Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Hii bado haijakamilika kuitwa mashine.View attachment 3680936Wakati mijadala mingi kuhusu elimu huzunguka KCSE, grades na ajira, Shule ya Sekondari ya Kebirigo Boys High School huko kaunti ya Nyamira imeonyesha upande mwingine wa elimu, yaani, kutumia maarifa kutatua tatizo la kila siku.
Ripoti zinasema Wanafunzi wa Shule hiyo wameunda mashine inayosaidia kupika na kuchanganya ugali bila kutegemea nguvu ya binadamu katika kuchanganya mchanganyiko huo, jambo linaloweza kupunguza kazi ya wafanyakazi wa jikoni wanaopika chakula kwa idadi kubwa ya wanafunzi.
Video ya mashine hiyo ikiendelea kufanya kazi shuleni imeanza kusambaa mtandaoni, na imeibua swali kubwa zaidi:
Je, huu ndio aina ya ubunifu ambao tunapaswa kuona zaidi katika shule zetu, yaani, wanafunzi kutengeneza teknolojia zinazotatua matatizo wanayoyaona kila siku?
Na kama mashine hii inaweza kufanyiwa maboresho zaidi, ingeweza kutumika pia katika shule nyingine, hospitali na taasisi zinazopika ugali kwa idadi kubwa ya watu?
Teknolojia ya mashine ya kusonga ugali mbona si ngeni?View attachment 3680936Wakati mijadala mingi kuhusu elimu huzunguka KCSE, grades na ajira, Shule ya Sekondari ya Kebirigo Boys High School huko kaunti ya Nyamira imeonyesha upande mwingine wa elimu, yaani, kutumia maarifa kutatua tatizo la kila siku.