Ufunuo usiosemwa: Je, Lilith ndio nyoka wa Eden? Je, ni mke wa kwanza wa Adam?

Labda Nikuulize mtoa mada,,,lengo lako kutaka mtu mwenye imani yake kamili kufikiri nje ya box ni nini?? Au unamtaka atoke kwenye box lake aingie kwenye box lako??? Eti lilithy!!
Hujalazimishwa nafikiri bado una tatizo la kujua ninini maana ya mijadala
 
Kuna mtu kashathibitisha Mungu yupo hapa? Au longolongo za kila siku tu?
 
Kuna mtu kashathibitisha Mungu yupo hapa? Au longolongo za kila siku tu?
Mimi hapa tena zaidi ya mara 1000.....!na nimekuthibitishia kwa hakika kabisa....!!!
 
Hakika ni thabiti.. Najua kwakuwa nimenena mimi...
Hahaha. Yani ukinena wewe ndiyo inakuwa kweli?

Ukinena wewe ni Bill Gates una mabilioni ya dola za Kimarekani Benki za Uswizi hilo linakiwa kweli?
 
Hahaha. Yani ukinena wewe ndiyo inakuwa kweli?

Ukinena wewe ni Bill Gates una mabilioni ya dola za Kimarekani Benki za Uswizi hilo linakiwa kweli?
Tofautisha hakika na kweli... Na hapa hatumjadili Bill Gates... Unatoka nje ya mada... Mfano wako huo sio valid
 
Inasemekana kuwa kuna malaika ambao walisaidiana na Mungu kumuumba Binadamu na baadae waliamriwa kumtii binadamu huyo na wale waliokataa walionekana wameasi kambi walipelekwa kuishi majini ingawa hawajawahi kupunguziwa nguvu zao, mi kwa fikra zangu hawa ndo hao nyoka maana wanaweza kujigeuza kwa maumbo wanayoyataka..........na haijawahi kusikika walikuwa jinsia gani
 
Tofautisha hakika na kweli... Na hapa hatumjadili Bill Gates... Unatoka nje ya mada... Mfano wako huo sio valid
Umeandika maneno haya

"Hakika ni thabiti.. Najua kwakuwa nimenena mimi..."

Unakataa hilo?
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na si hadithi za watu tu?
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo na si hadithi za watu tu?
Tunaongozwa na vitabu Biblia na Quran inathibitisha uwepo wake.......lkn vilevile kuna wanazuoni wengine wanavitabu vyao ambavyo wao hawaandiki kama Mungu hayupo bali kazi yao kutuachia maswali sisi wasomaji kutafakari baada ya maandiko hayo kuhusu uwepo wa Mungu au lah.........ila hivyo vitabu nilivyovitaja vinathibitisha uwepo wake na si vinginevyo
 
Vitabu hivyo havithibitishi Mungu yupo.

Kwa sababu vinapingana kimoja dhidi ya kingine na kila kimoja kinajipinga chenyewe.

Kujipinga huku kunaonesha ni vitabu vilivyoandikwa na watu na vinaelezea fikra za watu tu.

Si vitabu vya Mungu na wala havioneshi Mungu yupo.

Kitabu kama Biblia ni watu walikaa, tena kisiasa zaidi chuni ya uangalizi wa Mfalme Constantine, katika Baraza la Nicea, wakaamua kitabu kipi kiwekwe katika biblia na kipi kisiwekwe.

Halafu utasema hiki ni kitabu cha Mungu?

Quran ndiyo kabisa unaona ina contradictions za kitoto kabisa. Eti Mungu anaziba watu mioyo, macho na masimio na mioyo wasimjue, kisha anawahukumu watu hao hao kwa kutomjua. Huyo Mungu au Saddam Hussein?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…