NAMTUMBA
JF-Expert Member
- Feb 20, 2014
- 1,939
- 597
Naomba msaada wakisheria nataka kuliburuza jeshi la polisi Mahakamani.
1. Polisi ni wazushi wa matukio ya uongo. Mfano: Ugaidi wa Tanga.
2. Wanatumia mamilioni ya kodi za wananchi kutengeneza video za kizushi kwa manufaa ya mafisadi wachache ndani ya ccm. Mfano: video ya Rwakatare na video ya Ugaidi ya Bin Abdullah.
3. Matumizi mabaya ya Silaha. Sote tunafahamu kwamba silaha ni zagarama kubwa sana na serikali inanunua silaha kwa kodi za uma kwa lengo la kulinda raia na mali zao lakini Kwa muda mrefu jeshi la polisi limekuwa likitumia silaha ovyo ovyo paspo na ulazima hasa katika mikusanyiko halali ya wananchi name pengine kupelekea mauaji ya RAIA wasio na hatia. Mfano: Nyololo alipouawa Mwangosi, Mkusanyiko wa CUF Mbagala zakihemu.
4. Kuna kikundi maalumu cha vibaka na waporaji ndani ya jeshi la polisi ambalo linatumia pikipiki kuzunguka huku na kule kwa kisingizio cha kufanya doria wakati sikweli, hawa jamaa kwasasa wamejipa hatimiliki yakunyanyasa bodoboda na bajaji.
Sitetei bodaboda na bajaji lakini tatizo la kundi hili ni matumizi mabaya ya pikipiki za serikali na mafuta ya serikali kinyume na malengo yaliokusudiwa.
5. Kuna kundi la matapeli upande wa askari wa usalama barabarani ambao wanatumia vipima mwendokasi (speedometer a.k.a Torch). Hawa wanatapeli madereva wa magari tena wanauonevu sana. Lengo la vifaa hivi ilikuwa ni kudhibiti ajali lakini kwasasa ajali zimezidi kwasababu madereva wengi wanajaribu kufidia muda waliopotezewa na askari wa barabarani pindi wanapobambikwa kesi. Haya matumizi mabaya ya Mali za uma.
Kwa hayo maelezo machache hapo juu na mengine ambayo nitayasema mbele ya mahakama naomba msaada wakisheria nataka kulishataki jeshi la polisi mahakamani.
Ee Mungu ibariki TANZANIA.