Ufugaji wa Kware haikuwa utapeli bali thinking capacity zetu zilikuwa chini

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Kuna Triend nyingi sana huwa zinaelezea ufugaji wa Kware ulivyo kuwa utapeli na jinsi watu walivyo tapeliwa na kadhalika.

Kwanza Ukweli ni kwamba Mayai yake ni lishe na tiba, shida ni tiba kwa kiwango gani?

Je mtu mwenye kansa akiambiwa ale Mchicha sana maana yake anapona? Hapana inamsaidia tu.

Kware mayai yake yanaliwa kama ilivyo mayai mengine tu.

KWARE KAMA KITOWEO
Hapa ndo ninapo jikita kwamba Ufugaji haukuwa utapeli sema watu wengi walikomaa na mayai ya kutibu mara ukimwi mara Kisukarin

Kware wako aina nyingi na ukipata Jumbo au Giant Quils unaweza zalisha nyama.

Nyama ya Kware inawexa kiwa kitora nyumbani na watu wakashiba na siku ikapita.

Nyama ya kware inaweza chomwa kwenye mabaaa sawa sawa tu na inavyo chomwa nyama ya kuku.

Nyama ya kware inaweza kuwa mbadala wa samaki wadogowadogo wale wanao vuliwa wakiwa bado muda kwenye mabwawa ya Nyumba ya Mungu, Mtera, Ziwa eyasi na kadhalika.

Nyama ya Kware inaweza shindana na nyama ya kuku na hara Ng'ombe sokoni.

Shida kukuu ni kwamba wengi huwa hatutaki kuumiza vichwa hatutaki kuwaza kabisa hatutaki kwenda nje ya Box.

Wengi tuliishia kwenye Mayai basi tukasahau kwamba kware wanaweza kuwa kitoea wanaweza liwa na Ugari nawali na kadhalika.

Kware wanaweza Fugwa kwa ajili ya nyama na wanaweza kupunguza gharama za kununua nunua mboga.


NB: Nawatafuta sana ni ni Box,But na fight niwapate hasa Jumbo niwafuge hasa hawa Giant na Jumbo quills.

NB: Hawa ni Domestic Quails sio Wild quails, walioko kwenye Hifadhi zetu wako tofauti mno na hawa na wanatofautina vitu vingi sana.

NB: Nikijaga kuwapata hawa Giant au Jumbo nitawaleteaga mrejesho ila pia mtu anaweza watafuta ila kwa Bongo sidhani labda nchi kama Zambia au Malawi au Zimbabwe wapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…