Ugaidi ni nini? Jielimishe

Ugaidi ni nini? Jielimishe

Corticopontine

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2019
Posts
666
Reaction score
1,277
Ugaidi kwa maana nyepesi ni kitendo kinacholenga kusababisha hofu kwa raia, serikali au jamii ya kimataifa na vyombo vyake.
Sheria yakudhibiti na kupambana na ugaidi Tanzania imetoa maana pana ya ugaidi katika kifungu cha nne.

Kosa la ugaidi linajumuisha watendaji, wasaidizi na wadhamini wanaosaidia magaidi. Kifungu cha 4 mpaka 10 vinachambua kwa undani mambo yanayopelekea jinai ya ugaidi.

Baadhi ya mambo yanayoweza kuangukia katika ugaidi ni kama ifuatavyo;

I. Kufanya kitendo au shambulio linaloweza kuleta uharibifu mkubwa kwa nchi au taasisi za kimataifa

II. Kwa kutumia nguvu kuilazimisha serikali kufanya Jambo fulani kwa nguvu bila matakwa ya serikali yenyewe

III. Kutumia silaha au milipuko kwa lenga la kutisha umma wa watanzania.

IV. Kuteka viongozi wakuu wa kiserikali kwa shinikizo fulani

V. Kula njama, kusaidia, kuwezesha magaidi kufanya ugaidi.

VII. Kumiliki vifaa au dhana, namba, michoro au ramani ya eneo lililolindwa na kutumia vifaa hivyo kwa lengo la ugaidi etc

Kosa la ugaidi linafanana sana na kosa la uhaini ambapo kwa pamoja makosa haya adhabu yake ni kifo au kifungo cha miaka kadhaa kutokana na namna ya ushiriki katika uhalifu huu.
 
Ugaidi naona ni kuhalalisha ukandamizaji wa serikali kwa wapinzani wake. Ni neno lililowekwa kuhalalisha uonevu kwa mpinzani
Gaidi anakuja na kisu wewe unamuua kwa kombora la ICBM.
 
Ugaidi au kwa Kiingereza terrorism lina utata sana katika tafsiri. Mpaka sasa kuna tafsiri zaidi ya 1000 za ugaidi duniani.

Wakati mwingine tafsiri ya ugaidi inatokana na matakwa ya mtu, kikundi au nchi husika.

Kwa mfano mtu mmoja anaweza akatafsiriwa kuwa ni gaidi kulingana na mtazamo wa watu fulani. Lakini mtu huyo huyo akatafsiriwa na watu wengine kama mkombozi wa jamii ya watu fulani wenye malengo na mtazamo unaofanana.

Wakati wa utawala wa kibaguzi wa Makaburu wa Afrika Kusini, walimtafsiri Nelson Mandela kama gaidi, wakati kwa upande wa Waafrika alikuwa ni mkombozi/mpigania uhuru.
 
Ahsante sana kwa somo
Nalog off
 
Habari wana jamvi ?

Nimekuja kuuliza wajuzi juu ya neno hili. Maana siku mbili hizi limekuwa gumzo sana na kuonekana ya kuwa kuna mtu kama ameonewa kuitwa au kutuhumiwa kwa ugaidi.

Nataka nijue wanao pinga hilo wanazingatia maana ya ugaidi au ? Kwanini huyo aliyetuhumiwa juu ya ugaidi aonekane amedhulumiwa ?

Nini maana ya UGAIDI ?
 
Zamani kidogo gaidi ilikuwa lazima awe mwarabu au muislsm

Wakati uamsho wamebambikiwa kesi ya ugaidi kwa takribani miaka 9 bila kusikilizwa kesi yao, na baadae wakaonekana hawana hatia, so kuna watu humu walifurahia sana na kuwatuhumu kwamba ni magaidi pasipokua na ushaidi wowote kisa tu waisilamu. Ngoja 2one kwa Mbowe na wenzie
 
Ugaidi ni sehemu ya uhalifu, ni sawa na kusema unaomba kueleweshwa tofauti kati ya Tanzania na Mbeya.
 
Ugaidi ni aina ya uhalifu.
Ugaidi ni kitendo cha kuua au kuumiza raia kwa kusudio la kulazimisha mamlaka, kama serikali au mashirika ya umma, kutenda au kutotenda jambo fulani.
 
Habari wana jamvi ?

Nimekuja kuuliza wajuzi juu ya neno hili. Maana siku mbili hizi limekuwa gumzo sana na kuonekana ya kuwa kuna mtu kama ameonewa kuitwa au kutuhumiwa kwa ugaidi.

Nataka nijue wanao pinga hilo wanazingatia maana ya ugaidi au ? Kwanini huyo aliyetuhumiwa juu ya ugaidi aonekane amedhulumiwa ?

Nini maana ya UGAIDI ?
Jadili mada siyo mtu. Mtu atatiwa hatiani kwa hoja ambazo mleta mada kaileta
 
Ugaidi kwa maana nyepesi ni kitendo kinacholenga kusababisha hofu kwa raia, serikali au jamii ya kimataifa na vyombo vyake.
Sheria yakudhibiti na kupambana na ugaidi Tanzania imetoa maana pana ya ugaidi katika kifungu cha nne.

Kosa la ugaidi linajumuisha watendaji, wasaidizi na wadhamini wanaosaidia magaidi. Kifungu cha 4 mpaka 10 vinachambua kwa undani mambo yanayopelekea jinai ya ugaidi.

Baadhi ya mambo yanayoweza kuangukia katika ugaidi ni kama ifuatavyo;

I. Kufanya kitendo au shambulio linaloweza kuleta uharibifu mkubwa kwa nchi au taasisi za kimataifa

II. Kwa kutumia nguvu kuilazimisha serikali kufanya Jambo fulani kwa nguvu bila matakwa ya serikali yenyewe

III. Kutumia silaha au milipuko kwa lenga la kutisha umma wa watanzania.

IV. Kuteka viongozi wakuu wa kiserikali kwa shinikizo fulani

V. Kula njama, kusaidia, kuwezesha magaidi kufanya ugaidi.

VII. Kumiliki vifaa au dhana, namba, michoro au ramani ya eneo lililolindwa na kutumia vifaa hivyo kwa lengo la ugaidi etc

Kosa la ugaidi linafanana sana na kosa la uhaini ambapo kwa pamoja makosa haya adhabu yake ni kifo au kifungo cha miaka kadhaa kutokana na namna ya ushiriki katika uhalifu huu.
Chanzo cha ugaidi ni nini?
 
Back
Top Bottom