Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Changamoto sijakutana nazo bado kutokana na maeneo niliopo, soko la Mbuzi ni la uhakika kila mtu analifahamu, breed nmesema ni kienyeji pure,faida nmeizungumzia ya uzalianaji wa haraka maana bado sijaanza kuuza, nawewe kaa chini Kwa kutulia usome Kwa makini usikurupuke
Umeandika Kama unakimbizwa mkuu ...
Hujasema Ni mbuzi wangapi...
Breed gani?
Changamoto?
Faida ?
Masoko?


Kaa kwa kutulia au ulitaka Tuu tuone unae mbuzi ,kanga na kuku?

Kunywa maji andaa Uzi uliojitosheleza.
 
Umeandika Kama unakimbizwa mkuu ...
Hujasema Ni mbuzi wangapi...
Breed gani?
Changamoto?
Faida ?
Masoko?


Kaa kwa kutulia au ulitaka Tuu tuone unae mbuzi ,kanga na kuku?

Kunywa maji andaa Uzi uliojitosheleza.
Huu ujuaji ndio unaofanya watu wasitoboe,ameelezea kama kuhamasisha wengine.Masuala ya breed,changamoto toa wewe.
 
Jaman huyo kuku hapo mbona amefanana na kocha wa utopolo aliyepita, kweli dunian wawili wawili.
 
Hongera kiongozi
Karibu sana nikisema namaanisha tujitahidini jamani kwenye ufugaji mambo yapo vyema, kikubwa ni good management na uvumilivu ktk kusubiria mazao. nidhamu kubwa sana katika ufugaji na kilimo ni hiyo.
Changamoto zinapotokea usihofu kuuliz kwa walio kutangulia.
 
hongereni sana wote mnaofuga, hivi ile breed ya boer inapatikana wapi kwa hapa tz?

..mchangiaji mwenzetu anaitwa wakaliwetu alisema kuna wafugaji wakubwa wa Mbogo Farms wanasaidia Watanzania ktk kuagiza mbuzi wa Boer kutokea South Afrika. Mbuzi wa Boer, Savanna, na Kalahari, asili yao ni South Afrika.

..nilipowacheki jamaa wa Mbogo Farms nimekuta wana namba 784 785 785, wameitoa kwa watu wenye interest za kununua mitamba ya ng'ombe kutoka katika mashamba yao. Nakushauri ujaribu kuwatafuta ktk namba hiyo labda watakuwa na majibu kuhusu suala lako la mbuzi breed ya Boer.

..Ukishindwa kuagiza Boer, kuna mbuzi mwingine hapa Tanzania na Kenya wa breed ya Galla/Isiollo. Ni mbuzi mzuri, anastahimili magonjwa, anakua haraka, majike wanatoa maziwa mengi,na madume wako active kwelikweli ktk kuwapanda mbuzi jike. Mbuzi wa Galla/Isiollo kwa hapa Tanzania anapatikana zaidi ktk jamii za Wamasai maeneo ya Longido.

..Mbuzi wa Galla huyu hapa:
 
Asante sana mkuu, sasa naanza kuona mwanga. huu uzi ni mtamu sana ila usije kuingiliwa na watoto tu
 
Haya ndugu zangu hili ni ingizo jipya karibuni tujifunze sote.
 

Attachments

  • 20210306_143953.jpg
    265.9 KB · Views: 77
  • 20210306_143956.jpg
    326.4 KB · Views: 77
  • 20210306_144001.jpg
    318 KB · Views: 78
  • 20210306_144032.jpg
    275.7 KB · Views: 70
  • 20210306_144058.jpg
    312.4 KB · Views: 70
  • 20210306_144100.jpg
    267.4 KB · Views: 74
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…