UFISADI: The Making Of IPTL

how many times will sue us before we are able to come back to our senses?
 
However, since January last year, Tanesco stopped paying the capacity charges after discovering that IPTL had not injected equity payments since commencement of the project as a determining factor for capacity charge payments.

Hii issue si ni kama ya Richmond-Dowans tu? Maana kwenye issue hiyo kulikuwa na breach of contract on the Richmond side na ndio ikaja sababisha mkataba wao uvunjwe. Kama na akina IPTL wame-breach contract, then ina-make more sense for Tanesco ku-apply style iliyotumika katika issue ya Richmond-Dowans na kuubatilisha pia huu mkataba wa IPTL.
 
Hawa IPTL ingekuwa katika nchi ya kidikteta kama vile Iraq ya Saddam wangefungishiwa virago vyao mara moja au kuswekwa lupango na kutupa ufunguo baharini. How can we pay for something we are not receiving?
 
Hawa IPTL ingekuwa katika nchi ya kidikteta kama vile Iraq ya Saddam wangefungishiwa virago vyao mara moja au kuswekwa lupango na kutupa ufunguo baharini. How can we pay for something we are not receiving?

Wala haihitaji kuwa kwenye nchi ya kidikiteta, nchi nyingi za amerika ya kusini zimekuwa zinavunja mikataba kila mara inapojulikana kuwa kuna matatizo. Hata marekani kwenyewe walishikia bango mkataba wa kampuni moja ya dubai hadi ikajitoa na hakuna yeyote aliyewatuhumu kuwa wapinga ubepari.

Uoga wetu watanzania na ubinafsi wa viongozi wetu ndio unatupumbaza.
 

Hapa issue si uoga.. Issue ni kulinda ulaji...
 
Ulaji ambao unaiua TANESCO na kuwabebesha gharama kubwa za bei ya umeme Watanzania ambazo hawastahili kubebeshwa gharama za mikataba ambayo haina maslahi kwa Watanzania. Tanesco na serikali lazima wapambane na hawa jamaa ili ama wapunguze kwa kiasi kikubwa gharama za mkataba huo au wafunge virago vyao na kurudi kwo Malaysia.
 
The Tanzania Electric Supply Company (Tanesco) ended up paying the Malaysian firm - Independent Power Tanzania Limited - more money in capacity charges than what was actually due to it, the Minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, has said.

The minister said the dispute between the local utility firm and its Malaysian partner was basically one over bloated figures which the IPTL was claiming in capacity charges – some $86.54 million instead of only 50,000/- in proposed equity charges.

The minister clarified in Parliament here that the dispute between the government and IPTL is in principle based on that matter. “Tanesco has been paying more than the proposed capacity charges … and that is the main issue under dispute,” he said.

Mr Ngeleja made the comments in Parliament yesterday when presenting his ministry’s budget estimates for the 2008/2009 financial year, under which he requested for 362,922,265,600/- for both recurrent and development budgets.

The International Centre for Investment Disputes in 2001 ruled that capacity charges would be calculated at 30 per cent equity and 22.31 per cent of profit. “The amount of equity used then was $86.54 million but Tanesco later launched an investigation … it was then deduced that the proper equity was only 50,000/-,” he said.

The minister also said that Tanesco would start generating 100MW at its Ubungo plant in Dar es Salaam beginning next month. He said that the electricity generated at Ubungo is part of government efforts to enhance power generation in the country. “The government had also decided not to renew the contract with Alstom Power Rentals after it expired in March … and the contract with Aggreko ends in November this year,” he said.

The government, he said, reached an agreement with the World Bank in January this year to implement the Tanzania Energy Development and Access Expansion Project (TEDAP), whose implementation started last April. The project aims at improving the electricity transmission and supply systems in Dar es Salaam, Arusha and Kilimanjaro regions at a cost of $85.8 million.

Mr Ngeleja also said that the project will increase off-grid electrification by using natural energy to be used by institutions, domestic use and production activities at a cost of $22.5 million. The minister also said that talks were in progress between the government and an investor to construct a petroleum refinery in the country.

“The government is at the moment also assessing the company, Noor-Oil and Industrial Technology (NOIT) … the government will give NOIT the go-ahead to conduct a feasibility study once we get satisfactory feedback,” he said. Between July 2007 and June this year, he said, the government has signed contracts with three companies to explore for petrol in Ruvu, north of Songo Songo and north of Mnazi Bay. Mr Ngeleja also said that there are now 20 foreign companies exploring for uranium in the country. He said that the government will come up with a policy and legislation guiding uranium mining in the country.


Written by: KILASA MTAMBALIKE, Dodoma

Credit to: Daily News
 
This happens only in Tanzania😕. Itabidi warudishe hicho cha juu ya 50,000/ kwa miaka yote ambayo wakuwaover-paid.
 
This is too obviously, waziri hana lolote jipya IPTL imelalamikiwa sana na yote haya anayosema sasa yalishajadiliwa na hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa. Bongo waziri naye analalamika sasa sijui nani achukue hatua.

Nilitaka kuona waziri anakuja na nini kifanyike katika kuhakikisha watanzania wanapata nafuu kutokana na mikataba mibovu na ya kifisadi lakini Ngeleja anaona leo kwamba kuna overcharge lakini hasemi nini serikali inafanya kufuta mikataba mibovu. Tumechoka kusikia michakato kwa muda mrefu, sasa ni high time kuona hatua zinachukuliwa.

Wabunge wasipitishe bajeti yake mpaka aseme serikali inachukua hatua gani kurudisha hizo fedha. Unyonge huu wa serikali unatoka wapi, Rais analalamika, Waziri Mkuu analalamika, Mawaziri wanalalamika, Wabunge na wananchi pia. Kuna haja gani kuwa na viongozi wanao lipwa vizuri, ulinzi na misafara lakini maamuzi yao ya kawaida!

Ngeleja na wenzake wanatakiwa kutembelea mikono, kutembelea miguu kila mtu anatembelea hakuna cha ajabu. Tumechoka taarifa za kawaida sana
 
Ngeleja: IPTL wanatuibia

na Tamali Vullu, Dodoma
Tanzania Daima


SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limegundua kuwa limekuwa likidhulumiwa kwa kulipa gharama zaidi za umeme (capacity charge) kwa IPTL.

Hayo yalibainishwa bungeni jana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alipokuwa akisoma hotuba ya makadirio ya matumizi ya wizara hiyo.

Alisema kutokana na uchunguzi uliofanywa na TANESCO, imegendulika kuwa equity halisi iliyotumika ilikuwa ni sh 50,000.

“Kwa maana hiyo, malipo ambayo TANESCO imekuwa ikiilipa IPTL kama Capacity Charge ni zaidi ya kiasi kilichostahili. Huu ndio msingi wa mgororo wa sasa ambao serikali/TANESCO na ITPL wanaendelea kuujadili,” alisema Ngeleja akithibitisha kauli ambayo imepata kugusiwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni.

Alisema maamuzi yaliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (International Centre for Investment Disputes) mwaka 2001 wakati wa usuluhishi wa shauri lililowasilishwa na TANESCO na IPTL, iliamriwa kuwa Capacity Charge itakokotolewa kwa kutumia mtaji wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31. Kiwango cha mtaji kilichotumika kilikuwa dola milioni 86.54.

Aidha, alisema gharama za uzalishaji za TANESCO zimepanda kutoka sh 96 kwa mwaka 2005 hadi sh 120/- mwaka huu kutokana na kupanda kwa bei ya chuma na shaba kwenye soko la dunia.

Alisema gharama ya ujenzi wa njia ya Kv 33 zimepanda kutoka sh milioni 18 kwa kilomita moja mwaka 2006 hadi sh milioni 35 kufikia Januari mwaka huu.

Waziri Ngeleja alisema bei za nguzo zimepanda kutoka sh 96,000 mwaka 2005 hadi sh 153,017 mwaka jana kwa nguzo ya futi 10.

Alisema kutokana na hali hiyo, TANESCO imelazimika kununua nguzo kutoka nje ikiwemo Afrika Kusini kutokana na bei kuwa nafuu zaidi.

Kuhusu kuimarisha uzalishaji umeme, alisema mradi wa umeme wa MW 200 kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwira utaendelea kutekelezwa, na kwamba yatafanyika maandalizi ya ujenzi wa umeme ya msongo wa Kv 220 kutoka Kiwira hadi Uyole, Mbeya itakayounganishwa kwenye gridi ya taifa.

Alisema mtambo wa Ubungo wa Mw 100 utakaokamilishwa na TANESCO, unategemea kuanza kuzalisha umeme mwanzoni mwa Agosti mwaka huu.

Waziri Ngeleja alisema mkataba wa Alstom Power Rentals uliokwisha muda wake Machi mwaka huu, haukuhusishwa na mkataba wa Aggreko muda wake utaisha Novemba mwaka huu.

Akizungumzia uboreshwaji wa sera na sheria ya madini, alisema serikali imepokea na kuchambua mapendelezo ya kamati ya rais kuhusu usimamizi wa sekta ya madini.

“Serikali imepokea na kuchanganua mapendekezo ya kamati, hiyo na inaandaa mpango mkakati wa kurekebisha sera ya madini na sheria nyingine zinazohusu sekta ya madini, ili kuyatekeleza mapendekezo hayo,” alisema.

Alisema wizara inatarajia ifikapo Aprili mwaka 2009, sera ya madini ya mwaka 1997 na sheria ya madini ya mwaka 1998 ziwe zimerekebishwa.

Kuhusu kuimarisha uwezo wa serikali kusimamia sekta ya madini, alisema wizara inatarajia kupanua idara ya madini na kuendelea kuajiri wataalamu zaidi wa kusimamia sekta hiyo.

Alisema Ofisi ya Ofisa Madini Mkazi, Kigoma, ilifunguliwa Septemba mwaka jana, ikiwa na lengo la kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za madini na kuboresha utoaji wa huduma.

Katika kuendeleza wachimbaji wadogo, alisema serikali ilitenga maeneo katika sehemu mbalimbali za nchi ambayo yanajumuisha Kilindi mkoani Tanga, Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro ambako ilitenga hekta 269,842.

Aidha, alisema Maganzo, Kishapu na Ibadakuli mkoani Shinyanga ilitengwa hekta 14,870 na Marerani mkoani Manyanya 10,490.

Kwa upande mwingine, alisema serikali imepata dola milioni 206.5 kutoka Millenium Challenge Corporation (MCC) ya Marekani kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme.

Alisema dola milioni 89.7 ilitumika kwa ajili ya kuimairisha mifumo ya usafirishaji na usambazaji umeme katika mikoa ya Tanga, Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya na Mwanza.

Alisema dola milioni 53.7 zilitumika kujenga kituo cha kuzalisha umeme kwenye Mto Malagarasi cha MW 8 kwa ajili ya Kigoma, Uvinza na Kasulu na pia kujenga sub marine cable kutoka Unguja kwa gharama ya dola milioni 63.1.

Waiziri Ngeleja alisema wataalamu kwa ajili ya kusimamia mradi wanatarajiwa kuanza kazi katikati ya mwezi huu.

Pia Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) limetoa dola milioni 10 kwa ajili ya kuendeleza mradi kwa kuboresha miundombinu ya usambazaji umeme katika maeneo ya Masaki, Mikocheni na Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Kutokana na hayo, wizara hiyo inaomba kuidhinishiwa bajeti ya sh 362,922,265,600 kwa ajii ya matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka 2008/2009.

Wakati huohuo, Bunge, jana lilikabidhiwa ripoti ya Kamati ya Rais ya kupitia sheria na mikataba ya madini iliyoongozwa na Jaji Mark Bomani.

Ripoti hiyo ilikabidhiwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kwa Spika Samuel Sitta.

Baada ya kukabidhiwa kwa ripoti hiyo Spika Sitta alisoma majina ya wajumbe wote wa kamati hiyo.

wenyekiti wa kamati hiyo ni Jaji Mark Bomani. Wajumbe walikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (CHADEMA), Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe (Kyela), Mwenyekiti wa United Democratic Party (UDP), John Cheyo na mwanasiasa mkongwe, Iddi Simba.

Wengine ni Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishna wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Wajumbe wawili waliotangazwa katika kamati hiyo, ni Peter Machunde ambaye ni mfanyabiashara na David Tarimo, kutoka Kampuni ya ukaguzi wa hesabu ya Pricewaterhouse Coopers.

Hata hivyo Zitto ambaye ni miongoni mwa wajumbe hao hakuwamo bungeni jana na taarifa zilizothibitishwa zinaeleza kwamba yuko Dar es Salaam kwa ugonjwa.

Hadidu za rejea za kamati hiyo zinaonyesha kuwa, imepitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zinazohusu migodi mikubwa na kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta hiyo.

Aidha, kamati imepitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa unaofanywa na serikali, imechambua na kuainisha haki na wajibu wa mwekezaji na serikali.
 
Serikali yakiri kutapeliwa na IPTL

2
008-07-09
Na Jackson Kalindimya, Dodoma


Serikali imebaini kwamba imekuwa ikitapeliwa kwa kuilipa zaidi kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kinyume na makubaliano.

Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja, alisema hayo jana Bungeni wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya wizara yake.

Waziri Ngeleja alisema kuwa kufuatia uchunguzi uliofanywa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO), imegundulika kuwa malipo ambayo imekuwa ikiilipa IPTL kaa gharama za uzalishaji ni zaidi ya kiasi kilichostahili.

``TANESCO imegundua kuwa equity halisi iliyotumika ilikuwa Sh. 50,000. Kwa maana hiyo, malipo ambayo TANESCO imekuwa ikiilipa IPTL kama capacity charge ni zaidi ya kiasi kilishostahili. Huu ndio msingi wa mgogoro a sasa ambao Serkali/TANESCO na IPTL wanaendelea kujadili,`` alisema.

Alisema uhusiano kati ya TANESCO na IPTL umekuwa wa mashaka kufuatia kutokubaliana na kiwango cha gharama za uzalishaji kinachotozwa.

Waziri alisema maamuzi yaliyotolewa na Kituo cha International Center for Investment Disputes mwaka 2001 wakati wa usuluhishi wa shauri lililowasilishwa na TANESCO dhidi ya IPTL iliamuliwa kuwa gharama za uzalishaji itakokotolewa kwa kutumia mtaji wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31.

Kiwango kilichotumika kilikuwa Dola za Marekani milioni 86.54.

Kuhusu Kamati ya Kuishauri Seriali kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, alisema kuwa tayari imemaliza kazi na kuwasilisha taarifa yake kwa Rais Kikwete mwezi Mei mwaka huu.

``Serikali imepokea na kuchambua mapendekezo ya Kamati hiyo na inaandaa mpango mkakati wa kurekebisha Sera ya Madini, Sheria ya Madini na Sheria nyingine zinazohusu sekta ya madini ili kuyatekeleza mapendekezo hayo.

Matarajio ya wizara ni kuwa ifikapo mwezi Aprili, 2009, Sera ya Madini ya mwaka 1997 na Sheria ya Madini ya mwa 1998 vitakuwa vimerekebishwa,`` alisema.

Waziri Ngeleja alisema kuwa Wizara itakamilisha mchakato wa kuanzisha hifadhi ya mafuta, ambapo EWURA itawasilisha mapendekezo ya kuhusu uagizaji wa mafuta pamoja kwa lengo la la kuanza kutekeleza utaratibu huo mwaka 2008/9.

Kwa upande wa mauzo ya madini nchi za nje, alisema kuwa yameongezeka na kufikia Dola za Kimarekani milioni 886.5 mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2006 dola za Marekeni milioni 836.8

Waziri Ngeleja aliliomba Bunge kuidhinisha mapendekezo ya bajeti ya Sh. 362,922,265,600 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na taasisi zake kwa mwaka 2008/9

SOURCE: Nipashe
 
Hayo mashairi hatuna haja nayo tunataka sheria ichukue mkondo kwani matapeli wanajulikana ,sasa hizi tararira ni za nini ? Wakamateni walio watapeli na muwapandishe kizimbani ,wananchi tutafurahi sana sana na kuipongeza Serikali yetu lakini ikiwa kila siku mnakuja na vipande vya mashairi na ngonjera mkiongeza na mikakati ,kwa kweli mtakuwa hamueleweki.

Halafu wacheni kupindisha mada na kuita sasa eti ndio mgogoro wa Tanesco na Iptl unaojadiliwa ,hayo sio tunayotaka kuyasikia ,kinachohitajika ni nani na nani walitiliana saini mikataba hiyo ,hao ndio wa kuwaumbua na kuwaanika kwani ndio chanzo cha mikataba mibovu inayoitumbukiza Nchi katika matatizo na matope.

Yaani mnataka tuyashitaki makampuni badala ya watu wenye akili ambazo walipaswa kuzitumia na badala yake walitumia kutafuta mlo kwa kuzika feza ya Taifa ,mbona bado mheshimiwa hujatuelewa.

Wandugu wafuatiliaji wa Kunguni hawa ni lazima muwe macho sana kwani hotuba za aina hii ni moja ya mikakati ya kupindisha ukweli kama mnavyowasikia CCM wakinadi kuwa CCM sio Chama cha Mafisadi mafisadi bali ni mambo ya baadhi ya watu binafsi wakati watu hao wamo ndani ya CCM na hatujasikia kuchukuliwa sheria yeyote ndio kwanza wanatafuta makanisa na misikiti kwenda kuhubiri maudhi. Na ndio mlingano wa hotuba za aina hii za kuwabadilisha watuhumiwa na makampuni yaani hata kosa likipatikana itaamriwa Kampuni ilipe au ifilisiwe hakuna tofaouti na wale waliojiuzulu.

Maana wamejiuzulu na wanaendelea kupeta mitaaani ,na hawana wasi wasi kabisaa ,na ndio hivyo hivyo hotuba hii inakotupeleka , wataifilisi na kuchukua vitu na mali za ofisini yakiwemo magari na mambo mengine wakati walioidhinisha na kupokea mrungura wametulia pembeni wakicheka kwa kuwa sasa watakuwa kwa uwazi zaidi kwani jalada limeshafungwa ,au vipi ?

Angalia huu usemi :-

...Huu ndio msingi wa mgogoro wa sasa ambao Serkali/TANESCO na IPTL wanaendelea kujadili....!

Mzigo mzima wa hotuba ni ujumbe huo hapo juu ambao umewabeba kunguni wote.
 
Wapo ila .......... Dr Slaha hakufanya home work yake vizuri.

Upinzani style: KUKURUPUKA

I like this!!
Who commissioned Dr Slaa to do this piece of work mpaka umhukumu hakufanya home work yake?
What if we propose you to do the naming and shaming for a change?
Part of your TOR should read:
IN THE COURSE OF YOUR WORK MAKE SURE NO STONE IS LEFT UNTURNED.KUKURUKAKARA WILL NOT BE TOLERATED.Should this be proved...you will be put on the firing line.
HAHAHAHHHHHAAHHH...It should be quite an easy task for you i hope.
 


Wote mnaoona hivyo kuhusu kuvunja mkataba mnaweza kuwa sahihi..tatizo ni kuwa wanaopaswa ku set the ball rolling are heavily entangled kwenye hiyo mikataba.Wakifanya lolote... will be tantamount to committing suicide!
Kazi ni kubwa....
 

Dear madam, Do I need to respond to this?
 
Hivi kila mtu aliweza kuisoma hii post ya sam? Ukiweza Print it, read it at home or while alone, feel it... Come back for a discussion!

 
IPTL yaifilisi TANESCO

na Tamali Vullu, Dodoma
Tanzania Daima~Sauti ya watu


SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) imeilipa Kampuni ya Umeme ya IPTL fedha za ziada zaidi ya sh bilioni 150 kama gharama za kuzalisha umeme.
Hayo yalibainishwa juzi jioni na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alipokuwa akifafanua kuhusu mgogoro uliopo kati ya shirika hilo na kampuni ya IPTL.

Alisema baada ya serikali kushinda kesi nchini Marekani dhidi ya kampuni hiyo, serikali ilishauriwa kwenda kwenye baraza la usuluhishi ili kumaliza mgogoro huo.
“Ndani ya mwezi huu, tutakutana kujadili suala hilo na ikishindikana tutakwenda kwenye baraza la usuluhishi....tukishinda wataturudishia gharama zetu zote,” alisema Ngeleja.

Hata hivyo, Ngeleja alisema kwa sasa si rahisi kwa serikali kuvunja mkataba wake na kampuni hiyo hadi suala hilo litakapomalizika.

Akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti yake, Ngeleja alisema TANESCO imegundua kuwa imekuwa ikidhulumiwa na kampuni hiyo kwa kuilipa gharama zaidi za umeme. Alisema uchunguzi uliofanywa na TANESCO umegundua kuwa ‘equity’ halisi iliyotumika ni sh 50,000.

Alisema maamuzi yaliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (International Centre for Investment Disputes) mwaka 2001, wakati wa usuluhishi wa shauri lililowasilishwa na TANESCO na IPTL, iliamriwa kuwa ‘capacity charge’ itatolewa kwa kutumia mtaji wa asilimia 30 na faida ya asilimia 22.31. Kiwango cha mtaji kilichotumika kilikuwa dola milioni 86.54.

Akizungumzia kupanda kwa gharama za umeme, Ngeleja alisema imepanga kulifanyia kazi kutokana na malalamiko kutoka kwa wananchi.

Alisema wamekubaliana na Ewura kujadili suala hilo na kuangalia kama kuna uwezekano wa kupunguza gharama hizo.

Waziri wa Nishati na Madini alisema katika mkutano huu wa Bunge unaoendelea, wizara itatolea kauli suala la mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira, ambao umekuwa ukijadiliwa na wabunge wengi, wakipinga uwekezaji wake.

Mgodi huo unaodaiwa kumilikiwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Danel Yona.
 
Serikali yetu imekuwa ya wapuuzi. Sidhani kama inashindikana kupata sababu zozote za kuwashitaki IPTL ili mkataba wao uweze kufa

Kama TZ wakiamua kufuatilia mambo ya IPTL ki-usalama wa taifa, wanaweza wakapata visababu vya kuwaandama hawa jamaa mpaka wakauzira mradi wao.

Wanaweza wakaanza na yule bwana wa Bukoba aliyenunua degree pale UDSM, and then wakaendelea na hao partners wake na hatimaye kampuni yenyewe kama wafanyavyo US.

Wao FBI au hata polisi wa kawaida, ukiwashinda upande mmoja watakuvizia mpaka wakunase hata na kosa la kumchungulia mtu na kukupa max. Angalia kesi ya OJ ndio utajua.

TZ kama tulishindwa kwenye abitration, basi tuwanase hawa jamaa humo humo nchini maana ufisadi waliotufanyia ni wa wazi wazi. Wametumia sheria kutukandamiza na sisi tuitumie hiyo hiyo kuwamaliza ili mwingine asije akajaribu kufanya hivyo hata kama loopholes zikiwepo.
 
HIGH-LEVEL CORRUPTION: Report reveals how TANESCO was coerced to sign IPTL deal

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A PREVIOUSLY unreleased report has revealed how high-ranking government officials had exerted extraordinary pressure on the state-run Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO) to sign a dubious 20-year contract with the Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

The report by a Washington DC-based investigative consulting firm, Decision Strategies Fairfax International (DSFX), which was commissioned by the government contains statements from senior TANESCO officials describing how the 1994 IPTL was illegally pushed through by politicians, much like the 2006 Richmond energy scandal.

The report quotes TANESCO’s former Managing Director, Baruany Luhanga, describing in considerable detail how the power utility ’’was forced by senior government officials to conduct negotiations with IPTL.’’

Luhanga outlined a ’’top-down, highly-pressured’’ atmosphere where TANESCO ’’was shut out of the IPTL approval process’’ because senior government officials in the then Ministry of Water, Energy and Minerals and elsewhere were pushing the process.

He told investigators from the US firm how TANESCO was remarkably ’’never shown’’ a copy of the 1994 Memorandum of Understanding (MoU) between Mechmar Corporation of Malaysia and the energy ministry until after the MoU was signed.

’’Luhanga noted that it was ’incredible’ that TANESCO was ’’cut out of’ the MoU drafting process, as the MoU provided ’a fast track’ resolution to an existing power shortage by the utilization of an independent power producer, a concept foreign to Tanzania,’’ says part of the January 1999 report, which has never been made public by the government.

According to Luhanga, such a huge $163.5m (approx. 190bn/-) project for the generation of 100MW of power necessarily required lengthy analysis and oversight by TANESCO -- none of which occurred in the IPTL negotiations.

Luhanga told investigators how IPTL used the ’fast track’ provision incorporated in the MoU ’’like a hammer’’ to demand that TANESCO ’’move things along quickly.’’

’’In fact, Mr Luhanga noted that when we (TANESCO) did disagree with IPTL, then we got pressure from high-level officials to work things out IPTL’s way,’’ says the report.

The ex-TANESCO chief also told investigators that the IPTL director, James Rugemalira, enjoyed ’high access’ with senior government officials. ’’He (Rugemalira) can see anybody that matters,’’ he said.

’’Rugemalira is particularly close to (then) Finance Minister Daniel Yona and provided specifics underpinning his belief that minister Yona always does Rugemalira’s bidding,’’ the report quotes Luhanga as saying.

Luhanga maintained that he believed corruption was central to the facilitation of IPTL’s interests in the project.

Esther Masunzu, TANESCO’s former manager for special duties, who previously served as assistant commissioner of energy within the electricity section, also told investigators that IPTL ’’took advantage of their high government contacts to get things handled their way.’’

Masunzu, who chaired the IPTL negotiations, explained how she was reprimanded by senior officials in the energy ministry for ’’moving too slowly.’’

She said apart from being criticized by senior government officials for not speeding up the IPTL deal, Rugemalira would also burst into her office to complain that negotiations ’’were moving too slowly.’’

A former TANESCO company secretary, Mrs Subira Wandiba, also told investigators that there was ’’too much pressure from the government to approve it (IPTL deal).’’

As the legal adviser to TANESCO’s Board of Directors, Wandiba concluded that because of the high-level government pressure in favour of the IPTL project, ’’too many legitimate issues raised by TANESCO regarding IPTL’s proposal are left unanswered and unclear to this day.”

’’TANESCO should have had more time to analyze IPTL ... There was no need to put this on a fast track,’’ she added.

TANESCO’s then director of corporate planning and research, K.R. Abdallah, told investigators that he believed the tariff demanded by IPTL to be ’very excessive’ and expressed his strong views on the matter to other senior officials of the public utility.

He criticized the ’lack of competitive bidding’ where IPTL became the ’sole’ government-sanctioned solution to the energy crisis emergency.

Abdallah noted that the country would have been better served by other options apart from the overly expensive IPTL project.

Likewise, TANESCO’s then chief statistician, Felician Mayila, also asserted that ’’people outside of TANESCO at the Cabinet level were pushing the IPTL project.’’

He noted that the power company’s planning directorate was never consulted in the IPTL negotiations and only saw the controversial power purchase agreement lasting until 2014 after it had already been signed.

’’If we had been given a fair chance to analyze IPTL, then it would never have been negotiated out of contract because of their high cost,’’ he said.

Investigations by THISDAY have revealed that the ripple effects of the IPTL contract are still being felt today, more than a decade after the deal was signed.

The DSFX investigators carried out the assessment on the deal after being engaged by Acres International, a Toronto-based engineering consulting firm, which was commissioned by the ministry of energy and minerals to study the matter.

A team of US investigators had worked with the former Prevention of Corruption Bureau (currently known as the Prevention and Combating of Corruption Bureau) in their assessment of the IPTL contract, but remarkably no prosecutions have been made so far.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…