Ufunguzi wa Bonanza la Pemba Tourisport na Utamaduni Wafanyika Kuukuu Kangani

Ufunguzi wa Bonanza la Pemba Tourisport na Utamaduni Wafanyika Kuukuu Kangani

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Katika ufunguzi rasmi wa Bonanza la Pemba Tourisport and Cultural Bonanza uliofanyika Kuukuu Kangani, viongozi mbalimbali walihudhuria tukio hili lenye malengo ya kukuza utalii na urithi wa kipekee wa Pemba. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani, Ndugu Hamad Omar Bakari, ambaye alipokelewa na viongozi waandamizi, akiwemo Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Ndugu Arif Abbas, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale, Dkt. Amina Ameir Issa, pamoja na Prof. Mohamed Hafidh Khalfan, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Afisi ya Raisi, Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji wa Serikali.

Wengine waliohudhuria ni Afisa Mdhamini wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Ndugu Zuhura Mgeni, na Mkurugenzi Mkuu wa ZURA, ambaye alikabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano ya resi za ngalawa. Tukio hilo pia lilihudhuriwa na mwakilishi kutoka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), wadhamini wakuu wa Bonanza hilo.

Ndugu Arif Abbas, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, alieleza kuwa Bonanza hili lilianzishwa mwaka 2018 kwa lengo la kukuza sekta ya utalii na urithi wa kiutamaduni wa Pemba Pamoja na kuifungua Pemba katika Utalii wa Michezo na Utalii wa Utamaduni. Alielezea jinsi limekuwa jukwaa la kuonyesha utajiri wa tamaduni na michezo ya kipekee kama mashindano ya ngalawa, gwaride la punda, Triathlon, na Duathlon. Aidha, alisisitiza kuwa mwaka huu Bonanza limepata mwonekano wa kimataifa kwa kushirikisha mchezaji kutoka Kenya, hatua inayounga mkono dhamira ya Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ya kufungua Pemba kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Pemba, Ndugu Hamad Omar Bakari, aliwapongeza Kamisheni ya Utalii na Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kwa juhudi zao za kuandaa Bonanza hili. Alisisitiza kuwa ni jukwaa muhimu la kulinda urithi wa Pemba na kukuza sekta ya utalii, huku akiwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu. Aliongeza kuwa Bonanza hili ni fursa ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuonyesha uzuri wa Pemba kwa dunia.

Bonanza hilo litaendelea kwa siku nne, likihusisha michezo mbalimbali kama mashindano ya ngalawa, gwaride la punda, Triathlon, na Duathlon, pamoja na maonesho ya kiutamaduni na ziara katika vivutio vya kihistoria vya Pemba. Hii ni sehemu ya juhudi za kukuza utalii endelevu na kuimarisha urithi wa kisiwa hicho.

Katika mashindani hayo ya Ngalawa mshindi wa kwanza alizawadiwa hundi ya million 1.5, mshindi wa pili kapata milioni 1 na mshindi wa tatu kupata 700 na kila mshiriki alipatiwa tanga jipya la ngalawa katika mashindano hayo.
0D8BF59E-B853-4883-822C-1FFBA1FE2791.jpeg
0EC9E917-8FA5-4C73-A399-6F555761C69A.jpeg
3BB92D48-4A5D-43FE-896A-BC0AA474B90F.jpeg
3F392335-8D1F-49FC-AC43-A3B1D3778C8C.jpeg
4B646786-2485-4B62-BFE5-E059A3B6AF42.jpeg
4F4D52DD-8C95-4FF0-8D28-60C24FF0880A.jpeg
5F2A2778-4BFE-4440-BBD5-A9680560FD6E.jpeg
6DC5B619-77D6-45F5-A666-1AC181BA196D.jpeg
9A7D9AAB-80CE-4020-8517-871C8846E995.jpeg
9BA14EF4-3EC3-43BF-A080-F855C592E41B.jpeg
11BC2626-CC18-4D9E-B430-224B0304EDF0.jpeg
17AE1170-F422-4A5A-93BC-55F533AB3FC7.jpeg
28A4C41C-89F5-46D8-AEB4-DC92F97E5CFF.jpeg
49D8C2B2-8FF2-4349-B7A9-5F4AE2F273E1.jpeg
56BAC0CD-2970-4293-9911-53488F884287.jpeg
76C448A0-ADFE-44B4-A828-1F015373B127.jpeg
4197C746-05A0-449B-A0AC-4711556B3029.jpeg
93416FC9-3FCD-457B-8D44-C45032878F7F.jpeg
99221BC6-E814-42E5-B324-98F4BB9620F6.jpeg
981349C5-0FDE-49EF-9B1F-98A49A638EEC.jpeg
23378614-2DC3-48EF-A163-C9073D54B2F1.jpeg
68865281-9555-4951-A51D-F139C21F8817.jpeg
80843926-CD6C-48BE-8D99-C386E9A89D83.jpeg
B013078D-57FE-4B74-82E0-C6A541EB3A01.jpeg
C5E21285-A0B8-44F4-9C15-75B75C076085.jpeg
D2EC5647-F2F3-475F-BB50-9E90E968516A.jpeg
 
Back
Top Bottom