Uganda wanakimbia Tanzania wanatembea

Uganda wanakimbia Tanzania wanatembea

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
Habari za weekend wadau mapambano yanaendele tulipe tozo kwa ujenzi wa taifa letu na maendeleo ya SINGIDA BIG STARS,
ikiwa umepita mda mchache toka kumalizaka kwa mechi kati ya Tanzania dhidi ya Uganda huku Tanzania ikiambulia kichapo cha goli moja kwa nunge ila mzee mwinyi alitukosea sana.

Yeye ndiye aliyetupa jina la kichwa cha mwenda wazimu hajakosea maana aliona mbali sana wachezaji wote walio Tanzania kweli tunashindwa kupata wachezaji 11 wa kuliwakilisha taifa mpaka leo licha ya jitihada mbali mbali zinazofanywa na wadhamini na wadau wa soka.

Ukiangalia mpira wa leo wachezaji wa Tanzania hawajulikani ni mda gani wanashambulia na mda gani wana kaba maana wakiwa na mpira wanatembea wakiwa hawana mpira wanatembea wakati huo wapinzani wao wanakimbia mda wote wakitafuta ushindi wachezaji wanacheza kama hawajala leo chakula cha mchana inasikitisha kwa kweli ndio maana mzee wa chato kipindi chake alitaka achague wanajeshi waende kuwakilisha taifa.

Uganda wana project ukiangalia wachezaji wao wote ni below 30 and 25 muangalie yule goal kipa muangalie yule aliyetufunga goli wenzetu wamewekeza na wanawaamini vijana na kuwapa nafasi bado sisi tunapambana na kina mkude pamoja na kina lyanga huku vijana tukiwaacha kwenye ujenzi wa national team,
sisi ndo wazee wa zima moto tunaokota okota tu wachezaji bora awe simba au yanga ndio maana wengine wamechukuliwa national team lakini katika vilabu vyao hawachezi tunaita majina badala ya performance yaani imagine mchezaji kama tepsie Evans alikuwa ameachwa ila walimuita baada ya wadau kulalamika na kupaza sauti mitandaoni sisi ni wa kumtegemea mpole na kibu Denis pamoja lusajo wachezaji walio ukingoni mwa career yao ni upepo uliwapitia basi ila hawana maajabu.

Kama ni mgomo huu wa leo ni wa chuo kikuu kugomea nyongeza ya pesa ya kujikimu wachezaji hawakabi wana mark mtu kwa macho wakiwa na mpira hawafunguki na hakuna anayehangaika kumuomba mwenzako mpira au kuwa karibu yaani hawana tofauti na wachezaji wa chandimu it was totally disorganized formation and players.

watanzania tunapenda mpira ila wenye mamlaka hawatilii maanani mapenzi yetu juu ya mpira wanaendeshwa na siasa na mahaba kufungwa kupo ila sio kizembe kama leo kwenye mechi ile kuzidiwa kupo ila sio kama leo kwa uchezaji ule hakuna sehemu hata moja yenye nafuu kila kitu kinaendeshwa kienyeji enyeji hakuna mipango hakuna mikakati tunasubiria maajabu kweli hii ndo Tozonia.

NB: paulsen sio kocha wa kuisaidia Tanzania kocha anakuwaje mzito kufanya maamuzi na substitution umri umemtupa mkono akae pembeni apishe wengine wajaribu kukipa darasa kichwa cha mwenda wazimu.
 
Wapo uwanjani kimwili kiroho wanawaza tozo....
 
Back
Top Bottom