Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,120
Mkuu kama vipi itabidi unipe contact yako, siku ukipata mbegu bora zaidi nitaomba unishtue na mimi maana natarajia kulima mwakani Mungu akinijalia.
Na average mbegu wanauzaje kwa kilo? Nasikia pia ufuta mweupe ndo unalipa zaidi, kama ukipata mbegu yake itakuwa nzuri zaidi.
Kuhusu mvua nimesikia ufuta hauhitaji mvua nyingi kama mahindi, zaidi mvua inahitajika sana katika zile phase za mwanzoni kabisa, ni kweli??
Mkuu MalafyaleP msaada kama ukipata mbegu bora zaidi za ufuta.
Nimejipanga kuhudhuria maonesho ya nane nane mwaka huu popote pale yatakapofanyika. Hopefully nitapata something.
Mtwara wana kituo cha utafiti kinaitwa NALIENDELE ndiko nilikopata
Asante mkuu nitajaribu kuwasiliana nao.
Mkuu naomba nikuulize lastly, Kutokana na uzoefu ulionao hadi sasa, unafikiri kwamba unaweza zalisha zaidi ya kg 400 pa ekari kama ilivyokuwa mwanzo??
Sorry kwa usumbufu mkuu, am just too curious to know all about sesame.
Hivi Malila yuko wapi siku hizi?
nipo mkuu,haya ni majirani ya kupanda,niko porini mkuu napeleka mbolea na vifaa.
Tuko pamoja wadau wanataka nondo za UFUTA
CC Rocky
nipo mkuu,
haya ni majirani ya kupanda,niko porini mkuu napeleka mbolea na vifaa.
Mkuu wangu ni kweli ulipotea sana!unajiandaa kupanda nini mkuu?mimi nataka nijaribu mahindi kama heka 5 hivi,ila ni eneo jipya,ndio namalizia kung'oa visiki hapa!ni maeneo ya Msowero!sijajua litanipaje mavuno,maana wenyeji wanadai shamba jipya kwa mahindi utoa mavuno hafifu,ila mleta mada hapa amenidokeza shamba jipya ustahili kutoa mavuno mengi zaidi!mimi target yangu nipate angalau gunha 50 tu kwa heka zote 5
Shamba jipya halina shida, unachotakiwa kuzingatia tu ni kwamba hakikisha unapitisha tractor mara mbili kwa kutumia jembe kubwa, unalima mara ya kwanza unaacha mvua inanyesha na majani/magugu yanaoza halafu ndo unalima mara ya pili and then unapanda ili kuufanya udongo uwe laini na kurahisisha mizizi kupenya.
Wasi wasi wangu ni kwamba unaweza kuchelewa kupanda kama hujapitisha tractor hata ile mara ya kwanza mpaka sasa.
Asante mkuu,kwa kweli kwa sasa naweza nikachelewa kupanda kama ulivyosema,maana bado tractor halijapita hata mara moja na msimu ndio huu hapa!je nikijaribu kupanda hivyo hivyo kwa kupitisha tractor mara moja tu,nitakosa hata gunia 5 kwa heka mkuu?

Itategemea na aina ya udongo, kuna udongo unakuwa na rutuba lakini ni kama tifu tifu huo ni mzuri hata kwa kupitisha tractor mara moja kwa jembe kubwa and then unapiga harrow, usikate tamaa kwa kuanza unaanza tu hata usipofanikiwa sana mara ya pili utajua ulikosea wapi.

Mkuu tunafanana na mimi nategemea kulima mara ya kwanza mwisho wa mwezi na mahindi pia. Kikubwa pamoja na kanuni hiyo aina ya udongo itachangia, kwingine udongo ni mgumu au sio tifu hivyo angalia hilo pia. Lakini pia kuna mbegu ile ya miezi 3 ndiyo nitayoitumia maana hizi mvua sio za kutumainia. Ushauri zaidi kwa wenye ujuzi.
Asante sana Mama Joe ,kuhusu ili la mbegu,kuna wakulima wa eneo husika (wenyeji) wamenionya eti kua mbegu zinaendana na eneo husika,si kila mbegu ya mahindi inakubali popote!je kuna ukweli wowote hapo?
Duh na mie ndo ninajifunzia kwako kwavile ninawenyeji nao wanalimu nitaulizia kwao walau kwa mwaka huu kwanza irudi hela na nipate cha kulishia kuku. Pamoja sana
Sawa Mama Joe !Lets hope for the best