Tetesi: Ufunguzi wa shule za msingi na sekoondari

Tetesi: Ufunguzi wa shule za msingi na sekoondari

hb Mujahideen

Senior Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
152
Reaction score
164
Tumesikia kauli mbalimbali za viongozi na Rais wetu kuhusu UFUNGUZI WA primary and secondary school

Kwa wale mlioko karibu na connection, Serikali ikitangaza tarehe tu, mtuwekee taarifa hapa

Pia nyie wa connection, mnadhani kwanini tareh haitangazwi? Tulisikia wakisema baada ya wiki mbili toka tareh moja ya UFUNGUZI WA Vyuo, lakini wiki mbili zimeisha hakuna kitu.

Mbona mambo kama mpira, miziki, tayari yanafanya kazi?

Nawashauri viongozi wajue kuwa kuna watu tunateseka mbaya sana, japo kweli Korona inaua na lazima iratibiwe vizuri ndo tufungue, lakini wajitahid kubalance kuokoa Hali za baadhi ya Watanzania, tutangaziwe hata tareh tuh, at least tujipe moyo kuwa ni siku fulani,

Elimu ni ufunguo wa maisha

Sent by using alshabaab blog
 
MKUU WEWE NDO UNA UCHUNGU KULIKO HAO VIONGOZI TULIOWAPA DHAMANA?? TULIZA MSHONO WANAJUA WANALOLIFANYA NA WAO WANAJUA ZAIDI KUHUSU HILI JAMBO

Umemisi point ya mtoa mada yeye hajasema anauchungu na elimu bali anauchungu na uchumi wake ambao unaenda endapo zitafunguliwa hizo shule.

Hata mimi nataka zifunguliwe hata kesho nina Mchongo ya pesa huko na juzi nishai kuuliza wanafungua lini maana nacheleweshwa.

Kuna wengi waliohasirika Mamayangu ni mwalimu wa chekechekea kilasiku msemo wake wafungue shule chanzp chake kikubwa cha pesa ni shule kuna mamia ya watu aina hii.
 
Kuwa na subira,Rais alisema anaangalia hawa wa vyuo wanaendelea vipi kisha atafungua,,primary ni watoto wale,umakini unatakiwa,,mtoto anauma sana asee
Kiufupi heri nusu shari kuliko shari kamili
 
wanachuo ni sample one ambao ni testa, just wait and relax
 
Hapa ndo mnapokosea watanzania mnajua MTU akiwa kiongozi basi imani yenu ni kwamba yeye ana akili kuliko watu woote ,yeye anajua kila kitu yaani ni sawa na malaika,kiongozi ni MTU tu kama Wewe huwa anakoseaga kama Wewe,na huwa anahitaji kufundishwa kama Wewe,wanachostahili wao ni heshima tu kwa kuwa ni mamlaka,na ndiyo maana mungu alikupa ubongo na Wewe ili uwaze na kuchambua mambo
 
maamuzi ya busara Ni muhimu mfano darasa moja wanafunzi 60,social distance haitawezEkana labda LA 4 na LA 7
 
Shukran sana ndugu yangu kwa msaada wa majibu mazuri

Yaelekea huyo hajasoma ht kilichoandikwa

Ila ni kweli Kuna umuhim wa kushauri Ana kujadili kwa busara na hekima

Wakati wewe unaogopa kifo kwa watoto wako, Kuna mengi ya kufikiri, mfano, Namna gani korona inawaathiri ndugu zako, hapa ht huyu aliyetukana angekuwa miongoni mwao, cdhani km angeropoka hivi,

Unaye mjibu kwa matusi ni mzazi haswa,anawaza akikurupushwa ataweza kulipa ada ili mtoto aripoti?
Tujadili kwa staha,tumeathirika wengi na huu ugonjwa, nina watoto wanne na wote wanasoma mkoani, kuna swala la usafiri vile vile
 
Umeona Sasa, hivi ukitangaza ht hizo selection ili watu wajipange Kuna ttzo, mie ndugu yangu kafaulu vizuur tuh, lkn hamsha ya kupata fedha kumpeleka school ndo kimbembe, taarifa Ikija mapema ndo tutakavyojipanga mapema, Kinyume chake tukistukizwa itakuwa shida sana
Nchi nzima tunasubiri tamko la mtu mmoja. Selection za form five nazo wanasubiri tamko.
 
Umemisi point ya mtoa mada yeye hajasema anauchungu na elimu bali anauchungu na uchumi wake ambao unaenda endapo zitafunguliwa hizo shule.

Hata mimi nataka zifunguliwe hata kesho nina Mchongo ya pesa huko na juzi nishai kuuliza wanafungua lini maana nacheleweshwa.

Kuna wengi waliohasirika Mamayangu ni mwalimu wa chekechekea kilasiku msemo wake wafungue shule chanzp chake kikubwa cha pesa ni shule kuna mamia ya watu aina hii.
Wenye ambao tunadaiwa ada tunaomba zifunguliwe mwezi wa nane
 
Serikali bado inapata kigugumizi kuzifungua shule kutokana na shule nyingi za msingi na sekondari kuwa na mlundikano mkubwa darasani.Watoto ni wadogo na darasa hubeba wanafunzi zaidi ya mia,sasa itakuaje akiwepo mmoja mwenye maambukizi? Ndiyo linapatikana jibu la tusubiri ugonjwa umeondoka kabisa.
 
Back
Top Bottom