Ufuta unawafanya watu wawe na viburi mjini hapa

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
6,816
Reaction score
8,809
Habari za asubuhi mabibi na Mabwana,

Naendelea na uchunguzi sehemu mbali mbali unaweza ukafanya nini kwenye vijiji vyetu vilivyobarikiwa na Mungu wakati sisi vijana woote tunataka tuishi mjini huku tukiendesha mikoko mikali

Ni hivi

Huku bwana ni wakati wa mavuno, aseee watu wanapiga pesaa balaaa, hiki kijiji masemi hayakauki si kubeba mpunga (gunia limepanda hadi 50,000), mahindi nayo yanabebwa si utani, yaani Wasukuma wana pesa chafu sahivi, ikifika jioni ni ngomaa tu mpaka asubuji wanaenda kunywa supu.

Ufuta, ufuta ufuta hapa ndio funga kazi, mazee unafatwa shambani kwako au store kwako wazee wanataka ufuta, kuna mazee mmoja yeye anauza 260k kwa gunia, ila wazee wamefika 255k amegoma na hataki maelezo, mzee anagunia zake 40 za 80kg kila moja.

Jamaa mmoja amejenga ghala la kuhifadhi ufuta asee, hakuna ujinga kama Bachelor degree kwa kweli, ndani ya wiki moja tu pesa anayotengeneza anajua Mungu tu

Ghala halikai na mzigo, ni lulu jamani zao hili.

Nawasilisha tu kwa wakuu humu, mwenye masikio na asikie.
 
Ufuta umeufanya my bro family iachane na maisha ya Dar na kutumia muda wao mwingi kijijini! My sister, ambae maisha yake yote yupo town, analazimika kubaki Dar kwa sababu tu na mwanae wa mwisho bado yupo Form IV vinginevyo angekuwa kesharudi kijijini! Kuna ndugu yangu mmoja, ah Mungu Mkubwa kwa kweli!

Alikuwa na maisha dhalili hadi ilikuwa inatia uchungu! Siku hizi sasa, akipiga simu (zamani ilikuwa lazima nipige mimi), utamsikia, "Kaka njoo utusaidie kuvuna ufuta bhana!" Ananitega huyu binti, yaani Ibilis wa kukupa totoz ana afadhali!

To be honest, kwa vijana wasio na issue za kueleweka town ni kupoteza muda tu kuendelea kung'ang'ania kuwa dar! Ni vile tu maisha yangu yanategemea Internet kwa 100% na kwa bahati mbaya, ingawaje Bush kwetu huduma karibu zote zipo including umeme, lakini Internet imekuwa ni bonge la changamoto! Vinginevyo, lazima ningekuwa na makazi ya muda bush kwetu na kwa sasa nimeshaanza kutafuta kiwanja cha kujenga!!
 
Nadhani mikoa ya asili kwa hili zao ni Kusini, Lindi na Mtwara lakini nadhani siku hizi hadi mikoa mingine wameanza kulima ufuta kama walivyoanza kulima korosho!
🤝🤝🤝🤝
Vip una idea na mkoa wa Mbeya kujihusisha na hili zao?
 
Ufuta ni zao ambalo ambalo ukiamua kulilima halikuachi vibaya , maana utakuwa zaidi ya wauza unga hiyo fedha utakayoipata baada ya mavuno.
Jambo la muhimu upate ardhi sahihi au uiandae ardhi kwaajili ya kilimo hicho vizuri.
Hilo zao lisikie hivyo hivyo Kuna watu wanajinyonga huko ni hatari unaweza lima ekari nane na ukapata ufuta kg 2
 
Kilimo cha Internet

Wewe ndio unaesema kilimo cha internet, Wasukuma huku hawajuu hata smartphone, wanatumia michina ile ya zamani yenye masauti makubwa

Hivi kila kilimo ni kilimo cha internet??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…