UFISADI Kila Kona: Baraka za CCM KINGA ya Ufisadi BoT na Viongozi Mafisadi

duh.. yaani nimefikia 7000? duh I need to take a break.. ndio maana vidole vimevimba!
 

I read something similar in this week's Raia Mwema. It is an article by Lula wa-Ndali...
 
I love words.. I sure do.. na hapa bi mdogo umenigusa kumoyo.. yaani hiyo simile yako hapo juu imenifanya ubongo utetemeke kwa furaha.. "kuona moto katikati ya ukungu mzito wa theluji".. it is so oxymoronic..

...acha kuleta mapenzi ya usingizini,watu tuko kazini hapa kupambana na mafisadi ebo!
 
Huyo jama aliyeandika hiyo article anaonekana ni mtu smart sana na anafikiria kama mimi...Kitula na Mnyika wako wapi watuambie nani anasimamishwa na chadema ili nimchangie pesa za kampeni,nimechoka na mafisadi!
 
hii mbona bado inafuka moshi.watanzania hatubebeki hata kidogo sijui mungu tulimkosea nini.
 
Nimefurahi sana kuwa hapa unaona kuwa ccm "ndio mhimili mkubwa wa matatizo", halafu kuleeeeee huoni nyerere anahusika vipi, wakati uongozi wa ccm ni hand-picked na nyerere au hufahamu kuwa bwana JK alikwisha chaguliwa na nyerere tokea uhai kuwa ashike awamu ya nne? au huijuwi system ni nini?
 

Zomba,

Nyerere alitoka serikalini zaidi ya miaka 20 iliyopita. The guy has been dead miaka 9 sasa. Haya ya system inayoongozwa na watu waliokufa ni very dumb excuse kwangu. Kama wewe unataka kuanza ugomvi na kusingizia kila matatizo yako kwa mtu aliyekufa miaka yote hii wewe endelea tu mkuu.

Mimi ninaendeleza makombora kwa mafisadi walio hai leo hii bila kujali kuwa wamewekwa na dikiteta Nyerere au Kenyatta. Kitu kimoja nimekiweka wazi hapa ni kuwa mimi ni mpinzani wa ccm. Hakuna kitu wapinzani wa CCM tungependa kama kufutwa kabisa kwenye historia ya Tanzania jambo lolote zuri kuhusu Nyerere na kuwekwa mabaya yote kuhusu Nyerere ili kupunguza influence ya Nyerere huko vijijini.

Kama nilivyosema katika ile thread ya udikiteta wa Nyerere (ambayo nilianzisha mimi), mimi ndio ningekuwa na sababu kubwa sana ya kumpondea Nyerere hapa kwa vile huwa nakutana na wazee huko vijijini ambao ukiwatamkia ccm wao wanakumbuka mazuri ya Nyerere. Binafsi kama mtu niliyetaka Mrema awe Rais mwaka 1995 nina kila sababu ya kutompenda Nyerere kwa vile alimpigia kampeni Mkapa. Wengi tunajua yaliyotokea zanzibar mwaka 1995.

Kwa nini basi sipotezi muda kumpondea Nyerere?

1. The guy has been dead miaka 9 sasa.
2. Nitakuwa kichaa kuamini kuwa mtu aliyekufa bado yuko hai
3. Nitakuwa paranoid kukimbia system ya mtu aliyekufa
4. Nimejifunza ku-take responsibility badala ya ku-shift blames
5. Nimeshuhudia machimbo zaidi ya 10 yakiuzwa baada ya Nyerere
6. Siwezi kufanya kazi vile unavyotaka wewe
7. Kasome tena thread ya udikiteta wa Nyerere uone maoni yangu
 
Lula wa Ndali:
Surely, one of the few masterpieces on JF, ever.

Lugha imenyooka vizuri. Napendekeza nakala zitumwe vijijini wananchi wajisomee wenyewe.
That is the minimum we can expect for now.
 
jamani alichosema mleta hoja ni ukweli usiopingika hata kidogo.

Matatizo makubwa ni sisi wadanganyika ambao tunawapigia kura wezi hawa wa CCM. Kama kwa pamoja kabisa tutakataa kuwapa kura mafisadi hawa wa CCM tusingefikishwa hapa tulipo leo hii.

Hivyo ndugu wanabodi tuanze kampeni ya nguvu kabisa kuwafahamisha wadanganyika wenzetu kuwa sasa inabidi tuamke tusiwape tena kura CCM ni bora kuongozwa na jiwe kuliko mafisadi haya.

TAFADHALI NDUGU ZETU WA KITETO MSIIPIGIE KURA CCM HATA WAKIMWEKA NANI KATIKA KUGOMBEA KITI HICHO.
 
Binafsi nimeguswa, na niko tayari kuunga mkono hili la kuchukua Kiteto.. sasa wapinzani waanze mchakato wa kupata mgombea wao.. na wahamishe kambi yao Kiteto.. hakuna cha Dar wala nini wote kiteto.. !
 
sasa hapo safi na ndio mambo ya kuongea maana hii mifisadi hailali,dawa ni kuhamia kiteto wapinzani wote na watashinda tuu!
 
Du! Tatizo la wabunge wa CCM ndugu zangu ni kubwa kuliko tunavylitazama! We angalia kama utaona Mbunge yeyote pale. Hakuna Mbunge hata mmoja, wengi wanaingia pale kwa maslahi binafsi tu. Wafanyabiashara wa 'harmu' wengi wameingia CCM na kugombea ubunge! unadhani hao ndio watatetea wananchi? Wengi walitoa hela yao nyingi sana kuununua ubunge hivyo wanakuwa na kazi moja tu, kurdisha hela yao na faida juu!

Mimi napendekeza tuungane kuanza humu tuelimishe wananchi kuhusu ubaya na madhambi ya hicho chama. Ni chama ambacho kimechangia matatizo ya nchi hii kwa asilima 100! Leo hii bado hata umsimsmishe mbumbumbu mzungu wa reli ukasema nai mwana ccm tu wananchi wanamwaga kura zao! Kama tukielimika tutafika mahali bunge letu litakuwa kama la Kenya, na hapo tutona kasi ya maendeleo ya nchi yetu.

CCM inawadanganya wananchi kwamba ukichagua wapinzani itatokea fuja na kwa sababu wananchi wengi hawana uelewa wa kutosha, basi wanaamini. Wengi wetu tunahongwa vitu vidogo sana, kama kanga na mlo wa mchana tunapiga kura ambayo mwisho wa siku itakuwa imeongeza mafisadi. Mwisho wa haya umewadia!!!!
 
Hatujamkosea Mungu, na kwa kweli angeweza kuwaadabisha hawa Mafisadi wetu big time. Tatizo Wabongo wanamchanganya Mungu, kila anapotaka kuwaadhibu hawa mafisadi anasikia Wabongo hao hao wakiimba 'Mungu Ibariki Tanzania na Viongozi wake' tena wanaimba kwa unyenyekevu mkubwa, hivyo anashindwa asikilize ombi lipi la Wabongo, kubadiliki viongozi ambao ni mafisadi au kuwaadhibu.
 
Hatujamkosea Mungu, na kwa kweli angeweza kuwaadabisha hawa Mafisadi wetu big time. Tatizo Wabongo wanamchanganya Mungu, kila anapotaka kuwaadhibu hawa mafisadi anasikia Wabongo hao hao wakiimba 'Mungu Ibariki Tanzania na Viongozi wake' tena wanaimba kwa unyenyekevu mkubwa, hivyo anashindwa asikilize ombi lipi la Wabongo, kubadiliki viongozi ambao ni mafisadi au kuwaadhibu.
 
jamani viongozi wetu wawe na huruma ! watu wanabadilika sana na Misifa yote ya balali leo huwezi kuamini maana jamaa mapesa yalimgeuza kuwa mdudu! nadhani wapo wengi wa aina Hii
 
Jamani,

Wiki hii nimekaa sana nimetafakari, nimegundua kwamba karibu viongozi wetu wote ni mafisadi. Viongozi wakuu wametajwa kwenye JK eleven. Na karibu kila anayeteuliwa unakuta naye ana ufisadi wake. Hivi ni kiongozi gani wa serikali ya sasa na taasisi zake ambaye sio fisadi? Sasa kama ugonjwa wa ufisadi umesambaa kiasi hiki kwa nini tusiache tu mafisadi wote wajifie wazaliwe watanzania wengine wachache? Hivi hii si ishara kwamba wananachi watanzania waliowengi ni mafisadi ndio maana ufisadi ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku? Sasa kama sisi tumeshindwa kuacha ufisadi kwa nini tuwatake viongozi waache ufisadi? Hivi kwani tukaiacha tu nchi ikawa taifa la mafisadi kwani tutapata hasara gani? Si kila mtu atanufaika na ufisadi wa mahali pake? au dawa ni kukiondoa tu Chama Cha Mafisadi(CCM)?

Asha
 

Mimi sioni ubaya wa yeye kuchukua mkopo mkubwa kwa kuwa kwanza ni njia halali na pia ukumbuke kuwa ni njia ya kuwasaidia na wananchi wengine mbao kwa uwekezaji wake wamepata ajira na zaidi ya yote wananchi wamepata elimu ya ufugaji wa kisasa kwa vitendo.Nadhani tatizo ni wale viongozi kama Sani Abacha,Mobutu na wengineo ambao wanaiba na kwenda kuwekeza ktk mabenki ya nje.Winzi wa Mzindakaya ni sustainable.
 
Tafakuri butu -ve kama hii ktk jamii hii yetu ya Taifa Changa kama hili lenye Umri wa Miaka arobaini na ushee ni hatari kua na watu kama wewe.

Kauli hii yako na nikiangalia Kibwagizo chako inanionyesha kua chadema ni chama cha watu wenye mawazo butu na waliokata tamaa ya maisha ni hatari.

Ila kazi yetu sisi CCM ni kuleta mapinduzi ya Fikra ambayo tunajitahidi kuyaleta.

Jitahidi kuacha kutafuta majibu rahisi na tafakuri rahisi kama hivi na UGUNDUZI unaodai umegundua ni hatari kwa Afya ya chama chako.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 


Sasa una mkejeli nani kwa kujiita fisadi mtoto!? Unadhani ufisadi ni sifa nzuri!? 😕

Baba yako nani katika mafisadi hawa!? Mkapa, Ballali, Mzindakaya, au Mkono.

Utaonaje ubaya wakati wewe ni fisadi mtoto? Tangu lini BOT ikatoa mikopo kwa watu binafsi na siyo benki za biashara?

Moderators hili jina kwa maoni yangu lipigwe marafuku hatuhitaji watu kutumia majina kuwakejeli Watanzania katika hii vita ya kupambana na mafisadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…