyo ni vizuri tuwekeze huko bila kuchanganya na Siasa
 
Waalimu wapo ila hako kamshahara kakawapa akili ya kulima hata vitunguu ili wapate kipato kizuri. Hebu anzeni kuwapa hao waalimu marupurupu kama kazi nyingine muone mabadiliko.
 
Nimesikitika Sana.... Kama hii habari Ni kweli
 
Tunatengeneza taifa la hovyo sana kwa baadae.
 
Nilisikia kupitia radio one leo asubuhi kuwa, takribani asilimia 70 ya watahiniwa wa kidato cha nne wamepata alama sifuri katika somo la Hesabu...
Ni kweli changamoto zipo, ila hata malaika ndio wangekuwa waalimu wa hesabu hawa wanafunzi wa Instagram wangefail vile vile.

Haya masomo ya hesabu, fizikia, kemia na baiologia yanahitaji determination aisee na kupiga msuli hasa. Maana walimu husaidia only 20-30% ya ufaulu wako the rest ni misuli yako mwenyewe.
 
Wanafunzi zaidi ya 400,000 wamepata F, afu twasingizia tatizo Lugha
 
Yaap! Ukweli mtupu, somo la hesabu halina walimu mahiri ngazi ya msingi. Na wanaobabaisha wanarukaruka mada kama jometri na aljebra na zingine zenye kuhitaji ukokotozi wa thamani. Tatizo hili pia lipo zaidi ngazi ya sekondori, mada kama sequence and series na nyingine zinazofanana na hizo huogopwa kufundishwa kwa walimu wasio mahiri kwa somo hilo. Kuna walimu wanajititimua kufundisha somo wasilokuwa na umahiri nalo hawataki kusaidiwa kufundisha wasionekane hawajui kitu, matokeo yake huruka mada. Kama vipi serikali iruhusu watu wasio walimu wenye umahiri wa kufundisha hesabu hata kwa mkataba mfupi ili kupandisha ufaulu wa somo hilo. Mbinu za kufundisha somo hilo zipo nyingi
 
Walimu ni wengi kwenye ajira hiyo ila wanaochukua masomo ya sayansi na hesabu ni wachache. Unakuta walimu wanaishia darasa la nne kufundisha hesabu wanagombania. Ikifika darasa la tano mada zinaongezeka wanaanza kuogopa kupanda juu kwenye ukokotozi zaidi. Hata mbinu ya kualika mgeni kufundisha mada ambazo mwalimu haimudu haitumiwi. Somo la hesabu ni rahisi sana kufundisha na kueleweka ila limekosa walimu mahiri. Serikali ifanye mkakati wa kufundisha somo hilo kwa kila ngazi ya shule msingi na sekondari kwa kuwapa semina za wiki nzima mara kwa mara kwa walimu wanaofundisha somo hilo. Ikiwezekana waaineshe mada ngumu walimu wakafundishwe seminani. Kama vipi NECTA itunge mtihani kwa kila ngazi ya shule na walimu wote wanaofundisha somo hilo wafanye. Watakaopata chini ya asilimia themanini watathiminiwe kama wana uwezo wa kufundisha somo hilo. Hiyo hiyo mitihani wanayotungiwa wanafunzi na walimu wafanye
 
Walimu wengi wamekariri maswali ukikwepesha tu umewajamata.

Ni wakati serikali iwafanyie Usaili Walimu ili kulinda Elimu yetu
 
Multiple choice mbaka mathematics sio 🤷‍♂️

_20231123_191055.JPG
 
Back
Top Bottom