CHAPALAKATA
Member
- Sep 9, 2024
- 78
- 120
Mwabukusi, Rais TLS, hali ya mahakama za mwanzo ni ya kusikitisha. Kuna wanasheria uchwara wengi. Rais Mwabukusi, sijui kama unajua hali hii hapa Ukonga? Katika mahakama za mwanzo, zipo ofisi za "wanasheria" wa ovyo ambao wanapokea kesi za watu na kuzipeleka mahakama za mwanzo na za juu. Wengine hawa ni watu wenye elimu ya darasa la saba. Mwanasheria anajiita advocate, akiwa na kiwango cha elimu ya std 7, na ana ofisi Ukonga. Hii haifai kabisa, wananchi wanapigwa sana. Wengi hawana uelewa wa kisheria, wanatafuta unafuu lakini wanakutana na mawakili feki.
Hili ni jambo la kusikitisha. Je, chama cha wanasheria hakina mfumo wa kuhakiki mawakili wa kweli? Najiuliza, nini maana ya chama hiki cha wanasheria? Hili si suala la kulaumu serikali pekee, bali chama hiki kinashindwa kutimiza wajibu wake. Naomba Mwabukusi aliangalie hili.
Ukifika karibu na FFU Ukonga, nje ya geti kuelekea Mombasa, barabara ya Moshi, kuna mwanasheria wa kiwango cha std 7 mwenye ofisi huko. Ameumiza watu wengi. Anachukua kesi za watu na kuwatoza pesa nyingi. Kuna mtu ambaye kesi yake imechukua miaka 6, baba wa familia ambaye sasa amefilisika. Alikuwa na gari, akaamua kuuza ili amlipe wakili huyu feki. Juzi, ameuzwa butcher zake mbili kwa sababu ya kumlipa huyu tapeli. Baba huyu alikuwa na watoto wanaosoma shule za sekondari binafsi, lakini wote wamesimamishwa kwa kukosa ada. Mwanasheria huyu, mwenye asili ya kabila la Mgogo, ameendelea kuwalamba pesa watu.
Pia, baba mmoja aliyekuwa na kesi ya nyumba zake kwa wakili huyu aliishia kuuza nyumba hizo. Mwaka mmoja sasa, baba huyo amefariki baada ya kudanganywa kwamba atashinda kesi hizo.
Hii ni habari ya kusikitisha sana. Mwanasheria huyu bado anapokea kesi na kuwalamba watu pesa zao. Jamani, nchi hii inakwenda wapi? Imagine, utapeli huu unafanyika mkabala na Jeshi la FFU Ukonga!
TLS, tafuteni huyu wakili feki. Mwiteni, muulizeni kama anavyo vyeti vya uwakili. Eneo hilo litawaonyesha mtu huyo. Wanasheria, okoweni watu hawa! Akipatikana, abanwe, aonyeshe vyeti vya uwakili wake. Mawakili feki kama hawa wafutwe. Wananchi wanateseka, wazee hawajui pa kwenda, na maisha yao yanakatishwa na mawakili feki. Je, wanatofauti gani na majambazi?