UGANDA: Mkuu wa Jeshi la Polisi awaamuru wananchi kuwapiga mawe Polisi

UGANDA: Mkuu wa Jeshi la Polisi awaamuru wananchi kuwapiga mawe Polisi

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
ug.jpg

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Okoth Ochola amewaamuru wananchi kuwakamata au kuwapiga mawe maafisa wa polisi wasiojitambulisha wanapokwenda kuwakamata watuhumiwa hata kama wamebeba bunduki.

Amefikia uamuzi huo mara baada ya vitendo vya utekaji kushamiri nchini humo hivyo jeshi la polisi kuhusishwa moja kwa moja na masuala ya utekaji.

“Afisa wa Polisi anapewa mafunzo jinsi ya kumkamata mtuhumiwa, anastahili kujitambulisha na kumweleza mtuhumiwa sababu za kumkamta kabla ya kumkata. Kama hafanyi hivyo, raia wawakamate au wawapige mawe hao polisi,” amesema Kamanda Okoth Ochola

Aidha, raia nchini Uganda wamesema kuwa wanashindwa kuwatambua wanaowateka nyara jamaa zao, kwani wana tabia sawa na za maafisa wa polisi, wanao wakamata raia bila ya kujitambulisha, wala kuvalia sare za kikazi.

Karibu kila siku, matukio ya mtu kutekwa nyara, hasa wasichana na akina mama yamekuwa yakiripotiwa nchini Uganda.

Hata hivyo, Polisi nchini humo limewakamata wapiganaji wa Mai mai 26 kutoka Jamhuri ya Kidemokraksia ya Congo (DRC), baada kikundi cha wapiganaji hao kuwateka nyara wavuvi 6 raia wa Uganda katika ziwa Edward, magharibi mwa nchi hiyo.

Chanzo: Dar24
 



MKUU jeshi la polisi nchini Uganda amewaamrisha wananchi kuwakamata au kuwapiga mawe maofisa wa polisi wasiojitambulisha wanapokwenda kuwakamata washukiwa hata kama wamebeba bunduki.

Raia wa Uganda wamedai kwamba wanashindwa kuwatambua wanaowateka jamaa zao kwani wana tabia sawa na za maofisa wa polisi, wanaowakamata raia bila ya kujitambulisha, wala kuvaa sare za kikazi.

“Polisi anastahili kujitambulisha na kumweleza mshukiwa sababu za kumkamta kabla ya kumkata. Kama hafanyi hivyo, raia wawakamate au wawapige mawe,” amesema Kamanda Okoth Ochola.

Karibu kila siku, matukio ya mtu kutekwa, hasa wasichana na akina mama yamekuwa yakiripotiwa nchini Uganda. Utekaji pia umesambaa na kuwalenga watoto wadogo, chini ya miaka mitano licha ya maofisa wa polisi na jeshi kuingilia kati kukabiliana na watekaji. Mkuu wa polisi anahusisha utekaji nyara huo na makundi ya kigaidi.

“Baadhi ya washukiwa ambao tumewakamata wana uhusiano na makundi ya kigaidi lakini sitayataja kwa wakati huu kwa sababu bado tunafanya uchunguzi. Tutakapokamilisha uchunguzi wetu, tutawaeleza,” alisema Ochola.

Visa vya utekaji watu vimekuwa vikiendelea nchini Uganda kwa mda wa takriban mwaka mmoja sasa. Watekaji hudai mamilioni ya pesa kama ili kuwaachia mateka, na hata baada ya kulipwa pesa wanazotaka, huwaua watu waliowateka.

Wakati huohuo, polisi nchini Uganda wamewakamata wapiganaji wa Maimai 26 kutoka Jamhuri ya Kidemokraksia ya Congo (DRC), baada kikundi cha wapiganaji hao kuwateka wavuvi sita raia wa Uganda katika Ziwa Edwward, magharibi mwa Uganda. Wapiganaji wa Mai Mai wanataka kupatiwa masanduku kadhaa ya risasi ili kuwachia mateka.

“Pamoja na hayo na sisi, tumewakamata wapiganaji wao 26. Kwa hivyo tumewapa masharti kwamba waachilie raia wetu kwanza,” amesema Ochola.
 
Nilijua bongo asee nikamdunde mkuda flani hivi
 
Hiyo ndoshida ya kutumia raia katika intelejisia kuwafanya (crime priventers) badae kuwatupa bila kuwapa ajira za kudumu.....lazma watafute pesa ya haraka kwa njia zote
 
Vita sasa make polisi ana siraha raia hana na unaambiwa umkamate mwenye siraha, akikushot je?
 
Back
Top Bottom