Ufugaji Nguruwe Kibiashara sio rahisi ila unawezekana🙂

MalafyaleP

Senior Member
Joined
May 23, 2013
Posts
187
Reaction score
387
Habarini za mwaka mpya wana Jf!

Baada ya muda mrefu kuto post makala humu (nimekuwa busy kwenye media zingine kama instagram, utube,whatsap,telegram..),acha leo nichangie kidogo maana nimeona post nyingi kuhusu ufugaji nguruwe zenye mapungufu. Wakongwe wa Jf watanikumbuka maana nime post sana makala za ufugaji humu miaka hadi kumi iliyopita.

Ufugaji nguruwe kibiashara sio rahisi ila unawezekana.Ugumu unakuja kwa sababu ni biashara na biashara zote zina kanuni ili kujipa uwezekano wa kufanikiwa. Ili uweze kufanikiwa katika ufugaji nguruwe kuna maeneo makubwa mawili:

A.Uzalishaji
Uzalishaji wenye tija unategemea mbegu na matunzo. Matunzo ni mambo yanayohusisha mazingira ya kuishi wanyama, lishe sahihi, chanjo/tiba na utarartibu wa kuzuia magonjwa kuingia kwenye mradi.

B. Masoko
Hakuna namna mradi wako utadumu bila kuuza bidhaa zako. Biashara yoyote haiwezi kudumu kama hakuna mauzo. Wafugaji wengi huanza ufugaji bila kufanya utafiti wa soko na miradi yao hukwama

Hivyo kama unataka kufanya biashara kwenye ufugaji nguruwe chukua hatua hizi
1. Tafiti kuhusu ufugaji nguruwe kupitia machapisho mbalimbali kam vitabu,makala mitandanoni kama google,instagram na utube.

Hii itakusaidia kuuelewa ufugaji na changamoto/fursa zilizopo.

2. Pata ushauri toka kwa wafugaji wazoefu. Kuna faida kukutana ana kwa ana au kwa namna nyingine na mtu mwenye uzoefu kwenye ufugaji ukaweza kujadili nae na kujifunza mambo muhimu. Hata kama utahitajika kulipia huduma hiyo fanya.Ni muhimu sana kwako

3. Tafiti kuhusu soko la bidhaa za nguruwe. Hapa fanya utafiti wewe binafsi ndugu,usitegemee maneno ya kuambiwa. Soko la bidhaa za nguruwe lipo ila haina maana soko la bidhaa zako wewe lipo linakungoja!!

4. Amua bidhaa utakazozalisha na weka malengo kulingana na soko la bidhaa zako

5.Anza mradi kwa kuongozwa na mshauri mzoefu. Kila kitu kinategemea malengo yako:aina ya mbegu,ukubwa wa mradi,soko......

Ni waandishi pia wa kitabu cha ufugaji nguruwe cha kiswahili rahisi kwa kila mtanzania 'Kanuni za Ufugaji Nguruwe wenye tija'

Waweza wasiliana nasi kwa 0789412904/0754393838 kwa simu au whatsap. Tusipopokea andika ujumbe tutakupigia.
 
Habarini za mwaka mpya wana Jf!
Baada ya muda mrefu kuto post makala humu (nimekuwa busy kwenye media zingine kama instagram, utube,whatsap,telegram..),acha leo nichangie kidogo maana nimeona post nyingi kuhusu ufugaji nguruwe zenye mapungufu. Wakongwe wa Jf watanikumbuka maana nime post sana makala za ufugaji humu miaka hadi kumi iliyopita.
Ufugaji nguruwe kibiashara sio rahisi ila unawezekana.Ugumu unakuja kwa sababu ni biashara na biashara zote zina kanuni ili kujipa uwezekano wa kufanikiwa. Ili uweze kufanikiwa katika ufugaji nguruwe kuna maeneo makubwa mawili:
A.Uzalishaji
Uzalishaji wenye tija unategemea mbegu na matunzo. Matunzo ni mambo yanayohusisha mazingira ya kuishi wanyama, lishe sahihi, chanjo/tiba na utarartibu wa kuzuia magonjwa kuingia kwenye mradi.
B. Masoko
Hakuna namna mradi wako utadumu bila kuuza bidhaa zako. Biashara yoyote haiwezi kudumu kama hakuna mauzo. Wafugaji wengi huanza ufugaji bila kufanya utafiti wa soko na miradi yao hukwama

Hivyo kama unataka kufanya biashara kwenye ufugaji nguruwe chukua hatua hizi
1. Tafiti kuhusu ufugaji nguruwe kupitia machapisho mbalimbali kam vitabu,makala mitandanoni kama google,instagram na utube.
Hii itakusaidia kuuelewa ufugaji na changamoto/fursa zilizopo.

2. Pata ushauri toka kwa wafugaji wazoefu. Kuna faida kukutana ana kwa ana na mtu mwenye uzoefu kwenye ufugaji ukaweza kujadili nae na kujifunza mambo muhimu. Hata kama utahitajika kulipia huduma hiyo fanya.Ni muhimu sana kwako

3. Tafiti kuhusu soko la bidhaa za nguruwe. Hapa fanya utafiti wewe binafsi ndugu,usitegemee maneno ya kuambiwa. Soko la bidhaa za nguruwe lipo ila haina maana soko la bidhaa zako wewe lipo linakungoja!!

4. Amua bidhaa utakazozalisha na weka malengo kulingana na soko la bidhaa zako

5.Anza mradi kwa kuongozwa na mshauri mzoefu. Kila kitu kinategemea malengo yako:aina ya mbegu,ukubwa wa mradi,soko......

#Malafyale Farms tuna makala mbalimbali pia kwenye ukurasa wetu wa instagram: https://instagram.com/malafyalepigfarms?igshid=4koq1jc1dabp

Ni waandishi pia wa kitabu cha ufugaji nguruwe cha kiswahili rahisi kwa kila mtanzania 'Kanuni za Ufugaji Nguruwe wenye tija'

Waweza wasiliana nasi kwa 0789412904/0754393838 kwa simu au whatsap. Tusipopokea andika ujumbe tutakupigia.
Ndagha kikolo.
Hebu tupe maarifa zaidi tufaidike
 
Rafiki yangu Kitimoto katika pozi👇😁😁😁
16392258281641.jpg
 
Mkuu samahani najiandaa kuanza ufugaji huu lakini nataka kujua bei
Mfano nataka kuanza na nguruwe wawili kama cross ya largewhite na landrace
Wawe na umri ya kupandishwa niwachukue wakiwa tayari wamepandwa
nijiandaeje kwa sh ngapi boss

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Hapo namba #8 nimeuliza ujinga?
Mbona kama hujaona sababu ya kunijibu

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
chief usinikasirikie.Mambo mengi. Hata hivyo makala hii haikuwa na maudhui ya kuuza nguruwe.
1. Hatuna wanyama wa umri huo katika bidhaa zetu
2.Kwa mahitaji ya bidhaa zetu zozote wasiliana nasi kwa namba tulizoweka kwenye makala
🤝
 
Changamoto zake? Utafutaji wa soko etc. Tueleze mkuu
Kitu cha muhimu ni usafiri, miundo mbinu ya umwagiliaji. Ukilima nusu heka ya bamia unaweza kuvuna tano za bamia kama umemeagilia vizuri na mbolea ya kutosha.

Unalima heka moja unaigawa leo unachuma nusu hii unayapa siku moja ya kukua kesho unavuna nusu nyingine.

Ndoo moja ya bamia ukifika sokoni wachuuzi wabachukua kwa 50,000.

Pick up ya kwako mwenyewe ni muhimu sana hapa. Hata kama unaishi Mlandizi au Chalinze unaweza kuwahi soko la Kisutu au Kinondoni TX.

Ukishachukua mpunga wako unanunua mahitaji ya nyumbani unarudi porini.
 
Kiongozi..Unalima bamia pekee au mboga gani nyingine zinalipa .?
Unalima bondeni au unatumia maji ya kisima..?
 
Back
Top Bottom