Uganda: Jela miaka 13 kwa kumnajisi na kumpa mimba mwanae wa miaka 12

Uganda: Jela miaka 13 kwa kumnajisi na kumpa mimba mwanae wa miaka 12

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Charles Minaani(33), mkazi wa Luweero, Uganda atatumikia kifungo cha miaka 13 jela, hii ni baada ya kuongea na jaji kuhusu mashtaka yake ya kunajisi na kumpa mimba mwanae wa miaka 12, kosa ambalo alitenda mwaka 2016

Mchakato wa kuongea na jaji kuhusu mashtaka ni hiyari. Kama ilivyo Hiyari Tanzania (Kwa sasa) kukiri makosa ya uhujumu uchumi kwa DPP, ikiwa sheria imekuona

"Nimekubali kwa hiari ya kifungo cha miaka 13 kwa mashtaka ya hatia ya unajisi" ilisomeka taarifa hiyo katika makubaliano kati yake na jaji iliyotiwa saini na mtuhumiwa wakati wa Kikao cha Mahakama Kuu mbele ya Jaji Okwang huko Luweero tarehe 13 Januari, 2020

Ndugu wa karibu ambaye hakutaka majina yake kutajwa alidai kuwa wamemsamehe baba huyo "Hatukufikiria kuwa tukio kama hili lingeweza kutokea katika familia yetu. Tulimsamehe Minaani lakini sheria tumeacha sheria ifuate mkondo wake "alisema

Mshtakiwa amekubali kosa kwa kutarajia kupewa adhabu ndogo. Aliepuka kusumbua mahakama na kuipa mchakato mrefu Mahakama ambayo ingeweza kumfanya apewe adhabu kali

Chanzo: Daily Monitor
 
Back
Top Bottom