Mwanamakunda
Member
- Apr 1, 2021
- 19
- 91
Wanabodi hii nimeikuta kundi Moja la UVCCM, Rais Magufuli kafa na uzalendo wake, wateule wake wameanza kupiga deal.Kufa kufaana
KASHFA YA UFISADI MKOA WA KILIMANJARO
Mnamo tarehe 19 March Mwaka huu 2021 ziliibuliwa taarifa za kuwepo kwa ukiukwaji wa sheria ya ukusanyaji ushuru na kodi katika moja ya mpaka wa nchi yetu katika wilaya Mojawapo mkoani humo, Taarifa hizo ziliibuliwa na whistleblower (Mfichuaji) maarufu katika mtandao wa Twitter anayetumia jina la kivuli Goodluck Haule (@RealHauleGluck) zikidai amepokea taarifa nyeti kutoka kwa maafisa wazalendo katika ofisi za mipaka yetu kutoka wilaya ya Rombo.
Haule anadai amedokezwa juu kukamatwa kwa simu zaidi ya 2,765 zilizoingizwa nchini kwa njia ya panya kisha kukamatwa na maafisa ya usalama wa mipaka hiyo wakishirikiana na Maafisa kodi baada ya kupokea taarifa za siri toka kwa raia wema.
Haule anadai mnyetishaji wa tukio hilo ni mtu toka idara nyeti mkoani hapo alieshiriki katika zoezi hilo na task force hiyo, Na baada ya simu kukamatwa RC Mghwira aliingilia kati kwa kuanza kuwapigia simu maafisa hao waziachie mara moja simu hizo na mmliki wake ndugu Joseph Mafie kwani ni "Kijana Wake wa Kazi" ,ndipo maafisa hao waligoma na kumjuza Meneja wao wa Mkoa ambae nae alileta pingamizi dhidi ya maelekezo ya RC Mghwira akaishia kutishiwa kuswekwa Rumande kwa muda usiojulikana, Hata hivyo Meneja huyu kichwa ngumu alikaidi tena maelekezo hayo ya RC Mghwira aliekuwa amefura kwa jazba.
Suala hilo lilitua mezani kwa mkurugenzi Mkuu wa TRA Nchini ambae nae aliliwasilisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dotto James kisha likafika mikononi mwa Waziri Phillip Mpango (Kwa Sasa Makamu wa Rais) ambae bila ajizi aliagiza simu hizo zitaifishwe na zipigwe mnada kwa mujibu wa sheria za Nchi.
Pamoja na uwepo kwa agizo la Waziri Mpango (Makamu wa Raisi) bado RC Anna Mghwira ameendelea kutunishiana mabavu na maafisa wa TRA Kilimanjaro akizuia mnada huo usifanikiwe.
View attachment 1740443View attachment 1740444View attachment 1740445