Ufugaji kuku sio mwanzo wa utajiri pekee, unaweza ukawa mwanzo wa umasikini wa uhakika. Zingatia yafuatayo ili upate mema kupitia kuku

Ufugaji kuku sio mwanzo wa utajiri pekee, unaweza ukawa mwanzo wa umasikini wa uhakika. Zingatia yafuatayo ili upate mema kupitia kuku

Joined
Sep 6, 2018
Posts
93
Reaction score
290
Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa sana la watu kuweka ndoto za mafanikio kwenye swala zima la ufugaji kuku, swala ambalo watu wengi wanakosea kuingia kwenye ufugaji bila tathmini za kina HASA juu ya gharama na changamoto za ufugaji huo. Mara nyingi huwa tunaingia na mawazo chanya ya kufanikiwa haraka sana mara tu tunapoanza kufuga.

Ukweli ni kwamba hakuna kitu chenye faida kisichopitia hasara wala changamoto.

Changamoto kubwa ambayo wengi tunaisahau ni gharama za kuwatunza hao viumbe na kama tunazifahamu basi hatuzitafakari kwa kina na mwisho wa siku tunapoanza kufuga tunajikuta tunaanza kutumbukia kwenye utumwa wa kutoa pesa za chakula na madawa ya kuku bila kupenda ama kutarajia. Kuku ni viumbe na wanahitaji chakula bora pamoja na afya njema.

Changamoto kubwa mbili ni:
1) Gharama ya chakula ambayo huwa ni asilimia 75 ya gharama ya ufugaji kuku.

2) Gharama ya matibabu na kinga ambayo hufikia karibu asilimia 5 ya ufugaji wako.

Gharama hizo ni za matunzo ukitoa gharama za ujenzi wa banda pamoja na miundo mbinu.

Naomba nikupe mbinu za kupambana na changamoto hizo nilizo zitaja:

Kwa changamoto ya chakula; Unaweza ukatengeneza chakula cha aina yoyote ya kuku unayefuga kwa kutumia malighafi zilezile zinazotumika kutengenezea chakula kiwandani, kwa kufanya hivi utaokoa gharama karibu asilimia 60, yaani kama ulitakiwa ulishe kuku wako chakula cha sh 1,000,000 basi utajikuta kwa kutengeneza mwenyewe utatumia sh 400,000 kutengeneza chakula chenye ubora uleule wa chakula cha milioni 1.

Kwa changamoto ya maradhi pamoja na kinga unashauriwa uzingatie sana usafi wa jumla kwenye ufugaji wako, usafi huo ni kuanzia wewe mwenyewe, mazingira ya ndani na nje ya banda hasa uhakikishe banda liwe kavu, chakula pamoja na maji safi. Hii ni pamoja na vyombo vya chakula na maji kuwa safi muda wote, cha mwisho ni kuzingatia chanjo kwa wakati.

Kumbuka: Kutozingatia chakula bora cha kuku ni kujihakikishia ukosefu wa kuku bora wasiofaa sokoni na kuwa mzembe dhidi ya afya za kuku ni kujihakikishia msiba wa kuku wako wote.

UKIZINGATIA HAYO UTAJIKUTA UNAIFIKIA ILE HAZINA KUBWA SANA YA UTAJIRI ILIYOJIFICHA KWENYE UFUGAJI AMBAYO WENGI WAMEINGIA HUKO BILA UTASHI na KUIKOSA NA KUJIKUTA WANATAJIRISHA WENGINE NA WAO WAKIISHIA KUWA WATUMWA.

Kwa ushauri na pia malighafi za kutengeneza chakula cha kuku aina yoyote basi tuwasiliane.

Meet the Brahma rooster, the king of all chickens!.jpg
 
Hivi unaweza jitengenezea chakula bora kama cha silverland.Hats ufanyeje ile formula ni noma.Labda uende SUA ukafanyie PhD. Aisee ilw formula sijaona mbongo alieiweza.Piga UA chakula cha silver land hukikwepi kama kweli wewe in mfugaji.
 
Hivi unaweza jitengenezea chakula bora kama cha silverland.Hats ufanyeje ile formula ni noma.Labda uende SUA ukafanyie PhD. Aisee ilw formula sijaona mbongo alieiweza.Piga UA chakula cha silver land hukikwepi kama kweli wewe in mfugaji.

Hivi kwa hizi akili zako hata kama utapewa formula ambayo ni bora kuliko silva land utaamini?Kwani hawa jamaa wametoa mbinguni?Wandugu tuache fikra mbovu kama hizi tunajichelewesha.

Ulevi wa brand name ni mbaya sana,kwa wewe kama mtu akichukua kiroba cha silver land akaweka humo chakula cha falcon utaendelea tu kusifia silver land kumbe kilichomondani sicho.

Jifunze kwa kuuliza wengine itakusaidia sana kwenye ufugaji kuliko kuendelea kukariri.
 
Sidhani kama kuna shughuli yoyote inayokosa hasi na chanya, cha msingi ni kuzingatia tu kanuni za shughuli husika.

Mafanikio yoyote ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii, ukiacha mambo yaende tu yenyewe alafu usubiri manufaa utakuwa unafanya mazingaombwe.
 
hi

Hapana bado sijafanikwa kumiliki hii mbegu mkuu
Duhh inapatikana mitaa gani tuifuatilie maana sisi wengine tunaona utamu wa ufugaji wa kuku kutokana na kufuga kwa style uliyoisema , mimi sinunui chakula cha kuku madukani , natengeneza mwenyewe
 
chakula cha kuku kivipi ? au mnamaanisha makuku ya kizungu.mbona kuku wa kienyeji alfajiri tu wanafunguliwa wanaingia mitaani jioni wanarudi wenyewe wakiwa wameshiba au mimi ndio sielewi
Mkuu ukiwa na kuku 300 utawafungulia wakazurure? Huyu anazungumzia ufugaji kuku wawe wakizungu au kiswahili wrote wanahitaji chakula bora.
 
Back
Top Bottom