Uganda kufua umeme wa nuklia

Uganda kufua umeme wa nuklia

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,227
Reaction score
6,670
Ili kufikia lengo la Dira ya Maendeleo ya 2040, Uganda, kutahitajika nchi iwe uwezo wa umeme wa 41, 738 MW na kwa matumizi ya watu 3,668 kWh. Hata hivyo, uzalishaji uliopo kwa sasa (hydro, biomass, nk) hauwezi kwa mahitaji ya Dira hiyo. Kwa hiyo, ili kupunguza upungufu wa nishati, mkazo utahusu maendeleo ya nguvu za nyuklia ili kuzalisha 2000MW.

Swali, iwapo huo mpango utawezekana, Mradi wa Bwawa la Nyerere utakuwa na nafasi gani? Tunaambiwa tuna madini ya uranium Tanzania, naamini ni wakati mwafaka wa kufikiria uzalishaji wa umeme wa nuklia kuepuka changamoto za umeme wa maji unaotegemea kiwango cha mvua.
 
Uzalishaji wa nishati kwenye vyanzo vya hatari kama hivyo unahitaji usimamizi imara wa maadili

Kwa nchi za afrika zilizo na nyani walio kwenye hatua za mabadiliko ya kuwa watu, italeta maafa sana kuliko faida_sishauri
 
Ku handle uchafu wa nuclear ni ghali kuliko nafuu ya kuuzalisha.
Mungu katupa. maji jua,upepo,wnyama, miti, gesi, mafuta kwa nini tuhangaike na nuclear.
Mataifa makubws yanampango wa kuachana na nuclear sie ndio tunataka tuanzishe hio miradi.
Tuna vyanzo vingi sana vya umeme.
Tuna mito mikubwa kila kona, geothernal nk hivyi vyanzo havina gharama kubwa.
Tusiharibu mazingira kisa nishati.
 
Kabla hamjajenga izo power plant za nuclear, nendeni mkacheki documentary ya Chenobly accident
 
Nyukilia ni nzuri na hatari hasa nchi zisizo stable aisee!! Ikatokea waasi wakavurumisha kombora kwenye kinu chenu cjui itakuaje
 
Back
Top Bottom