Uganda Elections 2021: Wananchi wapiga kura kuchagua Rais na Wabunge leo

Uganda Elections 2021: Wananchi wapiga kura kuchagua Rais na Wabunge leo

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Wananchi Nchini humo wanatarajiwa kupiga kura kuchagua Rais na Wabunge leo Januari 14, 2020

Miongoni mwa Wagombea wa Urais ni Yoweri Museveni, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine), John Katumba, Willy Mayambala, Fred Mwesigye, Henry Tumukunde, Joseph Kabuleta, Nancy Kalembe, Patrick Oboi Amuriat, Mugisha Muntu na Norbert Mao

Museveni ambaye amekuwa madarakani tangu 1986 anawania muhula mwingine. Akizungumza na CNN, amesema atakubali matokeo ya Uchaguzi akisisitiza Uganda sio nyumba yake, hivyo akishindwa atarejea kwake kufanya masuala mengine binafsi kwa furaha

Kwa upande wake, Bobi Wine ambaye ametajwa kuwa Mpinzani mkubwa wa Museveni amesema atakubali matokeo ya Uchaguzi ambao ni Huru na wa Haki

TUME YASEMA ULINZI UMEIMARISHWA KUHAKIKISHA HAKUNA VURUGU

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Nchini humo (EC), Simon Byabakama, amesema uwepo wa Vikosi ya Ulinzi katika Vituo vya Upigaji Kura ni kwa ajili ya kuhakikisha hakuna vurugu

Taifa hilo linafanya Uchaguzi Mkuu leo ambapo kwa mujibu wa takwimu za EC, Wananchi wapatao Milioni 18 wamejiandikisha Kupiga Kura katika Vituo 34,684 Nchini humo ambapo zoezi limeanza saa moja litafungwa rasmi saa 10 jioni

Matokeo ya Uchaguzi huo yanatarajiwa kutangazwa ndani ya saa 48 baada ya zoezi la Upigaji Kura kufungwa

BOBI WINE APIGA KURA

1610626863771.png


NANCY KALEMBE AKIPIGA KURA

kalembe.jpg
 
Utabiri wangu

Kura halali

Bobi wine 72%, Museveni 18%, others + zilizoharibika 10%

Kura zitazotangazwa (uchakachuzi)

Museveni 92%, Bobu wine 5%, others + zilizoharibika 3%
 
Utabiri wangu

Kura halali

Bobi wine 72%, Museveni 18%, others + zilizoharibika 10%

Kura zitazotangazwa (uchakachuzi)

Museveni 92%, Bobu wine 5%, others + zilizoharibika 3%
Mweh!!

Basi basi demokrasia tuwaachie wenyewe mabeberu..tumeshazoea vya kunyonga Sie Afrika[emoji41]
 
Hivi tume ya uchaguzi ya Uganda viongozi wake wanatokana na Rais au?

Maana kama wananguvu kama wale wa Kenya basi mu7 mapema anapigwa nokout!
 
Back
Top Bottom