Sababu kubwa za Ajali ni Barabara za Nyembamba sana na Madereva wazembe...na si Magari yalio nyuma ya ten years...
Barabara zote zinazotoka DSM kwenda mikoani sio nyembamba, zimejengwa kwa viwango vya kimataifa, tofauti ni kwamba barabara zetu ni single lane. Pamoja na kuwa sehemu kubwa ni single lane, barabara toka DSM hadi Morogoro kuna sehemu wameweka double lane kwa ajili ya magari kujapita magari yaendao taratibu. Sehemu hizo ni zile zenye milima, ambapo advantage ya double lane inatolewa kwa magari yanayopanda mlima.
Tatizo la ajali TZ bado linaendelea kuchunguzwa linasababishwa na nini. Miaka 20 iliyopita wakati Tz ikitegemea usafiri wa mashirika ya mabasi (KAMATA, KWACHA, RELWE n.k) mabasi yalikuwa yakisafiri usiku. Na hata watu binafsi (mtu mmoja mmoja) waliopoanza kusafirisha abiria, ratiba ilikuwa ni usiku.
Mabasi yakaongezeka ya kila aina, toka ordinary bus, Luxury bus na express bus. Kila aina ya Mabasi ikaonekana TZ, Leyland CD(kinanda),Leyland Victory, Leyland DAF, M.Benz, Volvo, Scania n.k. Sasa soko la kisafirisha abiria likawa wazi na lenye ushindani mkubwa. Ajali zikaongezeka maradufu.
Ajali ya bus moja ambalo lilikuwa likisafiri kati ya DSM na Dodoma, ndio ikabadilisha ratiba ya usafiri kutoka usiku hadi mchana. Ratiba hiyo ni kusafiri kati ya saa 12 asubuhi hadi saa nne usiku. Iwapo basi litakuwa njiani saa tatu usiku ni lazima lisimame na kulala hadi kesho yake asubuhi, hata kama litakuwa limebakisha km 50 kufika kituo chake cha mwisho. Ratiba hii ipo hadi leo.
Pamoja na utaratibu huo mpya bado ajali zikaendelea kutokea, hatua zaidi zikazidi kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kufunga vithibiti mwendo, na kuwekwa matuta barabarani. Hata hivyo ajali bado zinaendelea kuwepo, na bado njia za kutafuta uvumbizi wa tatizo hilo zinaendelea, ikiwa ni pamoja na hatua ya sasa ya kuzuia magari yaliyotumika zaidi ya miaka mitano. Hatua ambayo mimi binafsi naiunga mkono, kwani ni mdau wa usafiri wa mabasi.
Tatizo ambalo naona linachangia ajali ni muda wa kuendesha gari. Ninavyojua kuwa dereva anatakiwa kuendesha gari kwa saa nane tu kwa siku. Lakini sio kwa madereva wa mabasi wa TZ kwani wengi wanaendesha zaidi ya masaa hayo. Matokeo yake wengi huchoka hivyo ni rahisi kusababisha ajali.
Kwa mfano toka DSM hadi MWZ ni zaidi ya km 1000, kwa mwendo wa km80 kwa saa, ina maana basi hilo litasafiri kwa masaa zaidi ya kumi na mbili, na dereva ni mmoja hivyo baada ya masaa nane ya kuendesha busi hilo lazima atakuwa amechoka tu. Hali hii ipo kwa mabasi ya DSM-MBY, DSM-RUVUMA n.k
Wakati wa Relwe na KAMATA, safari ya kwenda Songea tokea DSM ilikuwa na madereva watatu, Relwe toka DSM kwenda Mbeya ilikuwa na Madereva watatu. Basi la KAMATA toka DSM kwenda Arusha lilikuwa na Madereva wawili. Hii kwa kiasi kikubwa ilitoa nafasi kubwa kwa madereva kupumzika na kuendesha basi kwa uangalifu mkubwa. Aidha mabasi yao yalikuwa katika viwango vya hali ya juu na salama kabisa(kabla ya kuanza kufilisika).