Ufumbuzi wa tatizo la kubanduka plaster ya gypsum kwenye Ceiling

Ufumbuzi wa tatizo la kubanduka plaster ya gypsum kwenye Ceiling

Kudasai

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2016
Posts
214
Reaction score
254
Habari wanabodi! Moja kwa moja kwenye mada hapo juu.

Nadhani tatizo hili mtakuwa pia mmeliona kwa baadhi yenu! Nyumba ilipigwa plaster ya gypsum ambapo kama ilivyozoeleka na mafundi wengi gypsum powder huwa inachanganywa na rangi nyeupe ya maji. Kisha ikatumika kuplaster (skimming) Gypsum board. Lakini imepita kama mwaka mmoja hivi ndio nakutana na shida hii ya kubanduka na kudondoka chini!

Picha nimeambatanisha hapa.
Hebu tupeana ujuzi kukabiliana na kadhia hii.
Asanteni
IMG-20201110-WA0000.jpg
 
Rudia tena skimming mkuu, tafuta mtaalam.
 
Wakati wa ku skim, koti ya kwanza una skim na gypsum power iliyochanganywa na maji tuu.... then koti inayofuata ndio una skim na gypsum power iliyochanganywa na rangi nyeupe.
 
Kuna uwezekano waliskim bila ya kitanguliza binder
 
Shida ni fundi wako aliskim na vibaya, skimming ya gypsum unachanganya na rangi ya maji na sio maji. Mafundi wengine huchanganya na maji ndo hapo hujichanganya
Mkuu, fundi alichanganya gypsum powder na rangi ya maji. Sijasema maji na gypsum powder pekee!
 
Kuna uwezekano waliskim bila ya kitanguliza binder.
Mkuu, nilidhani binder inatumika kabla ya kupaka rangi. Yaani baada ya kuskim inafuata binder, then coat ya rangi.
 
Huenda fundi wako aliskim kwa white cement+Rangi.

Badala ya gypsum powder+Maji/rangi.

Hii kadhia iliwahi nipata.
 
Back
Top Bottom