Uganda: Mbunge wa Arua Ibrahim Abiringa NRM auawa kwa kupigwa risasi

Uganda: Mbunge wa Arua Ibrahim Abiringa NRM auawa kwa kupigwa risasi

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mbunge wa Manispaa Arua, nchini Uganda Ibrahim Abiringa, mmoja wa wale ambao waliokuwa mstari wa mbele kushinikiza mabadiliko ya Katiba ya Uganda ameuawa kwa kupigwa risasi jana usiku.

Polisi imesema mwanasiasa huyo wa chama tawala cha National Resistence Movement (NRM),na mlinzi wake waliuawa karibu na makazi yake kaskazini mwa mji mkuu wa Kampala na watu wasiofahamika.

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa amesikitishwa na mauaji hayo na kuagiza maafisa wa usalama kuwasaka waliomuua mbunge huyo.

Chanzo: VOA Swahili
FB_IMG_1528481110753.jpg
IMG_20180608_212248_637.jpg
 
Mashetani huwa yanafanana Duniani kote,Tanzania tunalo shetani kwa jina la Y*h*na kumbe na Uganda wanaloshetani lao
R.I.P Member of Parliament!
 
Hatari sana hii kwa siasa hizi za Afrika
 
Ila waganda washamba jamani gari ya njano na suti ya njano,
Rip sir
...........Na hawa wa hivi unawakuta kichwani weupeee!!!wao kupiga makofi tu hata kwa hoja mfu.

1+1=11 ndo jibu watakalokwambia.
 
Mambo ya kawaida kwenye Siasa Dunia nzima Sio Africa peke Yao

Kina Kenedy, Malkom X Na Martin Luther walipigwa Chuma

Kina Ghandi kule India
Kina Bhenazir Butoh kule Pakistan
 
je wangapi wenu mnajua kuwa Mp Abiliga ni mwanajeshi mstaafu wa cheo cha Major???
yeye na Mh. Raisini damy damu. tumepoteza mmoja wa wapiganiji wa nguvu.na nyie waTz mko hapa na fujo zenu bila hata kuwa na uelewa wa kutisha
amepigwa risasi akiwa ndani ya gari. sijawhi ona mtu napigwa risasi kisha tena na gari nalo linapigwa risasi
 
Mambo ya kawaida kwenye Siasa Dunia nzima Sio Africa peke Yao

Kina Kenedy, Malkom X Na Martin Luther walipigwa Chuma

Kina Ghandi kule India
Kina Bhenazir Butoh kule Pakistan
Kwanini iwe kawaida mauaji? Hapana Afrika siasa imezidi kuwa mbaya aisee
 
Aliyekufa ndiyo mwenye makosa, that’s all!
Life is totally wonderful!
 
Back
Top Bottom