Elections 2010 Ufisadi wa kutisha ikulu - Kikwete atumia bilion 29 kukarabati ikulu

Watu wazima na akili zenu timamu munatumia muda wenu kusambaza uongo na majungu. Hebu tumieni muda wenu kutubia kwa Mungu kwa uzushi wenu.

Aliyelala USIMWAMSHE.. Ukimwamsha.........................
 
.

Kiasi cha fedha hicho sio cha kutisha kukarabati makazi namba moja ya Taifa (Ikulu), CAG alitakiwa kueleza aina ya matumizi ndio hoja hii ingeweza kujadiliwa kwa marefu na mapana, hivi ilivyo ni kama inaelea hewani. Tangu, awamu ya Rais Mwinyi na Rais Mkapa ni miaka kadhaa imepita sio rahisi kulinganisha na hasa tukichulia kwamba kwa sasa mfumuko wa bei (inflation rate) uko juu na hata nguvu ya dola dhidi ya shilingi ni tofauti hivyo gharama zitakuwa juu. Kwa mfano, kama tunakumbuka Nyumba aliyokuwa anaishi Mkapa iliungua hivyo ilihitaji ukarabati au ujenzi mpya, yote haya hatujui kama yamo katika gharama hizo za CAG au la.
 
NAOMBA FAHAMISHWA...KUNA BINTI/MAMA ANATOKEA KWENYE PICHA NYINGI NI NANI HUYU......WOZOZA POST NAMBA 13 PIA KAMUWEKA nataka jua ili niijuvye akili yangu
 

Naona unachanganya madawa, Mahakama ya kadhi inaingiaje kwenye mada hii????? madai ya Makahakama ya kadhi haikuanza wakati wa awamu ya nne, madai haya yalikuwepo enzi za Nyerere, Mwinyi na Mkapa. Kikwete ameyakuta anaendelea kuyafanyia kazi kuanzia pale walipoacha wenzake. Hakuna ambaye alikuwa anajua kwamba Rais wa awamu ya nne atakuwa mwislamu. Kugongana kwa mahakama ya kadhi na Rais mwislamu wa awamu ya nne isiwe kesi ya kuzua kwamba Kikwete ndiye aliyeleta madai hayo.
 
hahaaa hiyo niliyo bold ndo imenichekesha sana.....keli na umenena ukweli mtupu

Tuache ushabiki tujenge hoja zitakazowasaidia watoa maamuzi kufikia hitimisho litakalosaidia kuanzisha au kutoanzisha mahakama ya kadhi bila kuleta vita ya kidini.
 
 
And who is the contractor doing all those works????
 
Hizo BILIONI 29 ni pamoja na yale matumizi ya shughuli za kifamilia tulizokuwa tunazifanyia WAITI-HAUSI na kumbuka familia yote iko WAITI -HAUSI unategemea nn hapo mkuu :mad2::mad2: halafu bado watu watapanga foleni kuipigia kura CCM

Haya ni majungu na hayatatufikisha hitimisho sahihi ya mada yetu. Kama haijaelezwa fedha hiyo imetumikaje basi ni vigumu kujadili mada inayokosa viambatisho muhimu vinavyoweza kutusadia kujua kama matumizi hayo ni sahihi au la. kwa kuangalia tarakimu 29 bilioni tu hatutakuwa tofauti na wasemavyo, "bila utafiti hauna haki ya kuzungumza" kwa kuwa unaweza kuipotosha jamii.

Mathalan, chukulia kwamba wote hapa tuna nyumba, mwingine anaweza kuwa amejenga kwa sh. milioni 20, milioni 30, milioni 50, milioni 80 na kuendelea. Kupata ukweli ni kwa nini nyumba hizo zimejengwa kwa gharama tofauti lakini zote ni nyumba inahitaji maelezo ya ziada.
 

Umeanza ligi? how long are you staying?
 
Endelea kufumba macho ili usiuone ukweli!

Hatuwezi kuuona ukweli wakati mada imeletwa hapa kisiasa badala ya ki-Hasibu. Kwa Wahasibu au wakaguzi wa mahesabu huwezi kumkamata mtu mwizi bila vielelezo na ndio maana tunasema tarakimu pekee haitoshi kusema fedha iliyotumika ni nyingi au ndogo. Nani kasema wote hapa JF ni wanasiasa kila mtu na fani yake.
 
NAOMBA FAHAMISHWA...KUNA BINTI/MAMA ANATOKEA KWENYE PICHA NYINGI NI NANI HUYU......WOZOZA POST NAMBA 13 PIA KAMUWEKA nataka jua ili niijuvye akili yangu

wewe unataka wenzako wafungiwe sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…