The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Wizara ya Elimu nchini Uganda imewasilisha Muswada wa Taifa wa Walimu wa 2024 Bungeni, ambapo Waziri wa Nchi wa Elimu ya Juu, John Chrysostom Muyingo, ameeleza kuwa muswada huo unalenga kuboresha viwango vya ufundishaji nchini humo.
Kulingana na Wizara ya Elimu na Michezo, sheria hiyo inayopendekezwa itashughulikia changamoto zinazowakabili walimu nchini Uganda.
Miongoni mwa mambo mengine, muswada huo unalenga kuanzisha utoaji wa leseni za mafunzo kwa walimu wote. Leseni hizo zinazoweza kuhuishwa zitaisha baada ya miaka minne. Pia inahitaji walimu wa ngazi zote kuwa na shahada ya kwanza kama sifa ya chini kabisa.