Ufisadi wa watangazaji redio

Ufisadi wa watangazaji redio

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
707
Nakumbuka kuna wakati wanamuziki wa kizazi kipya walikuwa wakilalamika kwamba watangazaji (presenters) wa vituo vya redio walikuwa wanataka kulipwa pesa nyingi ili waweke nyimbo zao kwenye vipindi vya redio wanavyitangaza.

Kwa wale waliosomea uandishi wa habari zama zile za "old school", hii inaitwa "breach of ethics" ambayo, kwa jina lingine, inaitwa "payola", yaani, mtangazaji kulipwa pesa ili ashupalie jambo fulani. RUSHWA! UFISADI!

Je, hali hii bado inaendelea?

Je, wasanii chipukizi wa kizazi kipya bado wanakabiliwa na hali hii, kwa kuwa watangazaji (presenters) ndio wamegeuka kuwa mameneja wa wasanii wakongwe?

Naomba kuwasilisha hoja.
 
Back
Top Bottom