UGANDA: Serikali yazipiga marufuku Radio na Tv kutopiga nyimbo au kufanya interview na msanii Bobi Wine

UGANDA: Serikali yazipiga marufuku Radio na Tv kutopiga nyimbo au kufanya interview na msanii Bobi Wine

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
1,817
Reaction score
4,061
Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imepiga marufuku kwa vyombo vya habari nchini humo kufanya 'interview' na mwanamuziki Bobi Wine, baada ya kuonekana kinara kwenye suala la kupinga ukomo wa urais nchini humo.

BobiWine-704x481.jpg

Bobi Wine

Taarifa hiyo imetolewa na mwenyewe Bobi Wine ambaye pia ni mbunge wa upinzani nchini humo kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa amepigiwa simu na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na kuthibitisha suala hilo, kuwa wamepigwa marufuku kufanya naye mahojiano yoyote.

"Hii asubuhi nilitakiwa kufanya mahojiano na Capital FM, baadaye nikataarifiwa kuwa wamepewa agizo na UCC na kupigiwa simu na watu wa usalama kwamba wasiwe na mimi, nikapigiwa simu na vituo vingine vya redio na runinga na kunithibitishia wamepewa agizo hilo hilo na kwa vitisho, na iwapo watakuwa na mimi watakuwa katika hatari ya kufungiwa", ameandika Bobi Wine.

Bobi Wine ameendelea kuandika akisema kwamba.. "Iwapo unaangalia dalili za kuanguka kwa serikali usiendelee tena, huu ni upumbavu na haukubaliki, serikali inadhani inaweza kutuzuia kufikia watu wetu, wanafanya vitu ambavyo havina tofauti na vile wanavyohubiri kuvipinga",

Bobi WIne amekuwa miongoni mwa viongozi maarufu ambao wanapinga vikali suala la kutaka kupitishwa kwa katiba ambayo itongeza muda wa ukomo wa urais, kitendo ambacho kitamruhusu Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo, kugombea tena awamu ijayo.

upload_2017-10-1_21-45-21.jpeg
 
Halafu hawa hawa viongozi wetu wanatuaminisha umaskini wetu Africa umeletwa na wazungu..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hata huku itafika tu Diamond ale Maisha Kwa kampeni muruwa. Mamlaka ni matamu Sana... kutembea kwenye zulia jekundu,vimulimuli barabarani na kulambwa miguu na wanaojipendekeza hakuachi mtu salama
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapa mwanamuziki akimpinga rais tu anatekwa (ref sakata la Roma)
Ndiyo tujue despite the odds. Uganda iko juu kidemokrasia kuliko Tanzania kwani hata matokeo ya rais inaruhusiwa kuyapinga mahakamani.
 
Sera za marais wa Afrika kujimilikisha madaraka ni aibu kubwa

Mugabe

Kagame

Nkrunziza

Nk

Sasa Kaguta zaid ya miaka 30 bado analazimisha kubakia ikulu hovyo kabisa
Mkuu naona umeogopa kumtaja sizonje
 
Halafu hawa hawa viongozi wetu wanatuaminisha umaskini wetu Africa umeletwa na wazungu..
Kwani hao waafrika wanaobadilisha viongozi wao kila baada ya miaka mitano/minne wana maendeleo gani? Mbona nchi hizo za wang'ang'ania madaraka bado zinatupiga ile mbaya sisi Wabongo kwenye maendeleo?
 
KENYA [emoji117] Trying to vote to have a President

UGANDA [emoji117] Tired of their President

SOUTH AFRICA [emoji117] Voting to remove a President

RWANDA [emoji117] Pretended to have voted for President

NIGERIANS [emoji117] Don't even know the whereabouts of their President

ZIMBABWEANS [emoji117] Are waiting for their President to kick the bucket

LIBERIA [emoji117] Still not sure who is the President

SOMALIA [emoji117] The President lives and run the country from Kenya

BURUNDI [emoji117] President cannot leave the country, scared of someone else taking over

DR Congo [emoji117] Government says they don’t have money to conduct election of new President

WELCOME TO AFRICA [emoji81][emoji81][emoji81][emoji81]
 
Nigeria and Burundi top the list but,
DR Congo
emoji117.png
Government says they don’t have money to conduct election of new President..

I guess DRC comes before.

Gotta Love the motherland! 😀😀😀
 
Back
Top Bottom