#COVID19 Uganda yasitisha matumizi ya Vitamin C kutibu COVID-19

#COVID19 Uganda yasitisha matumizi ya Vitamin C kutibu COVID-19

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wizara ya afya nchini Uganda imesitisha matumizi ya vitamin C katika kutibu virusi vya Covid-19 kutokana na matumizi mabaya ya wagonjwa.

Vitamni C ndiyo moja ya dawa zilizokuwa zinatumiwa kWa wagonjwa wa covid-19 nchini Uganda kwa sababu zinasaidia kuendeleza chembe hai nyeupe (White blood cell) kupambana kuondoa virusi.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya afya wanaoshughulika na masuala ya utafiti, wanadai vidonge vya vitamn C vinapatikana kwa urahisi na hivyo watu hutumia kiholela kupita kiasi na kuleta madhara.

Daktari Misaki Wanyegera ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kupambana na virusi vya corona katika wizara ya afya nchini Uganda, amesema walichukua hatua ya kuondoa Vitamic C baada ya wagonjwa hospitalini kukutwa wakitumia hovyo vitamin hizo na kusababisha figo kushindwa kufanya kazi kutokana na matumizi mabaya.

Kulingana na ushauri wa madaktari, matumizi ya Vitamin C kwa mgonjwa wa mafua ni tembe 2 kila baada ya saa 8, lakini watu wanatumia mara tatu ya hizo.

Mwezi Januari kulikuwa na ukosefu wa Vitamin C za Gramu 100 kote nchini humo kutokana na matumizi mabaya.
 
Mfamasia fulani alituambia kwamba utunzaji hafifu wa vidonge vya Vitamin C huvifanya viwe makapi tu by the time mtu anavikuta dukani. Ndiyo maana mimi binafsi navikubali zaidi supplements za Vitamin D.

Mbinu Binafsi dhidi ya Corona
 
Inatakiwa tuwashauri waje kukaa Bongo wale matunda
 
Back
Top Bottom