Ufisadi wa Nyumba za Serikali


Si wewe uliyenifanya niamue hivi. I have just been spending too much time in here. I need a break. I average over 6 posts a day which borders on insanity. Hakuna mwenye mawazo finyu humu ndani. Nitaendelea kusoma mpaka hapo nitakapojihakikishia mwenyewe kuwa ninaweza ku-moderate hii addiction. Kwa sasa hivi nimeamua kwenda cold turkey. Si unaona nimekujibu ingawa nilishaaga! Woe be me!!!
 

Kampuni inaundwa kusimamia utunzaji wa nyumba za serikali badala ya serikali kufanya hiyo kazi. Swali ni kuwa Kama mishahara haiwezi ongezwa kufikia hali ya soko kwa nini basi nyumba ziliuzwa?
 
Kubwajinga ,

Ukiangalia hili zoezi la kuuza nyumba kwa undani unaweza kulia ! Ni tamaa tuu za viongozi wetu kuona muda wa kustaafu umekaribia ndio uliopelekea kufanikisha hilo zoezi , ila kinachoniuma mimi ni kwa nini wananchi huko nyumbani wanaendelea kuwachagua ?

Tuna nafasi kubwa sana ya kuonyesha kuchukizwa kwetu na vitendo vyao kwa kuwanyima kura zetu ...
 
kikwete akisema aliuziwa nyumba wa kulazimishw anatudanganya....aliekewa mtutu wa bunduki?

hata kama kulikuwa na umuhimu wa kuuza nyumba za serikali, basi haikuwa zote. nyumba za mawaziri na makatibu wakuu zilikuwa katika hali nzuri tu. na isitoshe, wameuziwa katika bei isiyostahili kabisa
kuna watu waliuziwa nyumba oysterbay, ndani ya hicho kiwanja wameweza kujenga nyumba nyengine moja.
means wameuziwa viwanja viwili na jengo moja kwa bei ya kiwanja pekee. its such a shame
 

Ukisoma maandiko yangu utafahamu ya kwamba nilishasema ya kwamba, Dar es Salaam city planning haiwezi kusastain viongozi kutoka Mbagala na kuja kazini posta. US kwa bahati wana city planning and that help them a lot. Kiongozi anaweza kuja capital hill wakati anatokea Delaware, sio Dar es salaam.

Mkuu kama uoga ulikuwa ni wafanya biashara wenye cash supply kubwa wangeshinda bid, then serikali ilifanya analyisis gani kuona inapata maximu return kwenye ardhi inayo appriciate more than 15% annual? Na kama swala ni soko huria basi maana yake tunaangalia worth ya eneo, kisha tunaangalia how appriciate the area is, kisha tuna set price.Jee serikali ya Ben ilichukua mesure zote hizo?

Sasa ninaposikia ya kwamba nyumba imeuzwa kwa million 40 ndani ya masaki nakuwa devastated. Watu hao walionunua kwa 40 Million kisha wanawakodisha wafanya biashara wakubwa ambao wanajenga high rising condominium. Sasa who is a looser?

Kuangalia manufaa ya taifa means, wananchi wanabenefit at the same time serikali ina benefit. Sasa kama few people ndio waliokuwa serikali, then wakaset price, then wakanunua hizo nyumba. Swala linakuja where is check and balance? Kumbuka a lot of money ilitumika kufanya maintanance hizi nyumba wakati wa mzee Mwinyi, sasa uone kwamba kuziuza kwa bei ya chini ni kuwaibia tax payer?

I think the whole business ilikuwa full of corruption, the only way ni kuzirudisha then tuangalie utaratibu ambao wananchi wanatafaidika na serikali itafaidika. Na sio wakuu wa majeshi na mawaziri wachache kufaidika na serikali kuloose million of shilling.
 

City planning has nothing to do with it. Kwani hao wanaoishi sasa huko Kimbiji wanawahi vipi kazini? Najua watu wanatoka kibaha na ni wa kwanza kuingia kazini. Na nina wajua wanaoishi katikati ya mji na kila siku wanachelewa. Namna mtumishi anavyofika kazi haingii katika equation. Kama pangekuwa na supply ya kutosha ya nyumba, hawa viongozi wangeamua kukaa kokote wanakotaka na kazini kuwahi. Kinachogomba ni upungufu wa nyumba ambazo zinazoonekana ni za status zao kwa bei ilinayoendana na uwezo wa serikali. Hili lilikuwa ni kasoro na ndio maana mara baada ya zoezi kufanyika wakajenga nyingine. Proper planning ingewafanya waepuke makosa kama haya.


Mimi nilispeculate. sasa hiyo analysis ingesaidia nini wakati hatuna formal soko la nyumba au viwanja? Kumbuka kuwa kwa muda mrefu ilikuwa marufuku kuuza kiwanja. Hii ilichangia kwa kiasi kikubwa true value ya viwanja. Trust me, kinachogombaniwa huko Obei na kwingineko kama huko ni viwanja sio nyumba. Hiyo kitu nyingine unayozungumzia ni valuation na ilifanyika. Kwa umakini gani, that is open to debate.

Una maana gani na "how appreciate the area is" ? Kila mtu anajua kuwa bei ya nyumba nyingi katika prime area ilikuwa chini sana. Kuna watu wengine katika maeneo mengine katika miji nyingine walilalamika kuwa bei waliyouziwa ilikuwa juu mno. Hili ni tatizo.


Sasa ninaposikia ya kwamba nyumba imeuzwa kwa million 40 ndani ya masaki nakuwa devastated. Watu hao walionunua kwa 40 Million kisha wanawakodisha wafanya biashara wakubwa ambao wanajenga high rising condominium. Sasa who is a looser?

Si nyumba zote zilizokuwa Obei ni za serikali kuu. Nyingi ambazo zinejengwa hizo condominiums ziliuzwa na mashirika kama NDC. Katika mkataba wa kuuziwa nyumba ya serikal palikuwa na kipengele kinachomkataza mtumishi kuuza tena nyumba ndani ya muda fulani. Maendelezo yote ya kwenye kiwanja yalihitaji kibali cha serikali. Kwamba hii imekuwa abused? Inawezekana kabisa.

Naona Mkuu haujatembelea nyumba za watumishi wa serikali kabla ya kuziuza. Fungu la maintenance liliisha sahaulika zamani. Ni wale viongozi wa juu tu ndio waliweza kulazimisha matengenezo katika nyumba wanazoishi kwa kutumia vifungu wanavyojua wenyewe. Nyumba nyingi zilistahili kuwa condemned. Matumizi ya watumishi nayo yalichangia kwa kiasi kikubwa kuzipeleka katika hali hii. Watu walikuwa wanafunga mifugo kwenye servant's quarter. watu walipoahamishwa walikuwa wanaondoka na vitasa hadi masink! mkuu, hali ya nyumba nyingi ilikuwa mbaya sana.

Sijawahi kutetea utekelezaji wa zoezi zima. Ninachojaribu kufanya ni kuainisha sababu ambazo PENGINE zilipelekea kufikia uamuzi huo. Utekelezaji wake left a lot to be desired. Zoezi lilihitaji matayarisho makini zaidi na transparency.


Viwanja vya Obei vilikuwa vikubwa mno ndiyo maana ingawa nyumba nyingi zilikuwa na vyumba VIWILI vya kulala watu walitoana ngeu kuvipata. Nyumba nyingine ingewezwa kujengwa bila matatizo. hatari ya kufanya hivi ni ku'densify' eneo na kupoteza green character yake which ironically ndiyo inayofanya mahali pawe na value kubwa!

Kampuni inaundwa kusimamia utunzaji wa nyumba za serikali badala ya serikali kufanya hiyo kazi. Swali ni kuwa Kama mishahara haiwezi ongezwa kufikia hali ya soko kwa nini basi nyumba ziliuzwa?

Mishahara ya wafanyakazi ina impact bajeti ya serikali. hii hata hivyo haina maana kuwa watumishi hawana kipato zaidi ya mishahara yao! Serikali hata hivyo haiwezi kufanya maamuzi kwa kubase kwenye speculation ya kipato cha watumishi wake. Inawezekana kabisa kuwa kuna watumishi ambao wangeweza hata kununuua nyumba kumi katika MARKET rates. Hii ndiyo iliyopelekea serikali kuruhusu watumishi kulipa kwa installments ambazo zitaendana na kipato chao. Nyumba ziliuzwa kwa lengo la kupunguza gharama za kuhudumia nyumba hizo maana baada ya kuuza tu, mzigo huo ulihamishiwa kwa mnunuaji.

Naomba ieleweke kuwa sitetei uuzaji wa nyumba bali najaribu kuelezea mazingira ambayo pengine yalipelekea uamuzi huo. Ni juu yenu kuamua kama ni pumba au vipi!

Okay, folks, this is my fix for the day! Narudi kuwa msomaji tu.

FMeS, usibadili uandikaji wako kwa ajili yangu. Hautakuwa wewe tena.
 
FM thanks for your explaination.
City planning has something to do, inapotokea mkuu wa Polisi zote ya Kinondoni anakaa temeke, guess what will happen? Mtu wa kawaida sio sawa na kiongozi wa ngazi ya juu ya serikali au polisi. Mimi am not against kuuza nyumba za wafanyakazi wa chini, am against kuuza zile za mawaziri na wakuu wa polisi.

Na kama umefahamu supply ya nyumba iko limited, then nadhani unakubaliana na mimi hakukuwa na maana ya kuziuza hizi nyumba at all. Because we don't have enough supply to sustain growth ya viongozi, so njia pekee ni kukaa muda wako wa uwaziri ukiisha unabeba mabegi.

Naona wewe unazungumzia nyumba za Chango'ombe na sio za Obei. viwanja vyote vya maeneo ya ufukwe vina appriciate kwa atleast 15% annual. Analysis ingesaidia kuset price ambayo serikali ingepeta faida, compare na sasa ambapo serikali imepata hasara. You look at the holding period kuanzia nyumba kujengwa, then what is ongezeko la thamani ya ardhi annual katika eneo, you add with cost ya ujenzi. That is how you will eveluate nyumba.

Serikali ilafanya uuzaji huu kisiri siri na kiwizi zaidi pasipo walipa kodi kunufaika. kuappriciate maana thamani ya nyumba imeongezeka kwa asilimia ngapi? Obei nyumba ya kawaida ina worth 120K+
 
1. Nia na madhumuni ya kuuza nyumba kwa wananchi na viongozi, ilikuwa ni njema kabisa.

2. Ttaizo limekuwa kwenye utekelezaji, Tanzania as a nation hatujawahi kuwa watekelezaji wazuri wa maazimio ya chama na serikali, kuaniza Azimio La Arusha, uhamishaji wa wananchi vijijini, peration maduka, hatujui utekelezaji.

3. Katika zoezi zima, kuna wananchi waliofadika as intended, na kuna viongozi pia waliofaidika, na kuna abuse zilizofanywa n viongozi na wananchi pia, lakini the abuse asilimia ni ndogo sana kuliko waliofaidika.

4. Kama inabidi, serikali zizipitie kesi moja baada ya nyingine za the abuse, na kuzirudisha na kuziuza kwa the originally intended,

5. Majuu katika maaamuzi ya serikali, siku zote huwa kuna projected risk effect, kwamba huu uamuzi utawaathiri na kuwafaidisha asilimia ngapi ya wananchi, ikionekana kuwa wengi wataathirika zoezi husitishwa, na wengi watafaidika basi hufanyika, kwa mfano FDA inataka kupitisha madawa mapya ni lazima ifahamishwe na wanaohusika wananchi wangapia wanaweza kufa bila sababu kwa kutumia dawa hizo mpya, wao hupima asilimia na kupitisha au kusitisha, sijui kama thta is the case na sisi bongo?

6. Mkuu wangu Fundi Mchundo, mimi ni mwanasiasa tena a very serious one, niko hapa JF kujadili taifa langu, na kujifunza kutoka kwa wengine, na kufundisha pia, nimekuwa kwenye huu mchezo wa bulogu kwa muda mrefu sana, nimeona wananchi wengi sana hapa, wakiingia na kutoka, ninaiheshimu sana michango yako, wewe unaweza kunitukana as much as you want kama ulivyokwisha fanya jana kwenye ile post yako, lakini mimi sina noma ndio cause and effect ya kuwepo hapa ili kuhesabiwa as I do, na ndio siasa hiyo ninayoipenda sana, kwa hiyo usiwe na wasi wasi ndugu yangu, wewe tundelee hapa kumkoma nyani na ni matumaini yangu kuwa utabadili uamuzi wako wa kutoka na kubaki, hapa uwanja wa Golani yaani Jambo Forums.

Ahsante Mkuu.

ES = Emergency Sysstem.
 
Mkuu wangu Fundi Mchundo, mimi ni mwanasiasa tena a very serious one, niko hapa JF kujadili taifa langu, na kujifunza kutoka kwa wengine, na kufundisha pia, nimekuwa kwenye huu mchezo wa bulogu kwa muda mrefu sana, nimeona wananchi wengi sana hapa, wakiingia na kutoka, ninaiheshimu sana michango yako, wewe unaweza kunitukana as much as you want kama ulivyokwisha fanya jana kwenye ile post yako, lakini mimi sina noma ndio cause and effect ya kuwepo hapa ili kuhesabiwa as I do, na ndio siasa hiyo ninayoipenda sana, kwa hiyo usiwe na wasi wasi ndugu yangu, wewe tundelee hapa kumkoma nyani na ni matumaini yangu kuwa utabadili uamuzi wako wa kutoka na kubaki, hapa uwanja wa Golani yaani Jambo Forums.

Nakubali ilikuwa over the top! I apologise profusely. Ndiyo maana nimeamua kukaa pembeni maana naona hivi vitu vinaingia under my skin bila sababu yeyote. I should have behaved better.
 

Mkuu FME, one thing i like about you,is you stand on what you believe. Hapo umeongea point tupu. Jee serikali walifanya analysis gani prior kuziuza? That is $100 million question
 
Tatizo watu hamtaki kuface ukweli . Viongozi wetu walikuwa wanajua nini wanafanya walipofikiria kuuza hizi nyumba . Ni jambo ambalo walishaliona miaka mitano iliyopita , kwa nini walisubiri mpaka karibu na mwisho wa term ya Mkapa ?

Nashindwa kuelewa sababu zinazotolewa na watu kujustify vitendo vya kizandiki vilivyofanywa . Zoezi zima lilikuwa tainted na usiri mkubwa , ni nani aliyesema kazi serikalini kitumike kama kigezo cha kununua hizo nyumba ? Vipi kuhusu wafanyakazi wengine wa serikali waliostaafu huko nyuma ?
 

Mimi nakubaliana na wewe kabisa kuwa hakuna sababu yoyote ya maana iliyotolewa inayoweza kuhalalisha huu uuzaji. La muhimu kueleweka hapa ni kuwa sheria ilipindishwa ili kufanikisha malengo yao, i.e. kununua nyumba za umma kwa bei wanayoitaka wao.
 
Kubwajinga ,

Ni muhimu kwa watu kujua ya kuwa nchi aiongozwi na emotions..
 
1. Wakuu kuuzwa kwa nyumba kumewasaidia wengi sana, kuliko hata mnavyofikiri au kuhisi, wafanyakazi wengi sana wa serikali na hata mawizara, wamefaidika sana ninaisema hii tena kwa uhakika sana kwa sababu I know a lot of people ambao ni wa hali ya chini walionufaika na hili zoezi.

2. Kuna mengi sikubaliani na Mkapa, lakini I am not so sorry kwamba kwenye hili la kuuza nyumba, ninakubaliana na Mkapa 100%, wakati akiongea kuhusu hiii ishu I looked in his face, na siasahau point moja muhimu aliyoisema, kuwa "...mimi Mkapa, nliamua kwa kuwajali wananchi na not anything else, and I stand for my decision....." I mean nimezoea viongozi wetu wakipiga hadithi, lakini this was a very serious tone kutoka kwa head of state taking responsibility.

3. Pia kuna masharti ninayoyaheshimu kwenye ununuaji, kwa mfano huwezi kuiuza for the next 25 years, na ukishindwa kulipia mortgage, nachukuliwa na serikali I like that ingawa najua sio rahisi.

Now let me touch the point kuhusu utekelezaji, kwa wasomi bongo it is about time sasa wanahitaji kuja na solution of why wabongo tunaweza sana kuyaendesha mashirika ya nje tukipewa kazi huko, lakini hatuwezi ya nyumbani? WHY?

I mean tizama our history, we have failed na utekelezaji wa everything tulichojiamulia as a nation, Azimio La Arusha, kuhamisha wananchi vijiji vya ujamaa, Elimu, operation maduka, haiwezekani maneno ya Mwalimu yakawa mazuri kwenye kusoma tu, why not kutekeleza? yaaani mapka siasa za vyama vingi zimetushinda, WHY?
 

Maneno mazito hayo mkuu FMES, napenda kuongezea neno moja tu hapo kwenye "utekelezaji wa everything positive tulichojiamulia as a nation..."
 
Maneno mazito hayo mkuu FMES, napenda kuongezea neno moja tu hapo kwenye "utekelezaji wa everything positive tulichojiamulia as a nation..."

Sasa mnaanza kulipuka. Kuna vitu gani tulivyojiamulia as a nation?

Ujamaa, operation maduka, UPE, Azimio la Arusha n.k ni mawazo ya mtu mmoja au wachache. Na mawazo yenyewe ni Essay za shuleni ambazo hazina application yoyote katika real life.

Tukirudi kwenye mada ni upuuzi wa hali ya juu kwa serikali kuweka masharti kuwa nyumba ziuzwe baada ya miaka 25. Kuna mtu kainunua nyumba akiwa Tanga lakini akistaafu anataka kurudi kwao Njombe. Je ni lazima asubiri miaka hiyo 25?
 
Wengine wamesha anza kuziuza,pamoja na kupewa masharti wasuize mpaka ifikie miaka 20.lakini wajanja wameanza kuwauzia wafanya biashara wakubwa eti anampangishia kwa miaka 20,
Kumbe tayari kesha chota nyumba wameuziwa na serikali mln 30 wanauza mln 500 masaki msasani nk
 

tupe majina ya waliokwisha fanya huo mchezo,au ni nani unayemfahamu amenunua kati ya hizo nyumba
 
1. Haya maaamuzi kama u-China, yalifanywa na viongozi, kiongozi, na some-areas sisi wananchi, sasa kama China yalifanikiwa, ni kwa nini kwetu hayakufanikiwa? Ndipo tunaposema ni tabia yetu wabongo kutokuwa watekelezaji wazuri.

2. Now lets say, argument yako inasimama kuwa yalikuwa maaamuzi mazuri kwa Essay tu za darasani, toka tuachane nayo ni maaamuzi gani mapya as a nation tumeyafanya na kufanikiwa ili ku-make an academic case mbele ya watu wenye akili kuwa maaamuzi ya zamani, kanza yalikuwa sio collectivelly as society na kwamba yalikuwa mazuri tu kwenye karatasi, as of your claim?

3. Masharti ya uuzwaji wa nyumba hizo, ni absolutely a none- ishu, the ishu ni kama it was okay kuziuza period ukisha-establish hiyo kwanza then unaweza kuhamia kwenye masharti, kwanza tukubaliane kwenye uamuzi wa kuziuza.
 

Hebu tupatie hizo data za hao wengi ni kiasi gani ya millioni 37 ya watanzania wote. Tuache porojo na propaganda.


Nitashangaa kama kuna lolote usilokubaliana na serikali ya CCM, sasa na zote zilizopita. Maneno ya Mkapa hayana uzito tena baada ya kufichuka kuwa sio safi, bali mpuuzi kiasi cha kuweka vioski ikulu.


3. Pia kuna masharti ninayoyaheshimu kwenye ununuaji, kwa mfano huwezi kuiuza for the next 25 years, na ukishindwa kulipia mortgage, nachukuliwa na serikali I like that ingawa najua sio rahisi.


Prove to us kuwa hayo masharti yalikuwepo na yanatekelezeka.



CRDB iliendeshwa na mbongo na kupata mafanikio tunayoyaona hivi sasa. Dr. Rashid juzi tena akawa anataka kuifufua Tanesco, siasa za ufisadi zikazidi uwezo wake sababu ya issue ya Richimondi. Kwa kifupi ni kuwa, Watanzania hawashindwi kuitumikia nchi yao vema kama wafanyavyo nje, ni siasa na uongozi mbaya wa CCM ndio unaoimaliza nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…