Ufugaji wa Nguruwe

Kwenye bei ya pumba hapo ndio umeniacha hoi.
 
Mtaji mzima wa ufugaji ni shingapi na je utawajuaje mbegu nzuri ya nguruwe?
 
Uli ifanikiwe kufuga Nguruwe kwa usalama nafuu, anza kuandaa chakula kwanza.
Panda Maboga japo ekari moja, chagua mbegu ya boga kubwa na tamu.
Lima huku ukijenga banda la nguruwe.
Hifadhi maboga yako ambayo yanakaa hata mwaka mzima bila kuharibika.
Hapo ndo ulete ngurue wako ambao tayari una chakula asilimia 60.
 
Sikukatishi tamaa ila kwa 300K bora utafute shughuli ingine ya kufanya tu. Ntakupa tip ya bure! Fuatilia biashara ya ndizi mbichi!

Tafta eneo kitaa uanze kusebenza mikungu yako ya ndizi! Kama utamwaga mezani au kuitandaza chini freshi tu. Baada ya miezi miwili utakuja kunishukuru
 
Duh kuna maboga yanayoweza kukaa mwaka mzima bila kuharibika
 
Duh kuna maboga yanayoweza kukaa mwaka mzima bila kuharibika
Ndio yakivunwa yakiwa yamekomaa na yakitunzwa sehemu isiyokuwa na unyevyu unyevu. Nishawahi fuga Nguruwe na chakula kikuu yalikuwa Maboga ya kila Mwaka. Sema nilifuga kienyeji na sio kibiashara.
Ukiyachemsha kidogo na kutia Chumvi kidogo utaflahi Nguruwe wanavyo yachangamkia.
 
Mbona expenses hujazipigia hesabu?
 
nasikia sasa hivi mdudu kashuka bei sababu wanakufa mno
Sijui ila jana maeneo ya Ubungo ilikuwa ileile 11,000/- kwa kilo....na last week nilipita maeneo ya karibu na NIT ilikuwa the same price........
 
Duh kuna maboga yanayoweza kukaa mwaka mzima bila kuharibika
Kuna maboga yakikomaa yanadumu miaka tena sio mwaka. Chamsingi usitoe kile kikonyo chake na usiweke sehemu baridi yataanza kubadili rangi pale chini na kuanzia hapo kuoza. Kisha unamwagia majivu unayaweka sehemu kavu
 
Braza, chakula gani kina-boost ukuaji wa nguruwe watoto kwa haraka sana?
 
Ok
 
Braza, chakula gani kina-boost ukuaji wa nguruwe watoto kwa haraka sana?
Sifahamu mi nilifuga nguruwe kienyeji.
Ila najua sasa hivi ktk ufugaji wa nguruwe wafugaji wanaangalia.
1. Mbegu kubwa ya Nguruwe.
2. Chakula bora ( hili watafute wataalamu wa ufugaji watakusaidia)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…