SoC01 Ufugaji wa kuku wenye tija na matumizi ya teknolojia

SoC01 Ufugaji wa kuku wenye tija na matumizi ya teknolojia

Stories of Change - 2021 Competition

Quavohucho

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2020
Posts
798
Reaction score
2,028
Ni jioni tulivu ,jumapili ya tarehe 14/7/2021 ni siku niliyoamua kwenda kumtembelea mjasiliamali anayejihusisha na ufugaji wa kuku wa kisasa , ilikuwa safari nzuri sana toka maeneo ya iringa mjini hadi iringa vijijini, kwa mfugaji na mjasiliamali huyu maarufu kama mzee mwenda ,

Ilikuwa ni safari ya dakika chache tu, baada ya kufika na kujuliana hali na wenyeji wangu na kupumzika kidogo na kupoonza koo kwa maji baridi, ndipo tukaanza mazungumzo kwa kiasi kikubwa yalikuwa ni kuhusu ufugaji wenye tija na changamoto zake na je faida inapatika,

Mzee huyu anafuga kuku wastani wa kuku kama 500 katika mabanda tofauti tofauti kuna mabanda ya kuku wa nyama,mayai na vifaranga, eneo hili la mabanda ya kuku limejawa na ubize wa shughuri nyingi kama kusafisha mabanda ,kuweka vyakura, kuwapa chanjo kuku, kutoa mayai ,kuongeza vyanzo joto kwenye vifaranga ,kuwaondoa kuku waliokuwa tayari, n.k

Mzee huyu alinambia hizi ni shughuri za kila siku licha ya kuajiri vijana wa kusaidia kazi lakini huwa wanachoka sana na kukumbana na changamoto mbali mbali kama;

  • kushindwa kufanya shughuri nyingine za kiuchumi kama kilimo,
  • kushindwa kuweka vyanzo vya joto na kutoa kwenye mabanda kwa wakati,
  • kushindwa kujua kama vyakula vimeisha katika vilishio,
  • pia kushindwa kusawazisha mwanga katika vyumba vya kuku kwa wakati
  • kukosekana kwa rekodi za taarifa mbali mbali za kuku na vifaranga
  • kusahau ratiba sahihi ya chanjo ya magonjwa ya kuku,

Changamoto hizi upelekea vifo vya kuku na hasara kubwa sana na kuharibu mtaji, hivyo kushindwa kufika malengo ya kiuchumi aliyojiwekea , licha ya kutumia mtaji mkubwa katika kuanzisha shughuri hii lakini faida yake ni ndogo sana;

Baada ya kumaliza ziara hii fupi iliyojaa mafunzo mengi nilirudi nyumbani, Nikiwa na takafakuri kubwa sana!

JE SULUHISHO LA CHANGAMOTO HIZI NI NINI?

Kutatua changamoto hizi na kupunguza kazi za mikono na kukuza faida katika sekta hii ni nini kifanyike ??

TEKINOLOJIA!
Njia kuku ya kutatua changamoto hii ni tekinojia , na ni moja ya sekta inayokuwa kwa kasi sana ulimwenguni huu

Hivo basi kwa kuhusisha tekinolojia katika ufugajia wa kuku kutaleta tija kubwa sana kukuza hii sekta

MIFUMO YA KIDIJITARI
Mifumo hii ni mifumo ya kikompyuta ambayo ubuniwa ili kulahisisha shughuri mbalimbali katika maeneo kusudiwa.

Katika ufugaji wa kuku tunaweza kutumia mifumo hii ili kutatua changamoto kadhaa za ufugaji wa kuku,

Mfumo wa simu janja unaosaidia shughuri za ufugaji wa kuku
(Automatic chicken keeping app)

Mfumo huu huweka katika simu za kisasa maarufu kama( smart phones) na kutupatia taarifa na kupunguza shughuri nyingi zitumiazo nguvu katika ufugaji

Mfumo huu unaunganishwa moja kwa moja na banda la kuku na kufanya shughuri mbali mbali bila ya mtu kuwepo kwenye banda
Mfano ,
1: upimajia wa joto kwa kutumia sensor za joto
2:Upimaji wa unyevu kwenye banda
3:Upimajia wa uzito wa vyakula katika vifaa vya kulishia ili kujua kama vyakula vimepungua ili viongezwe
4: kuweza kutunza taarifa za kuku kama umri, mda wa chanjo,idadi ya kuku, uzito nk, katika kanzudata,
5:kuweza kuwasha na kuzima mwanga bila kuwepo kwenye banda kwa kutumia sensor za mwanga
6: kutoa taarifa kwamba mda wa kutoa chanjo kwa kuku umefika,
7:kuwepo kwa kanzudata kwa ajiri ya taarifa mbali mbali,

Taarifa hizi zote kutoka kwenye banda zitatumwa moja kwa moja kwenye mfumo uliopo kwenye simu kwa kutumia kiafaa kiitwacho
(GSM card)

-Kwa kutumia mifumo ya namna hii katika sekta ya ufugajia, kuta Fanya shughuri Iwe rahisi na nguvukazi kutumiaka kidogo na kwa ufanisi mkubwa, huku faida kubwa ikitengenezwa (ufugaji wenye tija)

-Pia kwa kutumia mifumo hii tutakuza kiwango cha ajira katika sekta ya teknolojia (watengeneza mifumo) na kuongeza kiwango cha ufugaji wenye tija katika jamii za kitanzania,

-Kutumia mifumo hii kutaruhusu mfugajia kuendelea na shughuri nyingine za kiuchumi huku taarifa za banda la kuku wake akizipata moja kwa moja katika simu janja yake.

-Kutumia mifumo hii kutakuza tekinolojia katika taifa letu.

- kutumia mifumo hii tunaweza kupata taarifa mbali mbali kuhusu kuku zitakazo tumika kwenye tafiti mbali mbali za kielimu ikiwemo mda sahihi wa chanjo za magonjwa ya kuku
-kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na wahitimu wa vyuo mbali mbali ambapo wataanza kujihusisha na ufugaji wa kuku,

Hivyo basi wajasilia Mali katika sekta ya ufugaji wa kubwa kwa wadogo ili kukuza faida katika sekta hii ni muhimu kutumia mifumo hii ya kidijitari katika shughuri zima ya ufugaji wa kuku lengo ni kutatua changomoto zinazokabili sekta hii katika uliwengu huu wa sayansi na teknolojia na kupelekea mitaji na faida kukua.

IMG_20210714_191236.jpg


IMG_20210714_195952.jpg
 
Upvote 1
Back
Top Bottom