BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Serikali ya Uganda imesema inapanga kuongeza umri wa unywaji pombe kutoka miaka 18 hadi 21 ili kukabiliana na unywaji pombe unaopita kiasi.
Akiongea katika kongamano la pili la Wakuu wa Kitaifa 2023, tukio lililolenga kuandaa mikakati ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kwa Wanafunzi nchini Uganda, Kamishna wa Wizara ya Afya, Afya ya Akili, Pombe na Dawa za Kulevya, Dkt. Hafsa Lukwata amesema dhamira ya sheria hiyo mpya ni kupunguza idadi ya Watu wanaonunua pombe.
Kwa mujibu wa Afisa huyo ikiwa Mtu hatumii kilevi chochote kabla ya kufikia umri wa miaka 21, uwezekano wa kunywa pombe kwenye maisha yake hupungua mpaka 48%.
Kulingana na ripoti ya mwaka 2023 iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa wastani, Raia wa Uganda hutumia lita 12.21 za pombe kila mwaka na Wanaume hunywa pombe nyingi zaidi kupita Wanawake ambapo Wanaume hutumia wastani wa lita 19.93 za pombe safi kila mwaka ikilinganishwa na lita 4.88 kwa Wanawake.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa vifo milioni tatu (5.3% ya vifo vyote) Ulimwenguni pote hutokea kila mwaka kutokana na unywaji pombe. Shirika la Afya duniani WHO inasema unywaji pombe kupita kiasi ndio sababu kubwa ya magonjwa zaidi ya 200 Ulimwenguni.