Uganda yaanza kutumia Bandari ya Dar es salaam kusafirisha mafuta

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274

Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC) limetangaza kuanza kutumia Bandari ya Dar es Salaam katika kupakia bidhaa hiyo kwa ajili ya kupeleka nchini kwao.

Awali UNOC ilikuwa ikitumia bandari ya Mombasa nchini Kenya katika kuchukua bidhaa hizo huku ikisafirisha kwa kutumia Shirika la Bomba la Kenya (KPC).

“Uganda imepanga kusafirisha takriban lita milioni 36 za mafuta kila mwezi (mizigo 1,028 ya lori) kupitia bandari ya Dar es salaam, “imeeleza taarifa hiyo ya UNOC iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Proscovia Nabbanja

Hata hivyo, UNOC imesema kiasi hicho kinatarajiwa kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

“Kundi la kwanza la lita milioni 18 (malori 520 ya lori) za mafuta zilianza kupakiwa wiki hii jijini Dar es Salaam na litawasili Kampala siku zijazo,”imesema taarifa hiyo.

Makubaliano kati ya Bandari ya Dar es Salaam na Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC) yalifanyika Mei 24 hadi 25, 2024 wakati wa Mkutano wa Pili wa Biashara kati ya Uganda na Tanzania uliofanyika Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, nchi hizo mbili zilikubaliana kuboresha njia za usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyingine kupitia Bandari ya Dar es Salaam badala ya Mombasa, Kenya.

Uamuzi huu ulifikiwa kutokana na mabadiliko ya kiufundi na gharama katika usafirishaji wa mafuta kupitia bandari ya Mombasa, na hivyo Uganda ikaamua kuongeza matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam kama njia mbadala ya usafirishaji wa mafuta.

Katika mkutano huo, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Doto Biteko alisema lengo la makubaliano ya mkutano huo ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi.

Snapinsta.app_455187570_1329149061379220_8778512683712915847_n_1080.jpg
 
Safi kabisa
 
Ewe Mwenyezi Mungu Muumba Mbingu na Ardhi MREHEMU kiongozi wetu na Rais wetu Al Marhum John Pombe Joseph Magufuli aaamin aaamin aaamin [emoji7]

Lifanye kaburi lake liwe miongoni mwa mashimo yaliyoko peponi ,aaamin aaamin [emoji2956]

#JMT Kwanza[emoji2956]
 
[emoji2956][emoji2956]
 
Museveni hua anaipenda Tanzania sana na anaiunga mkono na kila penye fursa hua anatupatia, akiishi mikocheni ndio muhoozi alizaliwa pale
 
Kumbe alikuwepo kwenye makubaliano yaliyofanyika mei 24 hadi 25 2024! Hongera kwake.
 
Museveni hua anaipenda Tanzania sana na anaiunga mkono na kila penye fursa hua anatupatia, akiishi mikocheni ndio muhoozi alizaliwa pale
Kuna fala hapo juu kamsifu magufuli kuwa ndiye kasababisha hili,hii nchi ina misukule mingi!!
 
Museveni hua anaipenda Tanzania sana na anaiunga mkono na kila penye fursa hua anatupatia, akiishi mikocheni ndio muhoozi alizaliwa pale
Kabila Joseph mbexi beach

Maisha hayaaaaa

Nimekunywa naoo sana Rose Garden enxihizooo na raisi waburundi nkurunzinza sema sikusoma nyakati

Wanakuja na mademu wanene wazuri sijui mamazao sijui dadazo achatu

Sahizii kila naemwona bar namliaa timing uwezijua keshoyaako
 
Back
Top Bottom