MANDINGO 1961
New Member
- Oct 14, 2024
- 1
- 1
Kiwanda hicho ambacho ni mali ya serikali kwa sasa hakifanyi kazi kimeuzwa kwa thamani ya shilingi bilioni 3 wakati thamani halisi ya kiwanda hicho ni zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 157 kwa mujibu wa uthamini uliofanyika mwaka 2023.
Vile vile nyumba 4 zinazomilikiwa na kiwanda hicho mbili zikiwa Kinondoni Ananasifu na mbili zikiwa Regent estate zenye thamani ya shilingi za kitanzania billion 3.5 zimeuzwa kwa shillingi billion 1 zote nne kwa kampuni inayoitwa IPILINGA PANYA ya jijini Dar-Es-Salaam.
Habari za kuaminika ni kwamba maelekezo ya kuuza mali hizo yametolewa na kusimamiwa na msajili wa hazina ndugu Nehemia Mchechu licha ya pingamizi la kutouza mali hizo lililowekwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara, Shirika la Nyumba NHC linatumika vibaya kama kichaka cha kufichia ufisadi huo.
Katika hali ya kushangaza NHC wamenunua majengo hayo lakini hawakununua madeni ya URIFIKI na kutoshirikisha uongozi wa kiwanda hali inayosababisha sisi wafanyakazi tukipata tabu ya kutolipwa mishahara yetu yenye thamani ya shilingi bilioni tano na milioni mia sita licha ya kushinda kesi mahakamani mwaka 2020.
Tuna imani na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwamba atasimamisha uuzwaji wa mali ya umma kifisadi namna hii na kiwanda hicho kufufuliwa ili kulinda mali za umma na kuwarejesha kwenye ajira zao wafanyakazi walioko mitaani ambao hapo awali walikuwa wakitumikia kiwanda hicho chenye historia kubwa nchini na hao mafisadi kuchukuliwa hatua zinazostahili ikiwemo kufanyika uchunguzi wa kina kuhusiana na ufisadi huu unaolalamikiwa sana na wananchi hasa kipindi hiki kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.