Ufugaji wa mamba

Xplorer

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
607
Reaction score
857
Nawapenda sana hawa viumbe,natamani nifuge angalau mmoja "as a pet",ni wanyama rafiki sana tofauti na watu wengi wanavyofikiri,kinachohitajika tu kuzifahamu tabia zao tu,ngozi ya mamba wa miaka mitano mwenye urefu wa 190cm huuzwa hadi $1500,na nyama yake pia ni kitoweo kizuri hivyo inaweza pia ikawa ni fursa nzuri ya biashara kwa wale wajasiriamali. kama unaelewa taratibu za ufugaji wa viumbe hawa pamoja na upatikanaji wa kibali nchini tafadhali msaada wako unahitajika hapa.
 

Dalili za uchawi hizi..mnaanzaga huku mnaishia kufuga fisi.
 

Zamani watu walikuwa wanaanza ukichaa then wanaokota makopo, LAKINI SIKU HIZI WATU WANAANZA KUOKOTA MAKOPO HALAFU BAADAYE WANAKUWA VICHAA....
 
nyama yake ni laini na kwa hapa nchini inapatikana kwenye mahoteli ya kitalii na wanaipata kwa kuagiza kutoka Kenya.
 
vp mayai yake?

Mayai yake yako "very delicate" Ukilibeba juu chini,ukiliweka kwenye mwanga mkali,au ukiliweka kwenye joto zaidi ya 36 degree za centigrade linaharibika,kwa kitoweo sina uhakika kama linafaa lakini linauzwa kwaajili ya kuanguliwa.
 
Mamba na mnyama asiye na urafiki na binadamu kwa namna yoyote ile, bora ya simba na chui, sio mamba, usithubutu kicheza nae hata km umedumu nae miaka 10. Ila anafugika kirahisi sana, anakula chakula kidogo ,maji si mengi sana, kijibwawa kidogo tu kinamtosha. Ukitaka maelezo mazuri km uko dar, nenda tegeta zoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…