Wakuu naamini Mungu ni mwema.
Naomba kwa heshima na taahadhima kubwa kupata ABCD za ufugaji wa samaki kwenye mabwaya ya kutengeneza man made Nina imani kubwa kuwa humu wako waatalamu wa kila nyanja na pia ktk hili langu nami niatapata wa kunielekeza nin cha kufanya katika. Mradi wangu huu zipi changamoto na way forward.
Natanguliza shukrani
Si umpe ABCD's hizo, lakini kwa kifupi ufugaji ea samaki unahitaji.Nilikuwa hivyo mwanzo kama wewe, ila nikaona kabla sijauliza watu niingie mwenyewe online kutafuta viji-kozi vidogo vidogo huko Google. Kiukweli nimeanza mwezi wa 4/5 na sasa najua process zote naona nawashinda mpaka wataaalam waliosomea SUA miaka 3. Nilichobakiza ni kuanza tu kazi
Ningekushauri na wewe anza kwanza kujifunza mwenyewe taratibu online, youtube imenisaidia sana halafu baadae unakuja kuuliza swali la moja kwa moja kutoka kwa wataalamu ili wakuelekeze
Si umpe ABCD's hizo, lakini kwa kifupi ufugaji ea samaki unahitaji.
1.Mbegu bora Sato/Kambale
2.Chakula bora (size,nutrient requirement, n.k),inatokana na aina ya ufugaji unaohitaji/fanya.
3.Eneo bora, lisilo na mafuriko, migogoro, linalofikika n.k.
4.Maji bora, yenye Oksijen ya kutosha, pH sahihi n.k.
Muhimu
i.Samaki(Sato uchukua miezi sita kufikia 500g)
ii.Samaki(Sato-madume), huleta tija zaidi kulinganisha na majike.
iii.Chakula cha samaki complete feed kilo moja ni 3500.
iv.Hii ni dondoo nakupa Sato ana life-span ya miaka 9, urefu wa 60cm na ufikia mpaka 4.3kg kwa muda huo.
Mwisho:Sekta bado inakua.