SI KWELI Uganda: Mwendesha bodaboda aliyekuwa amepakia ndizi na kukatiza mbele ya kundi la Simba auawa na kuliwa na simba hao

SI KWELI Uganda: Mwendesha bodaboda aliyekuwa amepakia ndizi na kukatiza mbele ya kundi la Simba auawa na kuliwa na simba hao

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Wiki mbili zilizopita kwenye mitandao mbalimbali ilionekana mwendesha bodaboda asiye na woga akiwaacha wengi katika mshangao baada ya kupita kwa utulivu katikati ya kundi simba wenye njaa wanaokula mnyama waliyemuua.


Inasemekana baada ya kuwapita Simba, pikipiki yake ilipata hitilafu ambapo alishindwa kuendelea na safari ndipo Simba waliweza kumshambulia na kujipatia kitoweo.

IMG_8048.jpeg


Picha ya mwisho iliyobandikwa ilionyesha simba wakiwa wamekaa pembeni ya pikipiki hiyo iliyokuwa imebeba na ndizi, lakini mtu huyo hakupatikana, jambo ambalo liliwashangaza wengi na kuamini kuwa ameliwa na simba hao.

VIDEO: Simba wakizunguka pikipiki huku dereva akiwa haonekani.


Katika Mtandao wa Twitter, mtumiaji mmoja maarufu kama Mwaisa MtuMbad alipakia video ikiambatana na maneno 'Scary dont open 18 jamaa kaliwa ayse'
 
Tunachokijua
Julai 2, 2023, video moja ikimuonesha mwendesha pikipiki akikatiza kwenye kundi la Simba ilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Mmojawapo ya watu walioweka video hiyo kwenye mtandao wa Twitter ni Depedro Deniss Nkya. Iliambatana na maneno haya;

"Wazungu wanazama baharini kuangalia mabaki ya Titanic. Halafu kuna mwamba hapo Uganda anapita shwaaaaa katikati ya Simba na bodaboda"

Baadhi ya Watumiaji wengine waliochapisha video hii iliyoonekana kuvutia watumiaji wengi wa mtandao ni Clouds Media.

Kuibuka kwa madai ya kifo cha Mwendesha Pikipiki
Mwendesha pikipiki ambaye alipigwa picha akiwa amebeba mikungu ya ndizi au kwa lugha maarufu nchini Uganda ya Matooke kwenye pikipiki alidaiwa kuuawa na kuliwa na simba katika Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii ikiwemo mmoja anayefahimika kwa jina la Mwaisa MtuMbad, Julai 10, 2023 aliweka video inayoonesha simba wakizunguka pikipiki yenye mikungu ya ndizi kuashiria kuwa mhusika alikuwa ameliwa na simba hao.

Aidha, Julai 12, 2023, mtumiaji mwingine wa mtandao huohuo anayefahamika kwa jina la Ankodidi aligusia pia kifo cha bwana huyo. Alisema;

"Mnaikumbuka hii video ya Boda Boda akikatiza katikati ya Simba Basi bwana mambo yaliisha hivi...Check Video Kwenye comments"

Ukweli wa uvumi huu
Uvumi huu umekanushwa na Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda (UWA) ambayo kwa mujibu wa Taarifa kwa Vyombo vya Habari iliyotolewa Julai 14, 2023 na Meneja wa Mawasiliano katika Mamlaka ya hiyo Bashir Hangi, mtu huyo kwenye kipande cha video hakuliwa na simba kama inavyodaiwa.


IMG-20230714-WA0455.jpg

Tamko la Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda (UWA) kukanusha uvumi huo

Hangi alieleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai 10, 2023, wakati bwana mmoja aliyekuwa amebeba Ndizi (Matooke) kwenye pikipiki kutoka Wilaya ya Rubirizi alipothubutu kuendelea hadi eneo la Kasenyi lililopo Ziwa Edward Wilayani Kasese kupitia Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth.

Hangi alieleza kuwa bwana huyo ambaye bado hajatambuliwa alishauriwa na Viongozi wa Mamlaka ya Wanyamapori Uganda kutotumia njia hiyo kwa kuwa kundi la simba sita wameonekana katika eneo hilo na hivyo usalama wake hauwezi kuhakikishwa.

Hata hivyo, mtu huyo alisisitiza na kutumia njia hiyo na kujaribu kuyafuata magari ya watalii hao akitarajia angejificha nyuma ya magari hayo na kupita bila kuonekana na simba hao au simba wakimuona angeenda mbali kwa simba kumfukuza yeye.

Magari ya Watalii yalisimama ghafla huku watalii hao wakianza kupiga picha ambapo simba hao walikuwa wamefika barabarani, alipojaribu kuwaficha simba hao nao walikuwa wakijihifadhi chini ya magari hayo.

Sehemu ya taarifa hiyo inasema;

Kwa bahati mbaya alipofika kwenye magari ya watalii yalikuwa yameegeshwa na watalii walikuwa wakipiga picha za simba waliokuja barabarani. Alipojaribu kujificha nyuma ya magari hayo, simba hao pia walikuwa wakijificha kuzunguka magari na wengine chini ya magari .”

Katika hatua hii, alikuwa ameingia kwenye eneo hatari la simba, wakamtisha na akaruka kwenye gari moja la watalii. Kwa hiyo, mwanamume huyo hakuliwa na simba kama inavyodaiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.”

Picha ya mwisho iliyobandikwa ilionyesha simba wakiwa wamekaa pembeni ya pikipiki iliyokuwa imebeba na matooke, lakini mtu huyo hakupatikana, jambo ambalo liliwashangaza wengi na kuamini kuwa ameliwa na simba hao.

Mamlaka zatoa onyo
Mamlaka ya Wanyamapori ya Uganda (UWA)
ilitoa onyo kwa wananchi kwa ujumla, na kubainisha kuwa wakati wanafanya kazi ya kuhakikisha usalama wa wageni wote wanaotembelea hifadhi za taifa, juhudi zao haziwezi kuwahakikishia usalama watu wanaoingia ndani ya hifadhi bila kibali kutoka kwa uongozi wa hifadhi.

Kutokana na hali hiyo, waliahidi kuendelea kuwaonya wananchi kuhusu hatari zinazohusishwa na kuingia kinyume cha sheria katika hifadhi za Taifa.
Back
Top Bottom