UGANDA: Rais Yoweri Museveni awafuta kazi IGP, Waziri wa usalama na kuteuwa wapya

UGANDA: Rais Yoweri Museveni awafuta kazi IGP, Waziri wa usalama na kuteuwa wapya

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Rais Yoweri Museveni Jumapili aliwafuta kazi mkuu wa polisi Jenerali Kale Kayihura pamoja na Waziri wa Usalama wa Nchi Jenerali Henry Tumukunde.

Katika taarifa kwa njia ya Twitter Rais alisema anamteua Elly Tumwine kuwa Waziri wa Usalama na Okoth Ochola kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP).

“Kwa mamlaka niliyopewa na Katiba, nimemteua Jenerali Elly Tumwine kuwa Waziri wa Usalama. Nimemteua Okoth Ochola kuwa Inspekta Jenerali wa Polisi na atasaidiwa na Brigedia Sabiiti Muzeei,” ilisema taarifa ya Rais.

Jenerali Kayihura, kuna wakati alifikiriwa kuwa ofisa wa jeshi mwenye nguvu zaidi nchini lakini hivi karibuni alipishana na Museveni ambaye ametawala Uganda tangu alipotwaa madaraka ya nchi akitokea msituni mwaka 1986.

Kayihura aliteuliwa kuwa IGP mwaka 2005, mwaka ambao kura ya maoni ilipitishwa kwa mafanikio kurejesha mfumo wa demokrasia ya vyama vingi baada ya kupigwa marufuku kwa miaka 20.

Utawala wake ulionekana ukitumia zaidi mbinu za vitengo vya kijeshi na vilevile ilienea dhana kwamba siasa iliingia katika jeshi hilo la polisi.

Tangu Machi 2017 yalipofanyika mauaji ya Felix Kaweesi, polisi mwandamizi ambaye alikuwa anatazamwa kama mrithi wake mwenye uwezo, Kayihura amekuwa akikabiliwa na presha kubwa kwa kushindwa kwake kuzuia ongezeko la ukosefu wa usalama.

Wanawake wapatao 23 wameuawa katika mauaji ambayo ufumbuzi wake haujapatikana na yasiyojitenga karibu na mji mkuu, kumekuwa na jeraha la vifo vya wananchi wa kigeni na juma jana mwanamke kutoka familia yenye ushawishi aliuawa baada ya kufungwa kwa wiki tatu kwa watoa nyara wanadai fidia kubwa.

Rais, ambaye mara kwa mara amekuwa akisisitiza kuwekwa kamera za CCTV katika maeneo ya mijini kama njia ya kupambana na uhalifu, hivi karibuni aliongeza kuwa ni wakati wa kutumia utambulisho wa viganja na vipimo vya DNA ili kusaidia kupambana na uhalifu.

Chanzo: Mwananchi
 
[HASHTAG]#shenzytyp[/HASHTAG] hahaha nlijua mawaziri mizigo hapa wameondoshwa
 
Nilidhani kalala mbele na waziri wa tembo na wazungu
 
Ngumu kwa hapa kwetu hii kutokea kwa sasa
 
Haya magazeti inabidi vichwa vya habari wawe wanaviangalia mara mbili mbili maana vinakera balaa.

Kuna siki (kama mwaka 2005) nimesoma kichwa cha habari kinasema "raisi apata ajari na warembo" basi nikatoka mbio naenda kimwambia baba kiwa raisi mkapa kafariki kwa ajali..baba akanipa hela nikanunie gazeti nafika nyumbani nakuta kumbe ni rais wa kampuni ya mitindo sjui ya nchi gani..

Kuanzia siki hio nachukia magazeti yote kasoro la michezo tu
 
Aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi bwana Kale Kayihura kapigwa chini huko Uganda na mkuu wake Raisi Museveni. Ikumbukwe kuwa bwana huyu kwa muda mrefu amekuwa akitembeza mkono wa chuma wa ajabu kweli kweli kwa akina Kiiza Besigya. Huyu bwana wa mkono ule bila shaka hakutegemea kuwa angekuja kuondolewa kwenye cheo hiki cha u IGP ambacho katika hali ya kushangaza wengi, wengine wameonyesha hadharani kukitamani mno, achilia mbali kufukuzwa kazi kama ilivyomtokea ghafla na unceremoniously bwana huyu.

Huyu bwana alikuwa katika nafasi ya kuweka mizania ya mambo mengi tu kuwa sawa na badala yake hakufanya hivyo. Watu kama hawa kesho ukiwasikia kuwa ati sasa ndiyo wako na kina Kiiza Besigye kudai haki huwa si ajabu hata kidogo. Hata hivyo uswahilini wanasema, huwa wanakuja kukumbuka shuka wakati kumeshakucha tayari. Wandugu wenye dhamana jifunzeni kutenda haki zaidi kwani hiyo pekee ndiyo hudumu.

Yu wapi leo the real right hand man wa kukandamiza haki za wenye mawazo tofauti Uganda Generali Kale Kayihura?

https://www.independent.co.ug/breaking-museveni-fires-kayihura-tumukunde/
http://www.monitor.co.ug/News/Natio...t-Kayihura/688334-4116134-11qcjjbz/index.html

Watakuja watakwenda nchi zitabaki.

Wekeni uzalendo mbele kuliko *mere* mikate yenu ya siku kwa siku. Historia itakuwapo kuwa hukumu.
 
Kila kitu na wakti wake.Hata Sizonje atapita.
 
Inawezekana ni kama Bashite hapa. Kapewe mamlaka ya kufanya lolote atakalo, ma hakuna chombo wala mtu binafsi wa kuhoji.

Siku baba J, atakapoona anavunjiwa heshima kwa kulinda jina la bashie, ataamua kujiongoa na ndiyo chanzo ya Umgabe.

Kumlea mtu katika maovu, ana kuzoea na kukona mko at pa. Siku ukimwonya anakuona ni adui na hivyo anakuwahi.
 
Back
Top Bottom