Time Bandit
JF-Expert Member
- May 22, 2013
- 615
- 321
UGAIDI NI NINI?Kwa maelezo mafupi,Ugaidi ni kitendo kinachofanywa na watu,taasisi,au kikundi cha watu kwa njia za vurugu,fujo na mauaji ili kutia uoga jamii lengwa na kifikia malengo mahsusi.Kwa ujumla,ugaidi unata nabahishwa na maeneo 3,ambayo ni gaidi,mhanga/wahanga wa ugaidi na jamii husika.Mara nyingi katika ugaidi, lengo sii muhanga(victim) bali msongo wa kisaikolojia(psychological impact) ya tendo lenyewe la kigaidi na mapokeo/mshituko wa jamii lengwa.Ugaidi utaonekana umefanikiwa kama jamii lengwa itaogopa sana kuhusu ilichokiona au itabadili mtazamo katika kile ilichokuwa inakiamini kabla ya kitendo cha ugaidi kutokea.
LENGO LA UGAIDI:Sababu za ugaidi zipo nyingi kulingana na kikundi husika cha ugaidi.Vikundi vya kigaidi vya kidini vina malengo tofauti na vikundi vya kigaidi vya kisiasa.Ugaidi wenye mrengo wa kidini hushambulia nyumba za ibada za dini nyingine,viongozi wa dini au mikutano ya dini zenye imani tofauti nao.Ugaidi wenye mrengo wa kisiasa unaweza ukafanywa kwa kutekeleza shambulio la kudhuru/kuua katika mikutano ya chama fulani au kikundi cha siasa,kushambulia ofisi ya kikundi /chama cha siasa,kuvamia na kushambulia watu wa daraja/kada fulani wanaodhaniwa au kutuhumiwa kuwa ni wanyonyaji,wezi nk.Legho la tendo lolote la kigaidi ni kutia hofu kubwa jamii lengwa,kujulikana ndani au nje ya mipaka ya kijografia(publicity),kuteka na kudai fedha nyingi ili kuendeleza operesheni zao ili kufikia malengo waliojiwekea.
SERIKALI HUWA ZINAFANYA UGAIDI?Jibu la swali hili ni ndio.Mara nyingi,serikali nyingi duniani zimekuwa zikitumia mbinu za kigaidi katika kuzima ushindani wa kisiasa au kuhakikisha sera fulani inafanikiwa.Kuna njia 3 za kigaidi ambazo serikali zinazitumia.
1,Ugaidi wa kidola(Government/state terror):Njia hii wakati mwingine inajulikana kama "terror from above".Katika njia hii,serikali inafanya vitendo vya kigaidi kwa wananchi wake kwa kuwakandamiza kwa kutumia vyombo vya dola kama polisi,jeshi,mahakama au kubadili sheria na kuruhusu utesaji(torture),mauaji, uharibifu wa mali kwa wazi bila kificho kwa visingizio kama "kutuliza ghasia","kulinda maslahi ya taifa" nk.
2,Serikali/dola kudhamini ugaidi(State sponsorship of terrorism):Hili hutokea pale serikal/dola inapo dhamini ugaidi kwa kutoa mafunzo,vifaa na vitu vingine kwa vikundi fulani(non-state organs) ili kufanya vitendo vya kigaidi kwa kikundi kingine ndani ama nje ya nchi.
3,Ushiriki wa dola katika ugaidi(State involvment in terror):Hili hutokea wakati serikali inapotumia government personnel kama polisi,usalama wa taifa au jeshi linapofanya vitendo vya kigaidi kama mauaji,mashambulizi ya kudhuru,utesaji kwa vikundi vya watu,vyama vya siasa,taasisi,wananchi wake au watu binafsi ambao wanaonekana ni tishio kwa usalama au maslahi ya dola husika.Ikumbukwe kwamba katika eneo hili la tatu operesheni hizi hufanywa /huwagizwa na kutekelezwa kwa siri mkubwa na kwa matumizi ya mbinu za kijasusi.