Ufisadi wa Nyumba za Serikali


Rufiji, let me school you, son.... I got the Litimus test..Campaign involves alot more than Friendship..JK & EL are friends on the virtue of Strategy for Power..They could of easily lots the 2005 election..Two camps Mitandao camps were in place in 1995...Nyerere distroyed Lowassa chance ndio akaunganisha mitandao with the assumption that once JKis done, he can emerged...sasa the guy thought kugombana na Subordinates ndio kuwa maarufu & he has always made decisions against JK will..

Friendship...he had to go...Yeye aliacha position ya PM for him & his boy Sam 6 to decide...Influence ya Rostam went for EL...sasa hapo ilikuwa ni kitu kimoja...1 year later, ilibidi achukue hatamu na thats when 10 Lowassa calls to JK , only 1 reply...Nilikuwa Dodoma ambavyo JK snub Lowassa akaenda chooni uwanja wa Ndege...and Yes, he betrayed Lowassa...but not the Tanzanian people...Wimbi la Ufisadi lina-gear kubwa because of his money..I know my facts B!!!
 

Mkuki kwa Nguruwe kweli kwa binadamu mchungu..wewe unasema Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni...Sasa unakacha debate for that??? haki yangu je? wewe you've suggested that I didnt have facts, unaniambia siko classy baada ya quote hiyo..anyway, stop being too emotional, sisi wote watu wazima.

Kwa manufaa ya wote..Uhusiano wa JK na Lowassa utakuwa mbaya sana..walimkatia matangazo TVT akijitetea..TZ kuna mawaziri wangapi ila coverage yake iko biased..Kama hujui JK ni Mkulima, sio wa mashamba madogo, mashamba makubwa lakini JK sio Fisadi..ukimuita JK fisadi humjui JK..Lowassa ni Real Estate Mogul, a Millionaire by far..uhusiano ulikuwa ni wa Maslahi..Sasa kila kitu kina wakati wake..Hit job ya Lowassa alipewa Sam 6 na Lowassa kaenda Dodoma hajui ripoti ya Richmonduli ina nini..haijawahi tokea...ila sasa hayupo, atatumia Media to create hii dispair inayoendelea..mimi nina uchungu sababu najua ukweli..thats it Rufiji..Tupunguze ushabiki lets remember kuna hela hata kwenye habari, watu wanacha kununua unga wanunue Mwanahalisi...lets be careful.
 

FMES,
Uongo gani uliosemwa ili tuombe msamaha? Mbona hueleweki?

Kwa hiyo unataka kusema Mnauye ndiye aliyesababisha nyumba zote za serikali zikauzwa? IFM na WB wameishia wapi kwenye utetezi wako?

Au una maana unawatetea hao waliouza mali zetu kwa vile kwa vile mmeoa kwa baadhi yao. Kwa nini nyumba zetu zisirudishwe halafu tukaichangia familia ya Mnauye peke yake, kama tulivyochanga kumuaga JKN, badala ya kuwapa mafisadi mali yetu tena bure bure??
 

Usitake kujua kila kitu, Mkuu. Kama hauna ushahidi kaa kimya kama tunavyofanya wengine.

Uamuzi wa kuuza nyumba haukupitishwa na Bunge. Uamuzi huu haukushinizwa na IMF wala World bank bali ulikuwa ni sehemu ya mradi wa kuboresha utendaji wa serikali kuu uliofadhiliwa na DFiD ( Hii haina maana kuwa serikali ya uingereza ilihusika katika maamuzi haya). Matokeo ya mradi huu ni uanzishaji wa Executive Agencies. Uamuzi ulitokana na sera ya kufanya idara za serikali ziweze kujiendesha bila kutegemea ruzuku serikalini. Maamuzi yalihusu nyumba zilizokuwa chini ya serikali kuu na idara zake. Nyumba za baadhi ya mashirika nazo ziliuzwa baada tu ya kurejeshwa serikali kuu.

Maghorofa yapi ya Tabata ya serikali kuu unayozungumzia?Ninavyojua mimi,maghorofa ya serikali kuu yako Ocean Road, Kinondoni na Masaki na chache katikati ya mji. I stand to be corrected lakini sijawahi kusikia kuwa watu wanaoishi katika maghorofa haya wameuziwa nyumba zao. Tatizo litakuwa katika umiliki wa hati ya uwanja. Kama unamjua mtu aliyeuziwa nyumba katika maghorofa ya serikali kuu tufahamishe. Vilevile sidhani kama nyumba zilizokuwa katikati ya mji ziliuzwa kwa wakaaji.

Kuna nyumba Oysterbay zimeuzwa chini ya milioni 50. Hii ilitokana na ukubwa wa nyumba, sehemu ilipokuwepo, hali yake n.k. Lengo lilikuwa ni kuweka bei ambayo mfanyakazi wa serikali angeweza kumudu na si vinginevyo. Hiyo ya mikopo kutoka benki siijui kwa hiyo siwezi kuzungumzia. Ndiyo maana waliouziwa hawakuruhusiwa kuziuza tena kwa muda fulani. Lakini tukumbuke kuwa huko Oysterbay na Masaki kuna baadhi ya mashirika nayo yalikuwa na nyumba zao ambazo waliziuza nje ya mradi huu. Hizo hazikubanwa na malengo ya mradi wa nyumba za serikali.

Sasa kama huo uamuzi ulikuwa sahihi au sio pamoja na taratibu zilizotumika ndiyo tujadili hapa. Hilo nawaachia wenzangu wenye kujua suala hili kwa undani zaidi.
 
Sijui ulijuaje kuwa hakuiba, lakini kama aliweza kununua nyumba ya O'bay/ Masaki, basi asingeshindwa kujenga nyumba kubwa zaidi Gongo la Mboto, Tabata nk.


Haya ni maneno maneno ya uongo, dhidi ya marehemu Mnauye, hakuwa na nyumba hata moja!
 
Uamuzi wa kuuza nyumba haukupitishwa na Bunge. Uamuzi huu haukushinizwa na IMF wala World bank bali ulikuwa ni sehemu ya mradi wa kuboresha utendaji wa serikali kuu uliofadhiliwa na DFiD

Mkuu wacha hizi, kwenye mkutano na wa-Tanzania kule hotelini Hermsley NY, akiwa anaaga Mkapa alisema kuwa uamuzi wa kuuza nyumba za serikali ulikuwa ni wake baada ya kushinikizwa na IMF na World Bank, ambapo pia alipata ushauri wa bunge, na akasema nasikia rais anayekuja ana mpango wa kuzirudisha, huku akimuangalia Muungwana, aliyekuwa kushoto kwake, akamalizia kuwa "... Namtakia Goodluck...", sasa mkuu hizi umezitoa wapi maana tunajua pia walishinikizwa na kuuza benki NBC?
 
Huenda ule ushahidi uliouliziwa na wajumbe kadhaa humu ndani kuhusu kuhusika kwa IMF na World Bank katika kushinikiza uuzwaji wa nyumba za serikali upo katika mojawapo ya hizo policy zao 157 na masharti 20 waliyotuwekea, kulingana na habari hii hapa:

The excessive number of policy prescriptions, or conditions, attached to the new loans and debt relief
amount to micromanagement of the GOT. Tanzania's Policy Matrix, 2000-2002," which was appended to
the Interim PRSP by the IMF and World Bank lists approximately 157 policies that the Government of
Tanzania will be pressured to implement during this time period. In addition, there are more than 20
policy conditions linked to debt relief, ten policy conditions linked to the World Bank's Country
Assistance Strategy (CAS), and additional conditions linked to IMF and World Bank-financed structural
adjustment loans.

The rest of the article can be found here:
http://www.tanzaniagateway.org/docs/SAP_alert_on_IMF_and_World_Bank_lending_to_Tanzania.pdf
 

Nimeishakuambia angalia unalozungumzia. Una base yote hii kutoka kwa hotuba ya Mkapa wakati akiwaaga? Bila shaka nae uko karibu nae. Wanasiasa wanatumia IMF na World Bank kama bogey figures pale wanapobanwa.

Kushauriwa na bunge imekuwa lini sawa na kupitishwa na bunge?

Nimekuuliza kuhusu hayo maghorofa ya Tabata, bei ya nyumba Obei umeshindwa kujibu. Kama haujui, nyamaza tuu, There is no shame in it.
 

Sioni mahali panaposema hawa jamaa waliishinikiza serikali kuuza nyumba zao. Ukishauriwa kupunguza matumizi ni uamuzi wako utafanya hivyo vipi, kuacha kula nyama, kuuza gari, kuhama kwenye nyumba unayoishi n.k. Hawa walitoa ushauri, technicalities za namna gani tunaweza kutimiza haya malengo zilifanywa na sisi.

Angalieni hii link itaweza kutoa ufafanuzi wa ninachozungumzia.
http://unpan1.un.org/intradoc/groups/public/documents/CAFRAD/UNPAN010583.pdf

Mradi ulikuwa na lengo la kuboresha utendaji na delivery of services wa serikali kuu. Nyumba zilikuwa ni sehemu ya services ambazo serikali kuu ilikuwa ikitoa kwa wafanyakazi wake. Chini ya mradi huu ndipo hii huduma ilipoangaliwa na maamuzi kufanyika. Hakuna mkono wa World Bank wala IMF much as we might have wished otherwise.
 
Waugwana tuangalie swala zima katika muono wa kisomi na sio wa kishabiki maandazi.

Wale wote mnasema kuuzwa kwa nyumba hizi ni sawa kutokana na operaring cost yake ni kubwa, naomba tutofautiane kwa hilo. Swala sio maintanance cost, swala ni mfumo tegemezi na ufujaji uliojengeka tangu Azimio la Arusha mpaka mfumo mzima wa soko huria ndani ya serikali. Kama tunasema serikali ime adopt mfumo wa soko huria, basi ni imani yetu mfumo umeadoptiwa kwa sheria na kanuni za mfumo.

Imagine safari tuliyonayo kuelekea kuwa nchi imara, jee itafikia muda mawaziri wanatakuwa wanatokea mbagala au kawe kwenda kazini? Jee wakuu wa polisi nao watakuwa wanatokea Kijichi kwenda central? Jee hatuoni kwamba in the long run sisi tulioshabikia nyumba ziuzwe ndio tutakuwa malooser? Kwa nini tumekuwa wakatili kiasi cha kuwaza Leo tuu, badala ya kuangalia vizazi vijavyo. Au Tanzania imekuwa kiwanda ambacho kiko kwenye maturity level, the best way is to sell all of its asset, so we can secure savage for tax purposes?

Na kama kweli Mh. Mkapa na washabiki wake waliona kuna umuhimu wa kuuza zile nyumba kutokana na cost, jee kwa nini nyumba hazikufuata sheria ya uzaji wa mali ya serikali. Au ndio mwenye kisu kikali hula nyama?

Tuacheni ushabiki usio na kichwa wala miguu, tusishadadie habari sababu uncle au shangazi yako ni mmoja wa wale walijiuzia nyumba ya serikali kwa bei nafuu. Tuangalie madhara yake in a long run, Jee hakuna siku kiongozi mwehu ataingia madarakani na kunationalize hizo nyumba zote? Na kama ikitokea jee mwisho wake utakuwa nini?

Hili swala linaweza kuwa domino effect, likatuchafulia hali ya uhuru na amani nchini kwetu.
 

Haya na tuongee kisomi ingawa mimi huko simo. Mkuu naona unaishi Marekani. Je huko serikali inatoa huduma hii kwa wafanyakazi wake wote? Condoleeza anakaa katika nyumba ya serikali? Au uingereza? Brown kabla hajaukwaa uPM alikuwa anaishi katika nyumba ya serikali? Au Afrika kusini? Au nchi yeyote iliyoendelea? Wafanyakazi wa serkali wanapewa nyumba za kuishi bure na serikali kuu?

Suala la kutoa huduma hii halikuwa sustainable kwa jinsi lilivyokuwa likifanyika. In the long run huduma hii inatakiwa itolewe na soko la nyumba. Mfanyakazi alipwe vizuri na sokoni pawe na nyumba za kutosha zinazokidhi mahitaji yake kwa bei atakayomudu. Kwa sasa hivi hapa kwetu hilo soko halipo. Mahitaji yamezidi mno production kiasi cha kuwafanya wenye nyumba hizo kutoza pango wanavyotaka.

Serikali kwa muda mrefu ilikuwa haitoi fungu kwa ajili ya kuzikarabati wakati pango lilikuwa pegged kwenye mshahara wa mkazi. Mshahara wa wengi waliokuwa kwenye nyumba hizo ulikuwa kati ya 100,000 na 200,000. Hawa walikuwa wanalipa asilimia 10 ya mshahara kama pango hivyo kufanya pango kwa mwezi kuwa sh 10,000 hadi 20000. Hii pango ilikuwa haitoshi hata kunua kitasa na ilikuwa chini ya pango la chumba Mwananyamala chenye umeme! Serikali kwa hiyo ilitakiwa aidha iamue kusubsidise huduma kwenye nyumba hizi ( kitu ambacho katika soko hilo la huria halikubaliwi), kuongeza mshahara wafanyakazi wake wanaoishi katika nyumba hizo ili pango liwe linaloendana na mahitaji halisi ya uendeshaji, kupangisha nyumba hizo kwa wakaaji wake kwa market rates, kuziuza n.k. Uamuzi uliochukuliwa ni huo wa kuziuza. Taratibu za uuzaji wa mali ya serikali unasema mali hiyo itauzwa kwa mnada. Hivi hizo nnyumba zingeuzwa kwa mnada wamatengo wangapi wangeona ndani? Tukumbuke hatuzungumzii za Masaki tu bali hata zile za Chang'ombe! Matokeo yangekuwa kuwa nyumba hizi zimenunuliwa na wafanyabiashara na tukiwa zaidi, wafanyabiashara ambao wengi wao wangekuwa ni wahindi, waarabu au makaburu tungesema nini?

Huyo atakayeamua ku'nationalize' hizi nyumba tena itakuwa uamuzi wake na bila shaka atafanya hivyo baada ya kujiridhisha kuwa ni uamuzi utakaoangalia maslahi ya taifa letu. tulitaifisha nyumba kibao, tukaanzisha Msajili wa Nyumba, zikatushinda kuzihudumia hadi hapa tulipo ambapo tunazirudisha tena katika soko huria.

Kama ulivyosema Mkuu. tuliangalie hili suala kisomi na tuache ushabiki usio na kichwa wala miguu!
 
Na kwa wale wanaoona mkono wa IMF na World Bank kila mahali hata pale tunapoteleza wenyewe, hii hapa ni sehemu ya hiyo link niliyoiweka hapo juu:

 
 
 
For the sake of argument let's say it was prudent and progressive for the government to shed the houses.

But why not put them on the open market? Or sell them at market price?

The fact that the houses were not on the open market, and not sold at market price is what raises the notion that there were some improprieties.
 

I think the fear that had they been put on the open market only a small section of the population would have afforded them. This would have further aggravated the socio-economic divide existant in our society. Can you imagine the outcry that would have been raised had those houses been sold to those of our community of a paler complexion? The Mtikilas amongst us would have had a field day!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…