ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
KWA miaka mingi, wavumbuzi walitafuta chanzo cha Mto Nile, ambao hupinda-pinda sehemu kubwa ya Afrika na kumimina maji yake katika Bahari ya Mediterania.
Hatimaye, wavumbuzi fulani waliangazia Ziwa Victoria na milima iliyo karibu nalo kuwa chanzo kikuu cha maji ya Mto Nile Uganda ina takribani wakazi million 45 na makabila zaidi ya 30 ina vijana wengi sana.
Uganda ni nchi yenye kupendeza iliyo kwenye ikweta barani Afrika. Nchi hiyo ina hali nzuri ya anga. Mito na maziwa mengi hupata maji safi kutoka kwenye milima yenye barafu ya Ruwenzori, inayoitwa Milima ya Mwezi. Kwa sababu ya udongo wake wenye rutuba na mvua nyingi nchi hiyo huzalisha kahawa, majani chai, na pamba.
Watu wa uganda wanakula sana karanga kwenye vyakula vyao ndo maana wana afya nzuri. Ndizi huzalishwa kwa wingi, nazo hutumiwa kutayarisha chakula kinaitwa matooke, mojawapo ya vyakula vikuu vya Uganda ni Mihogo, mahindi, ulezi, na uwele huliwa pia.
Inasemekana uganda ina karibu 80 % ya mamalia wote Wanyama kama vile simba, ndovu, kiboko, mamba, chui, twiga, paa, na pia sokwe walio katika hatari ya kutoweka, hali kadhalika tumbili wa aina mbalimbali hupatikana nchini humo.
Kuna ndege wengi maridadi wenye sauti tamu. Kuna mengi ya kuvutia nchini Uganda hivi kwamba nchi hiyo inaitwa “lulu ya Afrika. Ni moja wapo kati ya nchi nzuri sana kuishi Afrika.
Hata hivyo, inasikitisha kwamba katika miaka ya 1970 na 1980, misukosuko ya kisiasa na vifo vya maelfu ya watu viliathiri sana “lulu” hiyo pamoja na watu wake. Isitoshe, ugonjwa wa UKIMWI umezidisha matatizo nchini Uganda.