Pain killer
JF-Expert Member
- Aug 15, 2017
- 14,361
- 21,680
Watasituka badae sanaWizara ya afya Uganda imetangaza Visa vipya 31 vya Covid 19 baada ya sampuli 1,116 kupimwa na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253, wagonjwa 23 ni kutoka mipakani kati yao 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na 4 Wakenya, wote wamekabidhiwa katika nchi zao. Kwanza TV on Twitter
Huwezi wapangia. Ni serikali yaoUganda ajifunze kukaa kimya
Kila Nchi ina taratibu zake, mzee mseven ajifunze kwa Kenyatta
Wizara yao haiko responsible kwa serikal ya Tanzania. Iko responsible kwa serikali ya uganda.Anatakiwa akabidhi reports kwa wizara ya Afya upande wa Tanzania
Kuna mtu alishatoa wazo kama hilo. Ila mpaka sasa naona serikal hailifanyii kazi. Sijui wameridhika na haliHuu ugonjwa sasa unasambazwa na madereva wa malori....kwanini serikali isifanye hata jitihada kuwapima hawa madereva.
Tumeshawaelewa nia ya kutokutangaza maambukizi....kazi tunawaachia majirani kutuumbua tu kila siku.
Huku tuna ambiwa yamepungu jamani!Uganda imetangaza Wagonjwa 31 wapya wa #COVID19 waliopatikana baada ya sampuli 1,116 kupimwa ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya jumla ya maambukizi kufikia 253
Wagonjwa 23 ni kutoka mipakani ambapo sampuli 896 zilichukuliwa na 8 ni waliopimwa wakiwa Karantini baada ya kukutana na madereva waliotangazwa awali kuwa na #CoronaVirus
Wizara ya Afya nchini humo imesema katika ya wagonjwa 23 waliopatikana mipakani, 20 ni madereva wa malori ambapo 16 ni Watanzania na wanne ni Wakenya. Wote wamekabidhiwa kwa nchi zao
Aidha, Wizara imebainisha kuwa hadi kufikia sasa jumla ya Wagonjwa 69 wamepona
Juzi hapo walikuwepo madereva wa malori kama 800 Wanapimwa mabibo,au una maanisha kupimwaje?
Kwani kuna shida gani kama kwenye gari kunakuwa na watu wasiozidi 2?Wakapime mipakani. Dereva akipimwa Mabibo inaweza kumchukua siku hadi tatu kabla hajafika Mutukura. Hapo katikati anaweza kuambukizwa! Tujitahidi kuthibitisha kwa nchi jirani kuwa madereva wetu ni salama. Mpakani!!