Ufugaji wa Kuku wa Kisasa: Fahamu Mbinu, Faida, Changamoto na Masoko


Mkuu mambo niaje nimefatlia huu uzi kwa umakini mkubwa sana na nimejifunza mengi mno. Inaonekana una weredi mkubwa na mambo haya ya ufugaji wa kuku.

Mimi nina swali kuhusiana na jedwali hapo juu unaweza kutuambia vipimo vya hizo dawa hususani zinazohusisha sindano? Pia itakuwa vema sana kama utaweza kutupatia bei za hizo dawa kulingana na ujazo wake tafadhali.

Natanguliza shukrani zangu za dhati ndugu yangu uendelee kuwa na moyo huo huo wa ukarimu na Mungu atakuzidishia.
 
Asanteni xaaaaaaaaaaana nao ngoja niwaongezee mamisosi ili x-mas wawe wanono vya kutoshe
 

Nahitaji namba zako kaka.
 
Asante sana mkuu, Wakati mwingine nashindwa kuandika kila kitu kutokana na ubusy pamoja na majukumu niliyonayo, ninachofanya ni kuweka vile vitu vya msingi. Dozi na mambo mengngine mengi yapo kwenye kitabu changu cha mwongozo wa ufugaji wa kuku. Dawa nyingi za unga ambozo huchanganywa kwenye maji bei yake ni tsh 5000/=. Kama utahitaji huduma yeyote basi si mbaya ukanitafuta kwenye simu yangu kwa msaada zaidi.
 

Ahsante sana mkuu, nimekupata vizuri nikitulia kwenye hizi siku za karibuni nitakutafuta ndugu yangu. Nashukuru sana
 
So na,i nawezaje kupata nakala ya hicho ndugu zantsan
Niko uganda
 
Zantsan nimeiona jedwali la kinga na tiba hapo juu nimelipenda ila nina mambo ninayotaka kufahamu kwani mimi nimewatotolesha vifaranga 63 wa kienyeji wamebaki 59 kwa maana 4 wekufa kwa 2 kuliwa na vifaranga wenyewe na 2 walikanyagwa na mhudumu wa nyumbani, kwa bahati nzuri nimewachanja. Leo hii wana miezi 2 na nusu( wiki 10) hakuna aliyekufa kwa ugonjwa na ni wazuri wameota manyoya vizuri sana. Kuhusu lishe mimi nawaparazia mahindi na kuchanganya na wadudu fulani waliochangayika na dagaa na starter mash kwa ratio ya 4:2:1(vikombe 4 mahindi yaliyoparazwa,vikombe 2 hao wadudu wakiochanganyika na dagaa na kikombe 1 cha starter mash) nawapa vikombe vy chai 12 vya huo mchanganyiko kwa siku(kikombe 1 kwa vifaranga 5) na kadri wanavyokua nawaogenzea kama watakuwa wamekimaliza chote.Pia kwa kuwa ni kiangazi huku kijijini hakuna majani kipindi hiki nawapa Pharmaxine Chick Plus mara tatu kwa wiki katika maji ya kunywa.Sasa ninaomba niwape nini zaidi ili isitokee tena wakaanza kudonoana kwani sasa yapata wiki ya pili hakudonoana.
 
Last edited by a moderator:

waongezee DCP kwenye mchanganyiko wako... hii ina phosphorus and all essential minerals
 
Last edited by a moderator:
waongezee DCP kwenye mchanganyiko wako... hii ina phosphorus and all essential mimerals

Nini kirefu cha DCP mkuu ili nifanyie kazi ushauri wako kwani baadhi ya maduka ya mifugo wauzaji sio wataalamu.
 
Wakuu habarini, kwa nifahamuvyo mimi, kuna tofauti kati ya Degestible Crude Protein na ile DCP ya Di calcium phosphorus. Kwa munasaba wa aliyeuliza swali aliuliza kitu gani kikitumika husaidi kuwafanya kuku wasidonoane, hapa inayotakiwa ni DCP kama Coturnix alivyojibu lakini si ile ya digestible crude protein bali ni ile DCP ya di calcium phosphorous. Kudonoana kwa kuku mara nyingi kunasababishwa na upungufu wa madini mwilini hasa calcium na phoshorum ndio maana tunapaswa kuwasuppliment aina hiyo ya madini ambayo ina kiwango kikubwa cha madini ya calcium na phosporus ili kuwafanya wasidonoane. Lakini sababu nyingine zinazpfanya kuku wadonoane ni pamoja na mwanga mkali bandani, kulundikano wa kuku wengi kwenye banda kunakotokana na udogo wa banda nk, njia za kutatua tatizo ni pamoja kuwakata midoma au kutumia Dcp na wakati mwingine kuwaning'inizia majani au mboga wakati wa mchana husaidia kuwashughulisha na kuwafanya wasahau kudonoana.
 
nami nimepata kitu early 2014 naanza ufugaji
 

Mheshimiwa Zantsan nashukuru kwa ufafanuzi wako,ila nisingependa kuwakata midomo kwani nahisi watadhoofu kwa kula kwa tabu.Naona nikanunue hiyo DCP(Di Calcium Phosphorus) kwani kipindi hiki ni vigumu kupata majani mabichi ya kutosha na sokoni mchicha ni ghali japo nawapatia kidogo mara mbili kwa wiki.Kwa upande wa banda ni mita 3kwa 3 ila sasa nimewachia katika ua lenye upana wa mita 2 kwa 3 nililounganisha na banda hivyo wanajivinjari ndani na nje kwenye ua ila vifaa vya maji na chakula vipo ndani ya banda labda kama ni mwanga iwe kwa sababu hiyo.
 
Last edited by a moderator:

Mheshimiwa Zantsan nashukuru kwa ufafanuzi wako,ila nisingependa kuwakata midomo kwani nahisi watadhoofu kwa kula kwa tabu.Naona nikanunue hiyo DCP(Di Calcium Phosphorus) kwani kipindi hiki ni vigumu kupata majani mabichi ya kutosha na sokoni mchicha ni ghali japo nawapatia kidogo mara mbili kwa wiki.Kwa upande wa banda ni mita 3kwa 3 ila sasa nimewachia katika ua lenye upana wa mita 2 kwa 3 nililounganisha na banda hivyo wanajivinjari ndani na nje kwenye ua ila vifaa vya maji na chakula vipo ndani ya banda labda kama ni mwanga iwe kwa sababu hiyo.
 
Last edited by a moderator:
na mm pia naomba unitumie kwny email lastking9060@yahoo.com
Jamani naombeni nifafaNue kidogo,kitabu hiki hakitolewi bure bali kinauzwa kwa tsh 60000/=,ukipata hiki kitabu mambo mengi utakuwa ukiyafanya mwenyewe hutahitaji daktari. Pia kupitia kitabu hiki utaweza kudhibiti kwa kiasi kikubwa vifo vya kuku.
 
OK sawa tu mkubwa,utanitafuta kwenye simu nikuelekeze ni namna gani ya kutumia hiyo DCP ili ilete ufanisi mzuri zaidi.
 
OK sawa tu mkubwa,utanitafuta kwenye simu nikuelekeze ni namna gani ya kutumia hiyo DCP ili ilete ufanisi mzuri zaidi.

Nitakutafuta wakati wowote nikishanunua namba zako ni zile zilizopo kwenye post yako yaani 0767989713, 0786989713 na 0715989713 sio? Pia naomba kuuliza kwani kwa sasa maduka ya mifugo kwa miji midogo huwa hwana bidhaa mpaka uweke oda wakuletee nimekuta Broiler Premix yenyeCalcium 26% na Phosphorus 9% na elements nyingine je ni chukue au niweke oda waniletee?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…