UGANDA: Rais Museveni aidhinisha sheria kuondoa kikomo cha umri wa rais

UGANDA: Rais Museveni aidhinisha sheria kuondoa kikomo cha umri wa rais

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2012
Posts
2,046
Reaction score
3,971
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha mswada unaoondoa kikomo cha umri kwa wagombea urais nchini humo, hatua inayompa nafasi ya kuwania tena urais mwaka 2021.

Mswada huo pia unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.

Kwa kuwa sheria hiyo itaanza kutekelezwa sasa, Bw Museveni anaweza akaongoza taifa hilo hadi 2031.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, katibu wa rais Bi Linda Nabusayi amesema Bw Museveni alitia saini mswada huo kuwa sheria Desemba 27 na kisha akatuma waraka tarehe 29 Desemba.

Sheria ya awali ilikuwa inamzuia mgombea kuwania urais baada ya kutimiza umri wa miaka 75.

Bw Museveni kwa sasa ana miaka 73.

Hatua ya rais huyo kuidhinisha mswada huo imetoa wakati ambao amekuwa akihimizwa na viongozi wa kidini na wanaharakati wa kisiasa kutouidhinisha.

Bunge liliidhinishwa mswada huo mnamo tarehe 10 Desemba kwa zaidi ya theluthi mbili ya wabunge waliohudhuria kikao, wabunge 317 wakiunga mkono na 97 wakapinga.

Chanzo; BBC
 
Bw Museveni kwa sasa ana miaka 73.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinisha mswada unaoondoa kikomo cha umri kwa wagombea urais nchini humo, hatua inayompa nafasi ya kuwania tena urais mwaka 2021.

Mswada huo pia unarejesha takwa la rais kuongoza kwa mihula miwili pekee ya miaka mitano.

Kwa kuwa sheria hiyo itaanza kutekelezwa sasa, Bw Museveni anaweza akaongoza taifa hilo hadi 2031.
 
7259c0e5ef3bab7cb1c30dc0283b0ce6.jpg
 
Atakuwa na miaka 85 hivi hiyo 2031
Africa shenzi sisi
 
Na sio miaka 5 BALI NI MIAKA SABA SASA
 
Africa my Mama Land , very sorry but no way. God we need your Help.
 
Ndege wafananao. Hebu ngoja tuangalie na upande wa pili tuone. Aiseee.
 
MU7+KAGAME+NKURUNZINZA na tz nahisi tunaelekea huku! kuwa na raisi wa maisha!
 
Hiyo ndio maana kamili ya madicteta wa afrika hawatoki 1museni 2.kagame 3.mkulunzinza 4.kabila. sasa kansa hii inazidi kuenea hata huku itafika muda utatuambia
 
Back
Top Bottom