Janja weed
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 3,000
- 5,606
Kuna ufisadi mkubwa unaendelea wakala wa mwendokasi ambao unahusisha wanaojiita wataalam wa tehama, iko hivi kuna mfumo unaandaliwa wa ukusanyaji nauli kwa njia ya kielektroniki ambao kwa sasa haujakamilika na una zaidi ya mwaka mmpoja sasa.
Mfumo huo unatengenezwa na wakala wa mwendokasi na wataalam wengine wa serikali wakiwemo kutoka e-governmrt na kampuni moja ya kisanii ya kihindi. Kimsingi huu ni ufisadi kwa sababu tangu mfumo huo uanze kutengenezwa haujakamilika na wala haujulikani utakamilika lini ,kinachofanyika ni mamilioni ya pesa za umma yanaliwa na watun hao wanaojiita wataalam, na kimsingi wala hautakamilika kwakuwa ni mradi wa watu wa kupiga pesa.
Najiuliza hivi serikali imeshinmdwa kutafuta mtaalam ambaye angeweza kutengeneza mfumo huo kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi? Kwanini mfumo tu wa kukusanya nauli utengenezwe kwa zaidi ya mwaka mzima? Je, ulaji huo wa pesa za umma una tija gani kwa serikali ukizingatia wakala wa mwendokasi wenyewe uko taabani kimapato? Wahusika wanakaa kwa kupokezana katika eneo la chuo cha uailimu Morogoro ambako ndiko wasanii hao wanakaa wakijidai wanatengeneza mfumo.
Piga mahesabu watu 20 wanakaa mwaka mmoja nje ya kituo cha kazi wanalipwa 100,000 kwa siku Ukipiga mahesabu watu 20X siku 30 Mwezi mmoja huo X 12 Mwaka mmoja huo unapa milioni 720 hapo hujaweka gharama za chakula stationeries vifaa vya kujifunzia, mtandao na kadhalika. Kwa Serikali hii ya JPM inayojinasibu kubana matumizi ka kuziba mianya ya Rushwa kwa kutumia vyombo vyake imeshindwa kuona kama huu ni ufisadi wa kutisha?
Kazi hiyo haitarajii kuisha leo wala kesho na itaendelea hata miaka mianane ili tu watu waendelee kupiga hela huku wasafiri wakikosa huduma ya kadi za kusafiria. Tehama imekua sana na kuna wataalam wabebezi ambao wangeweza kutengeneza mfumo huo kwa gharama nafuu sana kuliko kinachoendelea hivi sasa