Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Vyombo vya usalama nchini Uganda vimethibitisha kuwakamata zaidi ya wafuasi 40 wa chama cha upinzani NUP kwa kushiriki maandamano ya amani yaliyotangazwa na kiongozi wao Robert Kyagulanyi siku ya Jumanne.
Siku ya Jumanne, kiongozi wa chama cha NUP, Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine aliwahimiza wafuasi wake kushiriki maandamano ya amani kupinga matokeo ya urais na pia dhidi ya kamatakamata ambayo Rais Yoweri Museveni amekariri inalenga kukabiliana na majaribio ya kusababisha ghasia.
Bobi Wine aliwahutubia baadhi ya wafuasi wake kwenye makao makuu ya chama hicho ambako alionyesha majalada kadhaa akisema ni fomu za matokeo ya uchaguzi alizokuwa amewasilisha mahakamani kama ushahidi.
Vyombo vya usalama vimeitikia tangazo hilo la maandamano ya amani kwa kuweka doria kali sehemu mbalimbali za miji na wamethibitisha kuwakamata zaidi ya wafuasi 40 wa chama cha NUP waliokutwa wakishiriki maandamano.
Chanzo: DW