Ndugu JF Doctors, niliwapa taarifa kuhusu majibu ya HIV yenye utata ya mchumba wangu. Napenda kuwataarifu kuwa baada ya kukosa ELISA na WESTERN BLOT katika hospitali ya Rufaa Mbeya, tuliweza kupata vipimo hivyo katika kituo cha Uchangiaji wa Damu Salama ili kuondoa utata huo. Tumeambiwa kufuata majibu baada ya wiki mbili. Hali ya mchumba wangu kisaikolojia ni nzuri kabisa na hana wasiwasi. Nitawapa taarifa baada ya majibu kutoka wiki mbili zijazo. Nawashukuru sana kwa mchango wenu!